Hali ya kiuchumi Arusha inazidi kushuka kila uchwao

Hali ya kiuchumi Arusha inazidi kushuka kila uchwao

Ni kweli mkuuArusha sio rahisi kupata msosi wa 1000 ni rahisi kuishi Dar kuliko Arusha. Arusha ni jiji la kitalii linapokea wageni wengi.
Nilisangaa et kwl msos wa kuku Arusha iwe buku kuku mbich wa broila n 7500 mpaka 8000 sasa mleta uz sjui anajua kuku au anazungumzia zle utumbo na miguu na kichwa ya kuku pala ngarenaro ndyo buku
 
Uhalisia wa mambo ndio ulivyo na ndio maana wengi wenu mmekimbilia dar. Ukikuta palangyo ana duka la spare basi tegemea kuwaona akina ayo, na ukikuta mushi asenga ana bar basi tegemea kuwaona akina laswai.
Jiji la arusha kwa uchafu linaongoza na ni kwa maeneo mengi hata uko njiro ambapo ndio ushuani walienda weka dampo huko. 🤦‍♂️
Inawezekana ulikuja Arusha ukitegemea kutoboa kibiashara kirahisi, biashara hauko hivyo, biashara zina changamoto popote uendapo, pambana mkuu acha kulalama mitandaoni
 
Jamaa yupo sahihi , Arusha kibiashara kutoboa ni kazi kwelikweli , Kheri ukafanye biashara Dodoma kuliko Arusha.

Mji una watu wachache eneo kubwa lakini uchafu kibao , Dar kuwa chafu ni kawaida kuyokana na wingi wa watu.
Unaishi Arusha? Ulishafanya biashara Arusha na Dodoma?
Ukitaka kufanya biashara Arusha lazima uwe creative na uwekeze vizuri
 
Mama kaiharibu nchi.uchumi wa Nchi uko mahututi.anachojua yeye ni kisafiri tu.hatukuzoea kuona Arusha kuwa na hali mbaya kiuchumi kiasi hiki.huyu bibi ni muuaji wa uchumi wetu hasitahili kuwepo kwenye hiyo nafasi.huyu alifaa awe muuimba taarabu.
 
Hivi Poker kumbe Arusha Kuna nyumba ya vyumba 3 unalipia Kodi ya 150k?
Ni rahisi kuliko Dodoma ama Dar es salaam

Wacha nitafute ya Chumba na sebule huenda itakuwa na Kodi ya 70k, ili nikiwa nakuja huko niwe nafikia badala ya kulala Lodge
 
Umeongea uongo mwingi sana, kwamba mji wenye wakazi zaidi ya Million 1.5 biashara ifanyike kwa kujuana tu, labda inategemea na biashara unayofanya mkuu, kuhusu uchafu, Kuna mji mchafu kama dar?
Hili la kujuana usilipinge ,kwanza ukiwa kule baada ya salaamu kinachofuata ni AISEE WEWE NI MTU WA WAPI?
Hakuna mchaga anayenunua duka la chasaka ama asiye mchaga wewe usitake kudanganya watu.
Wale wa mama wa soko kuu mfano wa Kanda ya ziwa wanachangiwa na wateja wa Kanda ya ziwa , wa huko wananunua kwa wauzaji wa huko huko.
Arusha naipenda weather Ila sio mji kirafiki una ukabila Kama miji ya Kenya.
Mana Arusha wachaga ni wengi ndio wameshikilia nguvu kuu za kiuchumi.

Binafsi nilitaka kuweka empire huko nikawaza mji wangu wa Mwanza na wasukuma walivyo wakarimu hawabagui jamani nikaona Bora niishi Mwanza.

Hili la ubaguzi naweza nikatoa hela tukafanya research kwa wafanya biashara wa Kanda zingine walioko huko.

Kuna mmama mmoja mhaya nilimuuliza kitu ichi akaniambia nikinunua dukani.kwake deto.

Arusha ni wanajifanya wajuaji Kama wameru na waarusha.yaani Yale meno ya kashata za karanga wao wanaona Kama ni gold wamebeba mdomoni.

Ubaguzi upo hapa nitakupinga Kama vipi tutaingia field tufanye sample hata maduka mia moja tulete mean ,range, standard deviation, variance Mana number don't lie
 
Hili jiji la arusha ambalo linasifika kwa utalii na ambalo lina historia nzuri ya kutoa wasanii, waigizaji na watangazaji maarufu, sifa zake kwa nje ni nyingi na nzuri sana. Ila kwa uhalisia ukifika ndani ya jiji hilo ni shida tupu.

