Hali ya kiuchumi Arusha inazidi kushuka kila uchwao

Hali ya kiuchumi Arusha inazidi kushuka kila uchwao

Haihitaji kufanya biashara Bali inahitaji kutembea na ku shop Mikoa tofauti
Nmeenda dodoma na mwanza customer care very poor hata hotel nyingi za hiyo mikoa inabidi waajiri watu wa arusha mosh ili atleast wasaidie hali
Hata kama umeshasafiri nje utakubali Tanzania customer care iko very poor
Arusha wanajua biashara chief 🔥
 
Nilifika Arusha siku za karibuni nilitembea toka Stand ya bus hadi Kijenge sikuona furushi la taka njiani Wala mifuko ya plastic na sabuni wala chupa za Mo na Azam energy suala la uchafu ni uongo mtupu.
Kiwanja Cha ndege Arusha kina miruko mingi ya ndege ikizidiwa na JNIA, KIA na Dodoma tuu hivyo hapo ni uongo wako tuu na kuweka taa Magu alichukua zilizotakiwa Arusha na kumpeleka Chatto.
Kahama Kuna dhahabu na mzunguko wa fedha zaidi ya Arusha ila quality of life and sophistication na elimu ni mbigu na ardhi.
Hivi mkuu uko serious ?
Yaani kiwanja cha ndege Arusha kizidiwe miruko na Dodoma ?
Embu google uangalie vizuri
 
Tatizo la Arusha na Miji mingine inayotegemea sekta za Utalii na Madini ni kwamba pesa hizo huenda Kwa watu wachache , makampuni na Serikali ila mtu wa chini hazimfikii sana.

Ikiingia hapo Mjini unaona magorofa yanapanda sana Kwa Ajili ya Mahoteli ila Sasa huku kwenye grassroots ndio Changamoto.

Ni tofauti sana na Dar ,Mwanza au Mbeya ambako Kuna shughuli za aina nyingi hasa zile za watu wa chini wanapata uhakika wa hela.
Ndugu yangu Dar inabebwa na vitu viwili tu.
1. Bandari
2. Wingi wa watu.

Kumbuka tu, 35% ya pato la taifa linatokana na Bandari, na 10% ya watanzania wako Dar na kati yao 90% wanaishi mjini. Penye watu, penye mji, pana shughuli na pana pesa. Huwezi kulazimisha Arusha iwe na shughuli nyingi wakati watu ni wachache, tena wengi hawaishi mjini, wamesambaa mkoa mzima. Shughuli nyingine zozote ndogo ndogo ni matokeo ya shughuli moja kubwa yenye kumwaga pesa nyingi kwa mara moja.

Utalii wa Arusha una mnyororo mrefu sana. Huwezi kugundua hilo vizuri unless uje ufanye kazi za kitalii ndio utaelewa. Na kumbuka, takwimu za muda mrefu zinaonyesha utalii unachangia chini ya 18% ya pato la taifa na katika hilo Arusha inachangia chini ya nusu.
 
Mji ambao anaweza akauziwa kitu mchina, mzungu, mhindi, mjapani, mkenya, mnyarwanda, msomali au mjamaika bila shida yoyote, sasa wewe mndengereko kwanini usiuziwe kama una pesa?

Arusha ni mji wa pesa, ukiwa na pesa utauziwa au kununua chochote, ukiwa huna hela utakuwa na maneno mengi tu ukitaka upunguziwe na uonewe huruma, na hapo ndipo unatafuta kutaka kujuana, mwisho utaishia kulalamika kuwa umebaguliwa.
Tafuta hela ili asilalamike.
Ngozi nyeusi ni ni mikosi, kule Zanzibar Mtanganyika ana baguliwa kwa kuitwa kafiri na Ukiwa mkristo wanakuchukia, lakini wazungu wanapendwa na wana hudumiwa kwa kunyenyekewa na Wazungu ni Wakristo kama ilivyo wa Tanganyika.
 
Hili jiji la arusha ambalo linasifika kwa utalii na ambalo lina historia nzuri ya kutoa wasanii, waigizaji na watangazaji maarufu, sifa zake kwa nje ni nyingi na nzuri sana. Ila kwa uhalisia ukifika ndani ya jiji hilo ni shida tupu.

Biashara ndani ya jiji hilo ni ngumu sana, watu wanafanya biashara kwa kujuana sana. Kiufupi mzunguko ni mdogo sana si soko la kilombero wala soko kuu.
Ukipita mitaa ya makao mapya utakuta nyumba self contained ya vyumba 3 shs 150,000/= na wanataka kodi ya hata mwezi. Ukienda huko ngarenaro mitaa ya shauri moyo unakuta wali wa kuku 1000.
Mbaya zaidi hili jiji mitaa mingi ni michafu sana kama sekei, sombetini, mbauda na huko mianzini. Biashara kubwa katika hili jiji ni biashara ya shule, biashara ya nyama aina zote na biashara ya bia.
Japo wanachuga hupenda kulitetea hili jiji, ila kiuhalia arusha ilipaswa kuwa mji kama miji mingine. Yaani saivi hata kahama kuna mzunguko wa hela kuliko arusha.
Hili ndio jiji ambalo matajiri wake wote hawapo top 100 ya matajiri Tanzania.
Hili pia ndio jiji linaloongoza kwa kuvaa mitumba wazee wa krokon na memorio.
Hili ndio jiji ambalo wakazi wake wengi ni lialia wakija kwenye biashara yako watataka uwapunguzie hata kitu cha mia.
Hili ndilo jiji ambalo ukikaa mwaka mmoja unaweza wafahamu wakazi wote wa hapo. Hapo utapata picha udogo wa jiji.
Imagine jiji uwanja wa ndege hauna taa za kuongozea ndege usiku. View attachment 3004742
Mitaa unayoitaja yote ni mikongwe... Nyie ndio mnasemaga Arusha ndogo (yani Arusha kati, levolosi, kaloleni na sekei)..Nimetoka chuga juzi kati, aisee kumbe siku hizi ni kubwa.. inafaa kuwa na manispaa mbili basi tu meru wamegoma kuungwa na jiji
 
Back
Top Bottom