Hakuna mwenye akili timamu atakayemuamini Mbowe na Chadema kuchangia hela? Kwanini hazindui ujenzi Arusha au Moshi?

Status
Not open for further replies.

πŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎ Ahsante sana Mkuu.
 
Akili za Mbowe ndiyo akili za Chadema wote, na ni vigumu kutenganisha Chadema na Mbowe yeye ni mwenyekiti wa maisha, na Mbowe sera yake ya sasa ni mapambano na maiti tu sasa ukisema hawa ni nyumbu unatukanwa kama nini.
Akubali ukuzima uchungu, Chuma kishaenda, Chuma kilimkalisha na kumfanyia mambo, ajikaze, kusahau, mbona yupo salama mengine ni siri yake, sasa anapo pambana sana na maiti au marehemu atatufanya tuanze kujiuliza maswali na kujua ya ndani sisi hatutaki. Sijui chuma kilimfanya nini maana kilikuwa na kama kauhuni hivi.
 
Kama ana hasira aende akapambane na kaburi la magufuli, ili hasira ziishe lakini kwa huku ni uzushi tu.
 
Wacha awaeleze watanzania madhira waliyo pambana nayo wakati wa utawala wa mwendazake.

Historia ni mwalimu mzuri sana maishani na ndiyo maana mwendazake aliamua somo hilo kuingizwa kwenye mitaala.
 
Huwezi kuanza kufundisha hesabu bila kuanza na moja.
Mbowe anajua nini anafanya maana msingi wa hayo mambo yote uliyotaja lazima uanze na chimbuko.
 
Upendo huonya. Safi!
 
Sure, sure kabisa... Mbowe jikite sasa katika current issues... Achana na mwendazake... Kwanini upo bize sana kupigana na marehemu?
 
mwanangu ungebelance vina vya mwisho ningetoa bonge la track kwa vina vyako
hahahahhha.......................... maaana inaonyesha kuwa mwenyekiti wa kutoka rombo anademka
 
Haya ni mapambano ya mageuzi, Wilaya zetu Kilimanjaro tume changia kwa miaka 27 taktibani sasa, kwa hiyo tupunzike kidogo Same Mwanga, Vunjo, Rombo, waliya ya Moshi, Hai na Siha wacha tupumzike, na hata kura zilionyesha hivyo.
Tutaona uchaguzi ujao.
 
Ndiyo kazi aliyopewa na wazungu na wana CCM MASILAHI hawezi kuacha kutaja hilo jina
 
Kwanza ninaamini Hana ushahidi wa anachokisema,

Pili, amekuwa na siasa za chuki na kichochezi zisizovumilka kwa kila mtanzania mwenye akili timamu na mwenye kupenda amani na utulivu

Tatu, mpeni miezi mitatu tu Mbele, tayari itajidhihirisha kwamba dishi lilishaanza kuyumba kitambo tu, si bure hapo alipo

Na kama JPM kama anavyodai bwana Mbowe kwamba alikuwa na agenda ya Siri kuhakikisha kwamba Sisi wachaga hatupati ajira serikalini, na wakati Mimi nimepata ajira yangu miaka mitatu tu nyuma Kwa serikali hiyo anayosema wachaga hawakutakiwa kupewa ajira na serikali ya JPM, huo ni uwongo, Kwa vile yeye anadai serikali ya JPM ilikuwa na agenda mbaya Kwa wachaga tena Ni kwa Siri, ameshindwa nini naye kulifanya Jambo hilo kuwa ni la Siri Kwa sababu Kwa kufanya hivyo, litatuweka kwenye Amani Yetu na kudhihirisha hekima ya bwana Mbowe na kama mkongwe wa siasa za kimageuzi nchini??

Kwa nini yeye atamke waziwazi Mbele ya kada mnasi na wakati huohuo akijua aliyekuwa akifanya Jambo Hilo tayari hatuko naye duniani, amejiuliza taharuki inayoweza kutokea ambapo hata mwenye chuki na wachaga hayuko duniani,

Bwana Mbowe atapata faida ipi Sisi wachaga Tulianza kunununiana na wasukuma ili Hali mgombanishi wetu hayupo?

Kwa nini hakutaja kulimeza Hilo Jambo ambalo Kwanza ninauhakika πŸ’―% sio Kweli Bali chuki zake tu zilizosababishwa na ukwepaji Kodi wake?

Ogopa Sana mwanasiasa anapoelekea mwisho wa umarufu wake na mwisho wa kukubalika kisiasa, huamua hata kuchonganisha jamii ili ajipatie umarufu wa kijinga na kipumbavu kama anavyotaka kufanya huyu mkongwe wa siasa za upinzani aliyejizolea umaarufu kipindi cha JK.

Mbowe anaelekea kubaya, mpeni miazi yake mitatu tu muone anavyovurugikiwa kichwani!!

Mbowe hawezi kuongoza watu wa Kada mbalimbali kutoka pande za Tanzania, Isipokuwa Uongozi wake inafaa aongoze watu wa kanda yake

Anasema maneno magumu Mbele ya wasukuma ambao nao wamo ndani ya Chama chake??

Hao wasukuma waliomo chamani kwake wanajisikiaje kusikia eti utawala uliokuwepo wachaga pekee hawakupewa ajira, Wakati kina mnyika mpaka Leo hii hata mishahara hawalipwi na chadema Kwa muda sasa, Magufuli kama msukuma, alishindwa nini kumfuata mnyika ili ampe hata ukurugenzi Kwa kuwa ni msukuma?

Mambo ya kipuuzi Sana haya
 
Ila Mbowe ipo siku atasababisha watu kujinyonga, chadema ni imani pamoja na KADI za viwango tofauti wapo pia wanachama watapenda changia mpaka mamilion,na tegemea hizo KADI za laki mbili kuchukuliwa Sana kuliko zingine
Tumehubiriwa bila matokeo kwa miaka 32 sasa na hata wengine tuli fukuza chuo mwaka 1994 na UDSM kufungwa wote kufukuzwa.

Kuchelewa kupata matokeo na mabadiliko yemefanya munkari wa mageuzi upungue nguvu sana. Na sasa hivi mtu yeyote akwambiae Chadema ina nguvu Kilimanjaro kama ilivyokuwa zamani anakudanganya.
 
Kwa heshima aliyonayo ,mh.Mbowe AJITOKEZE kutuomba msamaha watanzania....

Kama Mzalendo Kiukweli maneno aliyoyasema YAMETUUMIZA KUPITA MAELEZO....

Mh.Mbowe AMEJIFEDHEHESHA MNO...na kwa heshima yake ni bora tu akakubali amekosea.....

#KaziIendelee
 
Wasiliana na ndugu zako wa karibu, waulize wanakuonaje.

Nina hakika unakotakiwa kuwa ni hospitalini. Na sijui kama tuna hospitali nyingine zaidi ya ile Milembe Dodoma.
Kule awali nilionya kuwataka wenye akili timamu wamsusie huyo anayeelekea mwisho wa siasa zake, sikulenga wewe na wote wenye akili ndogo kama zako, hivyo wewe endelea
 
Wacha amseme kamuumiza sana kibiashara kafungia gazeti lake, kavunja hoteli bill, kaharibu shamba la maua, kampora ubunge, kafungia account zake pamoja na kuchukua fedha kiinua mgongo, wew ufanyiwe yote hayo usiseme yeye ni mwanadamu pia.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…