mamad.
Ni hivi, wanawake wengi wamejingewa au wamejijengea woga kuhusu mitaala kutokana na uchoyo na ubinafsi tabia ambayo ni asili ya binadamu, mfano ni asili ya binadamu kuogopa kifo huku anatamani kuingia peponi, utapataje pepo bila kufa??!!.
Katika Uisilamu ndoa ya mitaala inalo sharti moja la UADILIFU, mume anapokuwa na HAJA au ulazima wa kuongeza mke ni lazima ahakikishe kwamba atawatendea mahitaji yao kwa uadilifu kama hatoweza uadifu Qur'an inasema; Ni BORA abaki na mmoja vinginevyo kwake mitaala itakuwa ni kiwanda cha kujitengenezea madhambi.
Ni Zipi Haja na faida za kuoa mke zaidi ya mmoj:-
1-----Wanawake ni wengi duniani kuliko wanaume, Mungu hakuumba hivyo kwa makosa bali makusudio maalumu kuendeleza uzao wa watu duniani inabidi uwiano uwe hivyo na hata kwa wafugaji wa ng'ombe, kuku nk, ili kuendeleza uzao kwa mifugo yao utakuta Madume mawili kwa majike wengi au jogoo mmoja kwa makoo wengi nk.
2------Kulinda heshima na hadhi ya jamii; ni hivi heshima ya jamii ni pamoja na maisha ya staha ya watu wake, sio staha wanawake wawe wengi mitaani wakirandaranda bila kuolewa, hatari yake ndiyo vyangudoa na ukahaba na madanguro kuongezeka na watoto wasiokuwa na baba kuongezeka na hao watoto wakikosa malezi wanakuwa vibaka na wavuta unga nk, katika ukahaba ndimo magonjwa ya zinaa yatapatikana na kumbuka wateja wa hao makahaba ndio hao waume zenu mnaowatisha wasioe mke mwingine zaidi yako, unakataa mke mwenza unapokea Ukimwi na Hepatitis nk.
3----- Kumbuka wanawake wanaoranda mitaani kwa kukosa kuolewa hao ni ama mdogo wako, mtoto wa ndugu yako, mama yako mdogo, shangazi yako na hata anaweza kuwa ni mwanao, je unaweza kuwa ni mtu mwenye furaha kuona mwanao au nduguyo yeyote anaranda mitaani kutafuta wanaume wa kukidhi haja zake za kimwili kwakuwa tu hakuolewa???
4----Wanaobomoa ndoa za mke/mme mmoja ni nyumba ndogo, ushahidi uliopo ni kwamba ndoa za mke/mume mmoja zimekuwa zikibomoka kutokana na nyumba ndogo, mume ananogewa na nyumba ndogo mwishowe anatelekeza nyumba kubwa, yote hii isingekuwepo kama nyumba ndogo "zingehalalishwa" kupitia mitaala.
5-----Maradhi kwa Mke, inaweza kutokea mtu kaoa mke baada ya muda fulani mke akashikwa na maradhi ya kudumu kama ya kigenetic nk, na akashindwa kabisa kumuhudumia mumewe hapo mitaala inaswihi ili huyo mke mwenza aje kuwahudumia wote mume na mwenzake aliyekuwa mgonjwa, haitakuwa ubinadamu kumpa talaka huyo mgonjwa na kuoa mke mwingine.
6----- Kukuza uzao, mara nyingi inatokea watu wanaoa wanawake tasa na inapogundulika hivyo basi mitala inaswihi ili kuendeleza uzao, mke tasa sio ubinadamu kumpa talaka.
7-----Kukuza uzao wenye vipaji vingi, mbali na malezi kuna vipawa watu huwanavyo kutokana na vinasaba hivyo mitala ni njia mmoja ya kukuza uzao wenye vipaji kadhaa.
8--- Kukidhi haja za mume, lazima tukubaliane kwamba kuna wanaume wengine wana nguvu kubwa sana katika tendo wameumbwa hivyo na Mungu, watu wa aina hiyo wanapoweza kutimiza like sharti ya mitala basi ni ruksa kuongeza mke ili kumpunguzia "mzigo" mke mmoja na ili asiwe na nyumba ndogo.
NB: Wanawake wenye khofu na Mungu na wanaojua faida ya mitala hao ndio wanaoweza kuolewa na amani ikapatikana ndani ya nyumba na sio wale wanawake wenye tamaa ya matumbo yao na tamaa za watoto wao, wanawake wa aina hiyo ya tamaa katika nyumba ni kama jehanamu ndogo, hawafai katika mitala.