Hakuna Taifa linaloitwa Palestina liliwahi exists tangu dunia iumbwe kumbe

Hoja zingine ni za kijinga,kwani kabla ya 1961 kulikuwa na Taifa linaitwa Tanganyika?
Ila kulikuwa na watu katika eneo hilo ambapo badaye walikuja kupata uhuru na kuunda Taifa la Tanganyika.

Haiwezekani ukusanye watu kutoka eneo A uwapeleke eneo B kisha hao watu waunde Taifa,huku watu waliokiwepo hapo toka awali wakataliwe kuunda Taifa.
 
Tunawambiaga uku mtaani sisi bado tunasoma wanatukatalia....... tena sisi uku mtaani masomo yetu ni magumu sana atukalili ila lazima uwelewe🚢
 
Soma biblia kijana. Hawakuwa na nchi au sehemu yao maalum.

Wengine walikuwa wanaharamu wa Tamar ambae eti alizaa na baba mkwe wake alipofanya ukahaba, akaja kusingiziwa ndiyo kizazi cha Yesu.
Ni akheri usitumie Biblia kama unataka kusema hakukuwa na taifa la Israeli. Maana kuna mistari lukuki inayoonesha utaifa wa Israeli.

Sasa mtu kuzaa na baba mkwe umeona haiwezekani au? Mbona ni vitu vinatokea hata hapa Tanzania? Sio kila aliyetajwa kwenye Biblia basi ni kielelezo chetu leo. Hata Rahabu alikuwa kahaba lakini yumo kwenye ukoo wa Yesu, hiyo haina maana watu sasa ni ruksa kuwa makahaba.
 
Point
 
Wasamaria


Katika mataifa pia ilitakiwa waisrael wawafukuze kipindi waisrael wanarudi kanaani walikuwa ni wasamaria(palestina ya sasa)

Wao kwa makusudi wakaamua kuwaacha na Mungu aliawaonya kuhusu hilo.

Kwa mujibu wa kitabu biblia.

Japo sihalalishi huo ugomvi wa sasa ila huo ni ukweli.
 
Miaka yote hiyo uliyoitaja ya enzi hizo hakukuwa na taifa lililoitwa Tanzania, leo bila haya mnadai ni nchi yenu na mtailinda kwa udi na uvumba.
Si-support Palestine wala Israel lakini kwa sasa wote wana territories zao na wanastahili haki ya kuishi kwa uhuru.
 
Samahani Mkuu!
Unamaanisha Kuwa Wasamaria na Pelishit (Wafilisti) au Wapalestine ni Taifa Moja???

Kama Ni hivyo hauko Sahihi Kulikuwa na Wasamaria na Pia Kulikuw na wafilisti..

Wasamaria walikuwa jamii ya zamani ya Kiyahudi yenye imani zao na mila zao tofauti, na waliishi hasa katika mji wa Samaria na maeneo ya karibu katika Ufalme wa Kaskazini wa Israeli. Na wao Wanaamini Agano la Kale kama sehemu ya maandiko yao, lakini wanatofautiana na Wayahudi wengine katika mambo kadhaa ya kidini, ibada, kama vile wao kuamini kuwa Mlima Gerizimu ni mlima mtakatifu.
 
Tanzania Umeenda Mbali sana Taifa Linaloitwa Tanganyika tu halikuwepo 🀣🀣

Ambalo Limeanza mwaka 1961 na 1962 Likawa Jamhuri na mwaka 1964 April Taifa la Tanganyika Likafutika πŸ˜…πŸ˜…

Likazaliwa Taifa Jipya la Tanzania..

Na naunga Mkono hoja zamani walikuwa wakiishi pamoja kwa Amani nini kinachofanya sasa Wagombane maana walikuwa pamoja Tangu miaka yote hiyo aliyotaja kwenye historia yake
 
Kuna surah kabisa inaitwa banii israail/wana wa israel,ahadi iliambatana na masharti ambayo hayakutimizwa ukisoma hizo aya,najua umegugo ukakopi tu,halafu Quran Inasema musa alikua muislam si myahudi
Musa alikuwa muislam aaahaahaaa uislam huu wa juz juz hapa ambao muhamad muanzilish aliwakuta hata nduguze wakiwa wakristo aahaah huu huu unaoenezwa kwa mtutu wa bunduki au mwngne
 
Musa alikuwa muislam aaahaahaaa uislam huu wa juz juz hapa ambao muhamad muanzilish aliwakuta hata nduguze wakiwa wakristo aahaah huu huu unaoenezwa kwa mtutu wa bunduki au mwngne
Musa hakuwa Muislam na Jina lake halikuwa Musa
MUSA jina lake Ni Moshe hayo majina mengine ni Yaliyotoholewa..

Musa alikuwa Muisrael aliyefundishwa kwenye Dini ya Misri na kulelewa kama Mwana mfalme..
Na baadae Musa alikuwa ni Miongoni mwa Wakombozi wa BaniIsra..

