Hakuna siku ngumu kwa mzazi kama ya kumpeleka shule mtoto kwa mara ya kwanza

Hakuna siku ngumu kwa mzazi kama ya kumpeleka shule mtoto kwa mara ya kwanza

huruma sio malezi ,waacheni wakomae mbona sie tulikula sana mboko na tulivyofika vidato vya juu tukawa tena ndio vinara hata kuhamishwa shule hatutaki tena , ni kama jeshi lazima wapite, ten kwa vishule vyetu vya kisikuhizi kila kitu wanafanyiwa hakuna shida.
 
Huwa ni siku ngumu sana kwa mzazi kumpeleka mtoto shule kwa mara ya kwanza , umeshakaa na mtoto miaka 3 / 4 hajazoea na haujazoea mtoto kukaa na watu baki , yeye amezoea kukaa mazingira ya nyumbani na wewe umezoea kumuona akiwa home muda wote . So day one inakuwa ngumu sana watoto wengi wanakuwa wasumbufu wanalia , mtoto anskuwa hataki umuache shule
Ni kweli lakini baadae anazoea.
 
Siwezi kusahau mwaka 2002 nilichaguliwa kujiunga darasani la Kwanza Shule Fulani pale Mara ilikuwa Ni kilometer 4 ivi kutoka home nilipelekea na mwalimu kisha akasahau wakati w kurudi akasahau kurudi na Mimi na njia ilikuwa na Kona Kona,aisee Ile siku ilikuwa ndo day 1, naikumbuka wakati WA kurudi nilipotea njia ya kurudi nyumbani nililia Sana Ile siku,wasamaria wema wakanipeleka Hadi kwenye Duka moja ivi ndo nikapata njia siwezi kusahau Ile siku
 
Back
Top Bottom