Biashara ndani ya jiji hilo ni ngumu sana, watu wanafanya biashara kwa kujuana sana. Kiufupi mzunguko ni mdogo sana si soko la kilombero wala soko kuu.
Ukipita mitaa ya makao mapya utakuta nyumba self contained ya vyumba 3 shs 150,000/= na wanataka kodi ya hata mwezi. Ukienda huko ngarenaro mitaa ya shauri moyo unakuta wali wa kuku 1000.
Mbaya zaidi hili jiji mitaa mingi ni michafu sana kama sekei, sombetini, mbauda na huko mianzini. Biashara kubwa katika hili jiji ni biashara ya shule, biashara ya nyama aina zote na biashara ya bia.
Japo wanachuga hupenda kulitetea hili jiji, ila kiuhalia arusha ilipaswa kuwa mji kama miji mingine. Yaani saivi hata kahama kuna mzunguko wa hela kuliko arusha.
Hili ndio jiji ambalo matajiri wake wote hawapo top 100 ya matajiri Tanzania.
Hili pia ndio jiji linaloongoza kwa kuvaa mitumba wazee wa krokon na memorio.
Hili ndio jiji ambalo wakazi wake wengi ni lialia wakija kwenye biashara yako watataka uwapunguzie hata kitu cha mia.
Hili ndilo jiji ambalo ukikaa mwaka mmoja unaweza wafahamu wakazi wote wa hapo. Hapo utapata picha udogo wa jiji.
Imagine jiji uwanja wa ndege hauna taa za kuongozea ndege usiku. View attachment 3004742
Nilifika Arusha siku za karibuni nilitembea toka Stand ya bus hadi Kijenge sikuona furushi la taka njiani Wala mifuko ya plastic na sabuni wala chupa za Mo na Azam energy suala la uchafu ni uongo mtupu.
Kiwanja Cha ndege Arusha kina miruko mingi ya ndege ikizidiwa na JNIA, KIA na Dodoma tuu hivyo hapo ni uongo wako tuu na kuweka taa Magu alichukua zilizotakiwa Arusha na kumpeleka Chatto.
Kahama Kuna dhahabu na mzunguko wa fedha zaidi ya Arusha ila quality of life and sophistication na elimu ni mbigu na ardhi.
 
wabaguzi hao wakina Zanzibar-ASP mpaka wamekimbia , mji wa kishamba wanaangalia meno kama una meno meupe hupat wateja.
Huku zenji huwa tunaangalia kama una sigida usoni, umevaa barakashea kichwani, kanzu, msuli au kobazi ili tukuuzie kitu au tununue kitu.
Kama unataka kujua au kujifunza ubaguzi hapa Tanzania basi njoo Zenji.
 
Hili la kujuana usilipinge ,kwanza ukiwa kule baada ya salaamu kinachofuata ni AISEE WEWE NI MTU WA WAPI?
Hakuna mchaga anayenunua duka la chasaka ama asiye mchaga wewe usitake kudanganya watu.
Wale wa mama wa soko kuu mfano wa Kanda ya ziwa wanachangiwa na wateja wa Kanda ya ziwa , wa huko wananunua kwa wauzaji wa huko huko.
Arusha naipenda weather Ila sio mji kirafiki una ukabila Kama miji ya Kenya.
Mana Arusha wachaga ni wengi ndio wameshikilia nguvu kuu za kiuchumi.

Binafsi nilitaka kuweka empire huko nikawaza mji wangu wa Mwanza na wasukuma walivyo wakarimu hawabagui jamani nikaona Bora niishi Mwanza.

Hili la ubaguzi naweza nikatoa hela tukafanya research kwa wafanya biashara wa Kanda zingine walioko huko.

Kuna mmama mmoja mhaya nilimuuliza kitu ichi akaniambia nikinunua dukani.kwake deto.

Arusha ni wanajifanya wajuaji Kama wameru na waarusha.yaani Yale meno ya kashata za karanga wao wanaona Kama ni gold wamebeba mdomoni.

Ubaguzi upo hapa nitakupinga Kama vipi tutaingia field tufanye sample hata maduka mia moja tulete mean ,range, standard deviation, variance Mana number don't lie
Mji ambao anaweza akauziwa kitu mchina, mzungu, mhindi, mjapani, mkenya, mnyarwanda, msomali au mjamaika bila shida yoyote, sasa wewe mndengereko kwanini usiuziwe kama una pesa?

Arusha ni mji wa pesa, ukiwa na pesa utauziwa au kununua chochote, ukiwa huna hela utakuwa na maneno mengi tu ukitaka upunguziwe na uonewe huruma, na hapo ndipo unatafuta kutaka kujuana, mwisho utaishia kulalamika kuwa umebaguliwa.
Tafuta hela ili asilalamike.
 
Hili jiji la arusha ambalo linasifika kwa utalii na ambalo lina historia nzuri ya kutoa wasanii, waigizaji na watangazaji maarufu, sifa zake kwa nje ni nyingi na nzuri sana. Ila kwa uhalisia ukifika ndani ya jiji hilo ni shida tupu.

Biashara ndani ya jiji hilo ni ngumu sana, watu wanafanya biashara kwa kujuana sana. Kiufupi mzunguko ni mdogo sana si soko la kilombero wala soko kuu.
Ukipita mitaa ya makao mapya utakuta nyumba self contained ya vyumba 3 shs 150,000/= na wanataka kodi ya hata mwezi. Ukienda huko ngarenaro mitaa ya shauri moyo unakuta wali wa kuku 1000.
Mbaya zaidi hili jiji mitaa mingi ni michafu sana kama sekei, sombetini, mbauda na huko mianzini. Biashara kubwa katika hili jiji ni biashara ya shule, biashara ya nyama aina zote na biashara ya bia.
Japo wanachuga hupenda kulitetea hili jiji, ila kiuhalia arusha ilipaswa kuwa mji kama miji mingine. Yaani saivi hata kahama kuna mzunguko wa hela kuliko arusha.
Hili ndio jiji ambalo matajiri wake wote hawapo top 100 ya matajiri Tanzania.
Hili pia ndio jiji linaloongoza kwa kuvaa mitumba wazee wa krokon na memorio.
Hili ndio jiji ambalo wakazi wake wengi ni lialia wakija kwenye biashara yako watataka uwapunguzie hata kitu cha mia.
Hili ndilo jiji ambalo ukikaa mwaka mmoja unaweza wafahamu wakazi wote wa hapo. Hapo utapata picha udogo wa jiji.
Imagine jiji uwanja wa ndege hauna taa za kuongozea ndege usiku. View attachment 3004742

Hili ni tatizo lako binasfi, haliusiani na Mkoa wa Arusha
 
Ukiwaambia ukweli wanasema tuna chuki ilihali hali ya wafanyabiashara kwa mkoa wa arusha ni ngumu sana. Asilimia kubwa ya mapato ya arusha yanategemea utalii. Hiyo pesa ya utalii wala haiingii kwenye mzunguko wa huko town wa kila siku. Unaeza fanya biashara arusha miaka 2 na mtaji wa 100ml na usitoboe ila kwa huo mtaji nenda mbeya, kahama au dar au mbeya na hata morogoro uone utakavyotoboa.
Mimi ni mdau wa Utalii, Arusha naijua lakini hicho unachokisema kuhusu Utalii ni uongo mkubwa. Mnyororo wa Utalii ni mrefu na mpana mnoo kwa jiji la Arusha, sidhani kama kuna mji hapa Tanzania wenye mnyororo unaokaribiana na huo. Kwa kifupi sana ukiondoa kodi za serikali (ambazo hazizidi 1/3 ya matumizi ya pesa za mtalii) kiasi kingine chote kinakwenda kwa makampuni ya watalii, mahoteli, migahawa, madereva, mama lishe, masoko, boda boda, makanisani, mpaka malaya wa Shiva, Mrina nk
 
Jamaa yupo sahihi , Arusha kibiashara kutoboa ni kazi kwelikweli , Kheri ukafanye biashara Dodoma kuliko Arusha.

Mji una watu wachache eneo kubwa lakini uchafu kibao , Dar kuwa chafu ni kawaida kuyokana na wingi wa watu.
Swala la msingi ni kwamba competition ya Arusha ni kubwa ,huko kwingine unakosema ni kwamba Bado watu ni mbumbumbu.

Moja ya Mji watu wanajua biashara na customer care ni Arusha
 
Mbona watu wa kanda ya ziwa huwa mnachuki sana na kaskazini 😀
Alafu wachangiaji wote ni wasukuma watu wa chuga wametuliaga tu
Leo umeangukiwa na kitu kizito kichwani.

Eti mnaitwa Jiji la Wadudu 😁😁😁😁

Ukweli ni kwamba competition ya Arusha ni kubwa ndicho kimemshinda mtoa mada.

Anatakiwa kwenda Kwa washamba huko Mikoani
 
Ni kweli usemayo. Ujio wa kundi la wadudu Arusha ni uthibitisho tosha kwamba Arusha inaelekea kuwa kijiji kikubwa kama ilivyo miji yetu ya kitanzania. Inashangaza sana ni vigezo vipi vinaifanya Arusha kuwa makao makuu ya EAC.

Wiki mbili zilizopita nilitembelea tena Arusha baada ya miaka mitano kupita bila kukanyaga mji ule. Arusha badala ya kung'ara, inafifia. Arusha inarudi nyuma na wenyeji wanakiri kuwa kuna upigaji wa kufa mtu. Majengo ni yale yale chakavu, barabara nyingi zimejengwa chini ya kiwango. Arusha inasikitisha.😢
Wadudu wamepata Kiongozi wao saizi
 
Mama kaiharibu nchi.uchumi wa Nchi uko mahututi.anachojua yeye ni kisafiri tu.hatukuzoea kuona Arusha kuwa na hali mbaya kiuchumi kiasi hiki.huyu bibi ni muuaji wa uchumi wetu hasitahili kuwepo kwenye hiyo nafasi.huyu alifaa awe muuimba taarabu.
Toa upumbavu wewe,bila kurejesha Utalii mungeendelea kupauka na umaskini Hadi mkome
 
Back
Top Bottom