Hali ya maisha ya Mtanzania ni ngumu sana. Rais asipochukua hatua sasa hali itaendelea kuwa mbaya zaidi

Pamoja na kipato kuwa kidogo,

Bungeni wabunge wanaoshauri Serikali kuongeza wigo wa kukusanya mapato Kwa hao hao wanapata 10,000 Kwa siku.

Tunapopaza sauti kudai mabadiliko kama Nchi na Katiba mpya na usishiriki ukidhani kufanya hivyo ni Siasa,

Hakipo kitachobadilika.

Amen
 
Haya uliyoandika hapa yangekuwa yamekamilika kama ungeonesha role ya serikali, na vipi serikali imetimiza wajibu wake kufanikisha hilo. Nakuona unaendelea kuficha madhaifu ya serikali kwenye hili suala, naamini sababu inayokufanya uwe hivyo ni ile ile asali.

Kuwaambia watu waache kukimbilia kazi nyepesi za kubangaiza, wakati ndizo zilizopo, kwasababu serikali imeshindwa kuwapa wahitimu wa vyuo kazi nzito unazotaka wafanye, ni kuwaonea wapambanaji, show some respect!.

Serikali inayojielewa, ikishatambua changamoto wanazopitia raia wake, lazima itafute namna ya kuwapunguzia maumivu, mfano, serikali ikishajua raia wake wengi wanafanya kazi nyepesi, zinazowapa kipato kidogo, ni lazima ifanye iwezalo kupunguza mfumuko wa bei, hawa wapambanaji hawawezi control hilo.

Zaidi, unaposema watu watazame family planning, hapa napo unatengeneza tatizo jingine mbele ya safari, tunaona kwenye baadhi ya nchi zilizoendelea, hata kama teknolojia inayowarahisishia kufanya kazi zao, usiyatazame haya mambo kwa jicho la upande mmoja.
 
[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Msemo mzuri
 
Hazina ukweli wowote, maisha ni yaleyale tu na kila uchwao yanazidi kubadilika kua mazuri sema na sisi wananchi tunazaliana hovyo kiasi kwamba serikali inazidiwa kutuhudumia.
[emoji1320]
 
Gharama za maisha zimepanda ni matarajio yangu serikali ingekua imeshapeleka muswada wa kuongeza mishahara ya wafanyakazi. Na ni mategemeo yangu bajeti mpya itakwenda kuongeza mishahara na kima cha chini
[emoji1320]
 
Bams, mapendekezo yako hayawezi kuondoa "njaa" waliyonayo Watanzania. