Hali inayoendelea sasa Ndg Zitto, Mwigulu, Shonza, Nape, Mchange na Mwampamba wahojiwe

Hali inayoendelea sasa Ndg Zitto, Mwigulu, Shonza, Nape, Mchange na Mwampamba wahojiwe

Status
Not open for further replies.
chadema hakuna viongozi wenye nia njema na Taifa letu...
Dhamira yenu kubwa kwenye huu mchezo ni kujaribu kutuaminisha chadema hakuna viongozi wenye nia njema na Taifa letu. Kwa maana kuwa Chadema hawana taifa
 
Kumbe Mkuu Ben Huu ni mchezo uleule wa masalia ila sasa umefika mbali, nia ni kupandikiza uhasama na kubambika kesi ndani ya CHADEMA ili waweze kuwa na urahisi wa kuwashika wakuu wa chama ili wawabambike kesi kama hiyo ya Lwakatare ionekane wao ndio waliomtuma hasa Dr Slaa na Bwana Mbowe!!!
 
Mkuu The Boss, huyu jamaa simfahamu zaidi ya kumsoma tuu kwenye mitandao, sikuwahi kumfamu kabla ila gazeti la Jamhuri toleo la leo limeweka A-Z ya huyu jamaa, na pia wameiweka connectivity yake ya huyu Mkuu Ben, ndia maana nimesema "the guilt are afraid!", na msitegemee atasema lolote kuhusu kumjua Ludo!.

Kama Ludo ni kamanda wa kweli, aliyepikwa akaiva, atavumilia yote na kukubali kufa kizungu na tai shingoni!, lakini kama ni wa kuokotezwa, "the'll soon break him down na atasema kila kitu!, na amini msiamini, akifunguka!, hamtaamini!, kuna watu humu saa hizi wanatafuta pa kutokea!, dalili za mfa maji nimeishaanza kuziona!, nyie subirieni!.

Pasco.
Pasco, hapo kwenye red.
Unasema ulikuwa humfahamu kabisa huyu Ludo, lakini uliposoma tu kwenye gazeti la Jamhuri, (linaloandikwa na Manyerere aliyekuwa anashabikia kwamba Ludo akamatwe) habari zake, tayari haraka-haraka umekubali kuwa yaliyoandikwa na hilo gazeti ni kweli tupu bila chenga, na yamepelekea wewe kufanya conclusion kwamba "the guilty are afraid"!!
 
Last edited by a moderator:
Ahahahahah..Kamanda Ben unanifurahisha sana.Waonyeshe wewe ni jasusi uliyebobea hao vilaza.Kadri Mission inavyokuwa ngumu ndo umahiri wako unahitajika zaidi.Waonyeshe kwamba makamanda sio lege lege kama wala urojo waliokimbilia ndoa.We need intelligent boys like you.We need the heroes like you.Trust me, your ability and spirit will inspire many people and freedom is coming soon.Bravo Saanane,mimi si mwanachama wa chama chochote kile ila unanikosha sana na umahiri wako.Mungu azidi kukupigania mkuu.
 
Hii Movie Inachanganya sana, nahisi imeanzia Mwisho au tunachokiona sasa ni "Behind the Scene"... dawa ni Kupuuza kwanza ya sasa... staying tuned for the real and only One Original Reloaded Tanzania Politics Movie....
 
Duh,ujasiri wa Ben wakati mwingine nimejikuta namu admire.uwa wakati mwingine najiuliza huyu bwana mdogo anajiamini nini ? Kwa mfano suara ra Ludovick na deus Mallya nimependa aliyojibu na kuwaacha watu wakihangaika humu ila kitu nimenote ni kuwa kumbe Zitto inawezekana yupo nyuma ya huu mchezo akishirikana na akina mwigulu na kundi la Masalia?Ben ameamua kuwavaa tena kwa maneno yao wenyewe.Cdm jipangeni kukabiliana na hiri na kama kuna vijana jasiri sampuli ya akina Ben basi roho yangu imeturia

Mkuu JIBRIL,

Yaani hii ndio maana haswa ya thread hii ya Ben Saanane in a nutshell!
 
Last edited by a moderator:
Kabembe hapo Red hapo ni serious concern.....!
,
Hivi kumbe huu mchezo umeanzia mbali saana kwa malengo maalumu, huo uhusiano wa kina Zoka, TISS na Zito umelenga mbali ili kuondoa watu njiani kwa unafiki kupandikiza watu wao?? In millitary leadership we call it fifthy collum, a system within a system!!
Kwa hiyo wakuu wa CHADEMA hasa walengwa lazima walijue hilo kujihadhari kabla ya hatari. Sisi wengine tunajua kabisa CHADEMA ndiye tegemeo letu kwa ukombozi wa TZ!!! ZITAFANYIKA KILA MBINU NA HILA ILI UKOMBOZI USIPATIKANE TUENDELEE KUNYANYASWA. KUDHULUMIWA, KUIBIWA NA KUUWAWA!!! M4C MBELE KWA MBELE HAKUNA KULALA!!!

 
Jamani hivi ni kweli kua Lwakatare kaachiwa huru na mahakama?.
 
Huwa nashangaa mpaka haya mambo yanafikia hapa..full sintofahamu the so called 'Usalama wa Taifa' huwa wako leave au holiday?? Hii taasisi ingetafutiwa jina jipya..!
 
user-online.png
Mikael P Aweda
Today 10:36
#29 ​

JF Senior Expert Member
verified.png
Array


Join Date : 17th December 2010
Posts : 1,519
Rep Power : 6475
Likes Received1931
Likes Given1662​


icon1.png
Lwakatare aachiwa huru na kukamatwa hapo hapo Mahakamani kwa kosa lingine.


Taarifa nilizopata kutoka viongozi wa Chadema walioko mahakamani ni kwamba Lwakatare aliachiwa huru kutokana makosa 4 aliyokuwa ameshtakiwa nazo na sasa amekatwa tena hapo hapo mahakamani kwa kosa lingine ambalo halijajulikana.
My take.
Hata wakimbadilishia makosa tena, tayari imani ya wananchi kuhusu sakata hili itakuwa imeshapotea. kuna dalili ya mchezo mchafu wa kisiasa.​

Jamani ni nini kinaendelea? au ndio akili ndogo kutawala akili kubwa!
 
Acha uongo wewe! Evidence gani ulishaweka? Hebu niambie ulitumia utaalamu gani kugundua sauti ya asiye onekana tena kwenye clip yenye tatizo la sauti kiasi kile!
We ni mmoja ya wanamikakati kwenye hii clip natatizo lako ni kuropoka!
Huyu J. Shonza ni mropokaji sana, aliingilia kazi ya Manyerere Jackton
 
Pasco, hapo kwenye red.
Unasema ulikuwa humfahamu kabisa huyu Ludo, lakini uliposoma tu kwenye gazeti la Jamhuri, (linaloandikwa na Manyerere aliyekuwa anashabikia kwamba Ludo akamatwe) habari zake, tayari haraka-haraka umekubali kuwa yaliyoandikwa na hilo gazeti ni kweli tupu bila chenga, na yamepelekea wewe kufanya conclusion kwamba "the guilty are afraid"!!

Huyo ndio Pasco kama ulikuwa humjui
 
Last edited by a moderator:
Kwa kuwa kijana Mwenzangu Ben saanane umeamua kuwa mkweli,simamia ukweli si tu unaoufahamu bali uliopo.Mimi naamini uwongo hupotea lakini ukweli husimama.Kwa yanoyotokea sasa ktk siasa zetu ni kuonesha ni kwa kiwango gani kuyapata maendeleo ya kweli ni mgumu maana siasa zetu si za kujenga bali visasi,ghiliba na kubambikiana kesi.Mwenyezi Mungu akulindeni nyote wenye kusimamia haki na kweli.Simama imara Ben
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Ben Saanane upo vizuri sana mada imetulia japo wanafki wanajipofusha wenyewe na kutotaka kutumia akili japo kidogo,mapambano yanaendele tunawategemea katika kuendeleza misingi ya Taifa letu ,,kiujumla albam ya police ccm yenye wimbo wa lwakatare imegoma aiuziki mtaani watu wanackilizia M4C ipo wapi na kitu cha kanda ndicho kipo hewani kwa sana
 
Last edited by a moderator:
eight 8'oclock si ndo mda ambapo jua linakua kali...SASA HUYU JAMAA NI JUA KALI..LINACHOMA HASWA
 
WANAJAMVI,

NOTE:Haya hayahusu chama, ni jinai. Ingawa mimi ni mwanachama wa chama cha siasa na hawa wengine ni wanachama wa vyama vya siasa.Kwa hiyo demand za vikao vya vyama hapa ni irrelevant.Sasa;

Katika matamshi yanayoendelea kuandikwa kwenye mitandao ya kijamii na blogs kunihusisha na sakata la Mkuu wa Usalama CHADEMA na mambo mengine ni jitihada za maadui wangu na maadui wa CHADEMA kutekeleza malengo yao yenye nia ovu (evil). Katu,
kupitia mimi hamtaweza kuiangamiza CHADEMA. Mnaweza kunidhuru kimwili tu lakini nitaisimamia na kuipigania CHADEMA na taifa langu hadi tone la Mwisho la Damu.

Kupitia uanachama wangu kwa CHADEMA Kamwe msitegemea kosa lolote kutoka kwangu litakalowapa easy ride kwa mitego yenu. Kati ya watu wanaotakiwa kuhojiwa na jeshi la polisi kulingana na matamshi yao hadharani kwa sasa ni Mwigulu Nchemba, Juliana Shonza, Mtela Mwampamba, Festo Richard Sanga, Habib Mchange, Nape Moses Nnauyeili watoe ushahidi walio nao pamoja na ndugu Zitto Kabwe aliyedai kwamba alisikia mipango ya Mauaji inayomhusu yeye kutoka kwa watu waleee… Ahojiwe aeleze alisikia kutoka kwa akina nani. Najua watu wa Usalama wa Taifa mnapita hapa, Take Note (kama hamko katika hila hizi)


Jitihada za baadhi yao kutumia waandishi uchwara nitakabiliana nazo kwa haraka na kwa usahihi.


Jambo lingine,Kama Jitihada za kubambikizia kesi viongozi na wanachama wa CHADEMA zitaendelea ni dalili kwamba mbinu zile zile walizotumia makaburu Afrika Kusini ndizo zinazoelekea kutumika,natoa Rai kwa CHADEMA na kambi ya upinzani(wale wapinzani wa kweli) tujiandae sasa kutumia mbinu zile za Akina Nelson Mandela za Umkhontho we Sizwe(Spear of the nation) kupambana na ukaburu wowote utakaoinyemelea Tanzania.Kuna kila dalili ya kutaka ku-tarnish image ya wanachama,viongozi na CHADEMA kuwa ni chama cha KIGAIDI.

RED BRIGADE ichukue center stage kulinda viongozi na wanachama wetu pamoja na interest za chama popote bila kuvunja sheria lakini sheria itekelezwe bila bias. Hizi hila za kutaka kuchafua image ya chama ni mbinu ya kuwavunja moyo tu.Tusikubali.Vijana CHADEMA hatujawahi kuwa softy,siyo historia yetu, siyo falsafa wala itifaki ya Kombati kunyamazia haya.

Tukiwaonyesha woga wetu, itakua silaha imara zaidi kwao kutumaliza….



MWIGULU NCHEMBA
Huyu ni naibu Katibu mkuu wa CCM-Bara na katika matamshi yake ya tarehe 2 January 2013 kupitia kipindi cha televisheni kituo cha STAR TV alinukuliwa akidai anayo video inayoonyesha viongozi wa CHADEMA wakipanga mauaji.Ni jambo la ajabu mtu kuwa na video ya aina hiyo atangaze kwenye kituo cha televisheni bila kuipeleka polisi na kama aliipeleka kwenye vyombo vya dola ni kwanini hadi sasa hajahojiwa?Iko wapi hiyo video aliyosema alikua nayo?Ni kwa nini polisi hawakuchukua tahadhari hadi jambo hilo limetokea kama sio njama ovu za kuipaka matope CHADEMA?Taarifa ya matamshi hayo ililetwa humu ikajadiliwa na hakukanusha na aliendelea kusizitiza kuwa anayo video husika .Yakatolewa majibu ya ndugu Tundu Lissu na Ndugu Zitto kupitia uzi huu

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-wakipanga-mikakati-ya-mauaji-nchini-12.html


NAPE NNAUYE

Siku moja baada ya kuvamiwa Ndugu kibanda Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM aliandika hivi Kwenye ukurasa wake wa Facebook:

“Hili la kutekwa na kupigwa na kuumizwa kiasi hichi (hiki) kaka yangu Kibanda, kila nikilitafakari maneno ya waliosemahakutatawalika na makala za Kibanda mbili au tatu za mwisho kabla ya kuhama chombo cha habari kabla ya anachofanyia kazi sasa vinajirudia kichwani mwangu sana!


Je,hadi sasa vyombo vya ulinzi na usalama vimefanya nini kuhusu kauli hii maana huu ni ushahidi muhimu kwamba huyu anajua kinachoendelea.

ZITTO KABWE

Aliongelea kuwa (ana experience kuwa) kuna watu wanataka kumuua na haya yaliandikwa humu jamii forums siku chache kabla Mwigulu Nchemba hajatangaza kwamba ana video ya viongozi wa CHADEMA wanataka kumdhuru.Zitto alitangaza haya muda mfupi baada ya mipango ya kundi la MASALIA/PM-7 (kama linavyoonekana hapo kwenye picha isipokua Chege ambaye hakua Member) kutibuka.Kundi la PM-7/MASALIA lilitumiwa na Mwigulu Nchemba kabla hatujalilipua humu kwa ajili ya kukihujumu chama na ndiyo maana baada ya mipango kutibuka tu walikimbilia CCM kwa uratibu wa mwigulu Nchemba na Nape.Sasa kauli za kiuongozi wangu Zitto nazo zihojiwe maana inasemekana na hata yeye amekiri kwamba amesiki kauli hizi za kutaka kuuwa na wakati mwingine amekwepa na kuvuka hatari hizi.Baadaye akina Juliana shonza,Mtela Mwampamba na Habibu mchange kwa nyakati tofauti walikuja kutamka maneno yale yale aliyotamka Ndugu Zitto na hadi sasa wanayasema kwenye blogs na mitandao mbali mbali ya kijamii


‘
’Mwisho, nasikia sikia sana habari za kuchinjana. Kuuana nk. Nasikia habari hizi kwa watu wale wale wa kikundi kile kile. Moja, natoka Kigoma. Nimeaga kwetu.’’

Pia Post no:528 kuna kauli ya Zitto

‘Sijawahi kulalamika kutishiwa kuuwawahata siku moja, Sio hulka yangu hiyo. Nimekoswa na vifo vingi sana. Nimekunywa sumu nyingi sana. Nimekoswa ajali kadhaa. Lakini sio kawaida yangu kutafuta sympathy hata siku moja. You will never hear me doing that. Cowards do that.’

Rejea Kiunganishi hiki

----https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/370013-huyo-ndiye-ben-saanane-na-majibu-ya-zitto-27.html#post5251887

Kuna Makala ya kibanda hapa
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/373427-kibanda-naliona-anguko-la-zitto-kabwe.html


UFAFANUZi KWA UFUPI:
Masalia lililkua ni kundi la vijana walioenguliwa uchaguzi wa BAVICHA pamoja na baadhi ya wanasiasa waliokua wakilifadhili nje ya baraza la vijana.Baraza la vijana lilichukua hatua hatimae Makamu Mwenyekiti Juliana shonza akatimuliwa,Habibu Mchange na Mtela mwampamba wakafukuzwa kwa mujibu wa kanuni,itifaki na muongozo wa mabaraza wa CHADEMA kwa tuhuma za usaliti kwa chama.Walikua wakishirikiana na wanasiasa wenye nia ovu dhidi ya CHADEMA wa ndani na nje ya CHADEMA(Haya mengine sitayasema zaidi kwa kuzingatia katiba ya CHADEMA isipokua yale yanayohusu jinai tu).Turudi kwenye mada sasa:

TUNTEMEKE(ID iliyotumika na Mtela Mwampamba,Habibu Mchange na Festo Sanga)

Waliandika

Post No:9 ya tarehe 12 January 2013(siku 10 baada ya matamshi ya Mwigulu kuwa na video,siku Zaidi ya siku 24 baada ya kauli ya zitto na siku siku 22 baada ya kunituhumu kutaka kumuua zitto kwa sumu)

ID ya TUNTEMEKE iliyokua ikitumika na kundi la MASALIA walindika

‘’ kwa bomu linalokuja naona utakata tamaa kabisa,Kwa sbabu bomu hilo linaianika chadema na michezo yao yote michafu inayofanyika kwa usiri mkubwa na kuwaaminisha watanzania kwamba ni serikali kumbe ni wao.

Yaani,nakuombea uwe hai ushuhudie mwaka huu watu wanavyoumbuka.Asante mungu kwa kufanikisha hatua zote kilichobaki ni kuweka kwa tv muone ‘
'

Kwa hiyo hawa walijua kilichokua kinaendelea na mchezo huu ulipangwa mapema.
MTELA MWAMPAMBA

Leo ameendelea kuandika kwenye ukurasa wake wa facebook na Jukwa la TANURU LA FIKRA

JULIANA SHONZA

Aliandika:

‘’KUHUSU BEN SAANANE NA KUTUMIKA KUMUUA ZITTO KABWE

Wana jf,Nakili wazi hili swala lilitokea mnamo mwezi wa 5 mwaka 2012 tukiwa Lunch time hotel external kwenye mazungumzo ya kawaida(ambavyo ben saanane anaita ni vikao vya kuhujumu chama). Siku ya tukio tukiwa meza moja na Ben Saanane mkono wake wa kushoto alifunga bandeji akidai ameumia mkono(nakumbuka). Kwa babati mbaya sana katika maongezi yale Ben alilewa pombe (alikuwa anakunywa bia(kilimanjaro). Kulewa kwake pombe alijisahau na kutoa bahasha ya kaki yenye fedha, ndani ya bahasha ile wakati wa kutoa fedha alipe huduma ya chakula na vinywaji alidosha karatasi ya nailoni ndogo ikiwa na unga mwekundu ndani.

Tulimuuliza ni nini hicho akadai ni kuberi,na kuing'ang'ania tusifungue(aliyekiokota ni mwampamba).Lakini Mwampamba aligoma kumpa na kudai lazima ifunguliwe pale pale.

Ben saa nane akiwa katika hali yake ya kulewa alifura kwa hasira kutaka arudishiwe ilekaratasi,haliiliyopelekea uvunjifu wa amani pale lunch time hotel.Mwampamba aliondoka na mzigo ule kwa kukimbia nao, usiku ule Ben alitafutana na mwampamba hadi nyumbani kwake(temeke) akidai huo mzigo(ikumbukwe mwampamba na mm nimeishi kwake na nikaka yangu) . Lakini katika hali ya kusikitisha ben aliomba mzigo ule usiende mbali na kuahidi atasema kweli kile ni nini.

Ben saanane alikili wazi kwamba ile ni sumu lakini anapeleka nyumbani kwa ajili ya kuulia panya, Swala hili halikuishia usiku ule,ben hakufanikiwa kupata mzigo ule kesho yake asubuhi(jumapili) alikwenda kumsihi mwampamba ampatie mzigo.

Sharti lilikuwa aseme ni nini kwasababu huwezi kuwa na sumu eneo la starehe kama pale hotelini huku akisisitiza kuonana na zitto ambaye alisafiri usiku ule kwenda marekani bila kuonana na yeyote kati yetu?