Ila kama anamaanisha Musa alikuwa Ni Mu'Islam ni kweli Maana Islam maana Yake Ni Mnyenyekevu au Kunyenyekea Ni kweli Musa alikuwa Mnyenyekevu Mbele ya Mungu ila hakuwahi kuwa Muislm kama Dini
 

Nani alikwambia Musa alikuwa akiitwa Moshe?. Hujui kuwa Musa alikuwa na jina la kale la Wamisri?.
 
Sijakuelewa?

Kulikuwa na mataifa mengi tu ambayo yote ilipaswa yafukuzwe. Hata ukigoogle now.Palestine ya sasa ndio samaria ya zamani.
 
Nani alikwambia Musa alikuwa akiitwa Moshe?. Hujui kuwa Musa alikuwa na jina la kale la Wamisri?.
Missile of the Nation

Habar!
Kwakuwa Umeleta Mada Hii na Mimi niko tayari kukueleza Uhalisia wake!
Ni kweli kabisa Jina Halisi la Musa sio Moshe wala Musa yenyewe..

Jina la Musa Halisia alikuwa Akiitwa "Hapimose"
Wakati huo neno "Hapi" lilikuwa linaamisha "Maji" au "Mungu maji" au "Mungu kutoka Maji ya Mto nile"
Na Neno "Mose" Maana yake "Yeye aliyetokana na"
Au unaweza ukasema "mwana wa" au kwa wale wenzetu wa Tanzania Tungetumia majina kama "Mwana...", Kwa watani wangu Wasukuma wangesema "Ng'wana...." kwaKabila zingine kanda ya Ziwa wangesema "Nya..."

kwa Wazungu wangesema "Son of...." au "Child of.." etc..


Sasa Unapata Picha halisi sasa kwamba Jina halisi la musa Lilikuwa "Son of Hapi" au "Child of Hapi" au "The one Come from Hapi" au Simply "Born of Hapi"

Au Kwa tafsiri halisi "The one comes from water" au "the One comes from water God"

Majina ya Maprince wengi wa kimisri yalikuwa Lazima yawe na Root Ms au Mose kwa sababu waliamini Kwamba Prince hawi prince ila Mungu amemteua Kuongoza taifa..

Kina Moses wengine ni kama "Ramses" tafsiri yake "The one comes from God Ra" au Simply "Born of Ra"
Mwingine..Thutmose ("born of Thoth")


SASA ILIKUWAJE HAPIMOSE akawa MOSHE (AMBAYE WENGI WANAMFAHAMU KAMA MUSA/MOSES)

Usisahau kwamba Mlezi wa Hapimose (Yaani Yaya, Au kw Lugha Nyepesi Dada wa Kazi wa Hapimose) Alikuwa ni mama yake Mzazi,

So yeye Alikuwa Anamuita Musa Jina MOSHE kiebrania Na Ambalo ndilo limetumika Hata kwenye Biblia ya Kiebrania Mpaka leo..

Akifupisha Jina Hapimose kwa hiyo yeye alimuita Simply MOSHE akimaanisha "Aliyetolewa" au "Kutoa"

Hakuwahi Malizia Aliyetolewa kwenye Maji kwa sababu ilikuwa Ni kuabudi Miungu Mingine kama Huyo Mungu Hapi wakati wao kama Waebrania Hawakuwahi kuabudu Mungu mwingine kwahyo yeye Alikomea Kuita Moshe tu..

Na hilo ndo likawa Jina La Musa kwa Waebrania wote, Hata alipokuwa Anarudi nyumbani kueleza Kuhusu Jinsi mtoto anavyokuwa Alikuwa Akitaja Moshe na Sio HAPIMOSE..

Na hata Musa alipotoroka Misri alianza Kujiita Moshe badala ya Hapimose..

Nadhani umenielewa Ila kama una swali unaweza Kuniuliza
 
Sijakuelewa?

Kulikuwa na mataifa mengi tu ambayo yote ilipaswa yafukuzwe. Hata ukigoogle now.Palestine ya sasa ndio samaria ya zamani.
KWanini unasema Ilibidi wafukuzwe πŸ˜…πŸ˜…

Wangoni Asili yao ni Afrika ya Kusini,Amakonde asili yao ni Msumbiji, Wamakua Asili yao ni Msumbiji na Zambia, Wamasai asili yao ni Ethipia, Hakuna Kabila Tanzania Lililokuwa na Asili yake hapa..

Swali Baada ya Kupata Uhuru Tanganyika Ilibidi Tuwafukuze makabila ya Nje kwakuwa Yapo kwenye Ardhi yetu??

Pengine Hata Hatukuwahi kuikaa Ardhi hiyo ila Ni ardhi ya Kihistoria??

Nazungumzia Palestine/Paleshit/Ardhi ya wafilisti ni tofauti na Taifa la Samaria ambalo ni wayahudi waliokengeuka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…