Hakuna mchawi anayechanja chale watu usiku, acheni kulalia vitanda vichafu.

Akili za watu wanaoamini uchawi!!!?
 
Huu nao ni utoto tu ukikua utaacha.
 
Bagamoyo niliwahi amka nimechajwa mwili mzima
Sitasahau

Nb mimi sio muumini wa imani za kishirikina kuanzia wazaz mpaka mimi

Mkristo
Mluther
Walau wewe ni muhusika na sio wa masimulizi.

Baada ya kuamka na chanjo mwili mzima namna hiyo je, ulijaribu kufuatilia nini sababu ? Mfano kwenda hospitali labda kujua tatizo kwa vipimo vya sayansi ya afya nk.
 
Huu nao ni utoto tu ukikua utaacha.
Unaamini kuna watu hupaa na ungo, halafu wakifika wanakokwenda wanapita ukutani bila kuonekana wakiwa wamebeba viwembe na muda mwingine wakiwa uchi kisha wanachanja watu?
 
Moja hapa kuna watu wasiojua kuchanjwa na mikwaruzo. Mikwaruso itabakia mikwaruzo aidha sababu ya kujikuna, au babau yeyote ile.

Ukisikia kuchanjwa ni kitu kina pattern, yaani mtirirko kama mara tatu sehemu moja , inaenda tena mara tatu sehemu inayofuatia.... hata sehemu 10 tofauti kwa mtirirko wa 3..3....

Mimi ukweli sijawahi kuchanjwa ila nimeshuhudi watu 3 tofauti na wawili waliacha kazi waliyokua wanafanya maana ilikua kila mwezi lazima wachanjwe...

Kuhusu mtu kulala ndani na kujikuta nje huku milango yote imefungwa(yupo nje na boxer) ikabidi amgongee mkewe amfungulie na mkewe anashangaa walilala wote iweje yupo nje.

Haya mambo au hii dark science ipo sana
 
Hamna anayechanjwa na wachawi. Hiyo inaitwa dermatographia, yaani ni kama mtu anaandika kwenye ngozi hivyo kunakuwa na pattern kabisa. Hao wanaodai kuchanjwa waliona hata damu kwenye mashuka? Au watadai wachawi waliokuja na ungo wameondoka nayo? Kifupi ni kuwa ujinga ndiyo unatufanya tuamini mambo haya.

Mtz akiona hivi asubuhi atasema wachawi walikuja wakamchanja.



 
Bila shaka hao kituo cha kazi ilikuaa ni kijijini au ndanindani huko. Hao ni itakuwa walikuwa wamatafuta sababu za kuacha kazi, au kuhakimishwa kituo cha kazi, labda wahamishiwe mjini nk.

Hawana tofauti na tukio moja la waalimu fulani kwenye kijiji fulani ilitoka hadi kwenye taarifa za habari wakieleza mbele ya mkuu wa wilaya mambo wanayoyaita kuwa ni ya kichawi wanayofanyiwa hapo kijijini ikiwemo kujikuta wamelala nje, wamechanjwa na mwingine mke wake kujifungua vitu vya ajabu ajabu sijui matikitiki maji yenye shanga kama sikosei nk. Ila zote izo ilikuaa ni sababu tu za wao kutaka kukimbia mazingira ya kijijini.
 
SAwa kwakuwa bado hujakutana nao au hujakutana nayo hayo maswahibu ila kwa ss tunaokaa uswahikini tunaishi na wachawi na tushawah kushuhudia matukio hayo au kuyapata kabsa huwez kuelewa mpka sku uone kwa macho
 
Kuna rafiki yangu mmoja naye haamini sana hayo mambo, sasa siku moja alijikuta kwenye mabishano na bibi mmoja ambaye watu wengi wamekuwa wakimuita mchawi.

Watu walimfata kumwambia ajishushe ili bibi asiweze kumroga lakini jamaa alikuwa ni mtata sana.

Basi kuna mchizi mmoja akamuambia leo night jiandae kupokea mgeni sababu hii bifu haijaishia hapa lazima ukabwe.

Jamaa alimjibu kuwa kama grand ni mchawi basi leo night ndio nitashuhudia mwenyewe, si mnasema wanakuwaga uchi wa mnyama wanapokuja kukukaba wanakukalia kwa juu?

Basi leo navua nguo zote halafu nalala chali huku mzigo ukiwa umesimama, grand akijichanganya akatua vibaya tu atajikuta ameukalia
 
Kuamini sorry za kishirikina/uchawi ni kiwango cha chini kabisa cha uwezo wa kufikiri yani zwazwa
 

Mitanganyika kitu chochote ambacho hawajui wanasema ni uchawi hawataki kuumiza vichwa
 

Word. Story zote za uchawi ni hearsay, watu wanaamini kama zilivyo nao wanaanza kusimulia. Inabidi uwe zwazwa kuamini hizi story
 
Mtu akiamka akakuta hivi atasema wachawi wamemchanja usiku. Inaitwa dermatographia.

Nyembe kabisa nilikuja gundua wakati naoga asubuh mwili unawasha sana
Kutoka bafuni nikaenda kujikagua mwili ndani kuangalia
Nyembe zimepita za kutosha na ile siki nililala na jinsi nimerdi gheto sa 8 usiku nikajilaza mazima

Na jinsi haina tobo hataaa
Nikampigia simu antie yangu Moro ye ni mtu wa kusali sana akasema mwanangu utakuwa husali huko bagamoyo lazma

Nikakausha
 
Walau wewe ni muhusika na sio wa masimulizi.

Baada ya kuamka na chanjo mwili mzima namna hiyo je, ulijaribu kufuatilia nini sababu ? Mfano kwenda hospitali labda kujua tatizo kwa vipimo vya sayansi ya afya nk.
Hapana sikwenda hospital manake niliwaza naelezaje aibu hii

Alama za nyembe mwili wote
 
Bagamoyo ni wachawi we dada acha afu kule sio mpaka uwachokoze
Wanakuchezea tu tofaut na wafipa mpaka umchokoze
 
Ni kama conditions hapo juu au ulipitiwa na allergic reactions. Uliona damu zilizotokana na kuchanjwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…