Ndipo Ben saanane akakili ile ni sumu akilenga kumpatia zitto akiwa ametumwa na Dr.slaa.Tulihamaki kusikia kile kitu(hapa tulikua tabata reli stand tukisubiri usafi).Nilimuuliza uthubutu wake wa kufanya kitu kama hicho na kwanini afanye unyama huo,akadai ametumwa Kisa kikiwa ni zitto kumsakama dr.slaa ndani ya vikao vya chama.

Swala hili lilifika mbali kwa kuwekeana mipaka ya kula vyakula mahotelini na kutoshirikiana tena katika ushikaji wetu kama masalia.

Lakini urafiki wetu na ben uliendelea na tukayamaliza haya mambo kishikaji kawa wanasiasa vijana,Ben alifurahi sana ndipo akaja na wazo la PM7 kama movement ya kuendesha harakati huru ndani ya chadema zikilenga kukataa kutumika na viongozi wa chama kama ben alivyotumika kutaka kumuua zitto.

Hilo wazo la PM7 lilikaliwa mazungumzo mara nne lakini likaaishia hewani mara baada ya kuona halitakuwa na manufaa ndani ya chama na litaleta mtafaruku.

Tokea kupigwa kwa hoja hii ya ben saanane ya PM7,ndipo tulipo anza kutengenezeana uadui wa kisiasa hadi hii leo tumefikia hapa'' .

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...r-slaa-kwenye-siasa-za-juliana-shonza-39.html


awa niliowataja hapa juu ni wanasiasa (isipokua Festo Sanga).Hawa wanajua wanachofanya na hawawezi kusema hayo kama hawajui lolote.Matamshi yao yapo facebook na huku JF na kwenye blogs.

View attachment 87521View attachment 87522
hawa kunguru wote wanachowinda ni kuiharibia chadema tu na sasa mpango wa ujumla uliopo ni kwamba watu wanapandikizwa kwa nia ya kuiua chadema na wamo sana ndani ya chama na wengi wanatoka hata katika wilaya za asili za viongozi wenye lengo la kukilinda chama mf ndugu yetu lema ,wenje, john heche, wana shida sana maana ccm ina kila mbinu kuwaangamiza kisiasa na kuna makina yamewekwa pia rehani kuwa ikitokea mtu kapatwa na yaliyompata wao ndio wahusika haraka sana yaani wamewekwa kwa ubambikwaji kesi hawa ni pamoja na wewe ben sanane
 
Wewe adui wa CHADEMA si ndiyo ungefurahi zaidi?

Leta uthibitisho,nina haki ya kufahamina na mtu yeyote.Hakuna wa kunichagulia marafiki au maadui
Ben,
Sitaki wala haitatokea niamini kwamba unaihujumu CDM bila kufahamu. Najua unatekeleza mpango maalumu. Anyway, ama ufanikuwe au la, naamini historia unayoiandika sasa, tutapata nafasi ya kuisoma baadae...
 
Unaweza kuwahada Watanzania kwa muda mfupi,lakini kamwe uongo unaotengenezwa husahulika mapema kuliko unavyo fikiri.Nelson Madiba Mandela,aliitwa gaidi kwa kuwa tu alizitambua haki za watawaliwa na kuzipigania,lakini pamoja na ugaidi wake wa kubumba bado walimbembeleza wamuachie huru ili yeye na familia yake tu,lakini alikataa.Tunacho jaribu kukiona ni picha ambayo ilishachezwa na viongozi wengi madhalimu duniani lakini sasa ina kuja kwa style mpya ya TEHAMA.

Cha msingi wanyonge tusikubali kuona CDM inarudishwa nyuma,kwani kufikia hatua hii itahitaji miaka mingine zaidi ya 20 kuitengeneza na kufikia hatua hii.Yesu alikataliwa na Wafalme wakihofia dola zao kuanguka sembuse CDM,mtaitwa majina mengi sana na kwa kutumia uovu wao dhidi yenu hakika ipo siku ukweli utasimama.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom