Bila shaka ninyi sio wahusika na wala hayajawakuta ila haya mnayoeleza ni maneno tu ya kuambiwa, kusimuliwa, na kusikia kuwa ooh ni vile na hivi basi. Ila kiuhalisia hao wachawi wenyewe utawakuta wapi ? Zaidi ya kutishana tishana tu kwa masimulizi ya kusikia kama ivi mnavyofanya.
tatizo huwa siyo kwamba wachawi hujificha kwa sababu mambo yao ni ya siri, la hasha, isipokuwa kwa kuwa hao wanaoitwa wachawi "HAWAPO". Na huo unaodhaniwa kuwa ni uchawi "HAUPO"
tumebaki na kelele tu, “Kuna wachawi na uchawi”, “Kuna wachawi na uchawi,” “Kuna wachawi na uchawi”. Tukiulizana wako wapi wachawi wenyewe. Tunabaki kusema, “Oh, hayajakukuta”, “Oh, yakikukuta utajua” na kadhalika.
Kifupi, watu tumebaki kudhaniana dhaniana tu na kutoa mifano ya mbali kwa mbali. Ukizungumza na watu wa Lindi watakusimulia hadithi za Sumbawanga au Mwanza. Ukienda Sumbawanga utasimuliwa habari za Malawi. Ukienda Mwanza utasimuliwa hadithi za Tanga na Msumbiji. Ukienda Kenya utasimuliwa habari za Tanzania na India. Ukiishi Tanzania utasimuliwa habari za Kongo na Nigeria.
Kiuhalisia ukiamua kufuatilia au kutafiti hata ninyi mwenyewe ni kuwa mtaishia kukutana na hadithi hadithi tu au na vituko vingi. Vingi ya vituko hivyo utaambiwa vilitokea mwaka juzi au miaka mingi iliyopita. Vituko vyenyewe wala haviwi vya pekee sana, vingi vyake huwa vyenye kuelezeka tu na vingi ya hivyo utakuta ni "ujanja ujanja" tu na mambo ya kufanyiana "timing" basi. Na vichache kati ya hivyo ni mambo yanayoelezeka kisayansi.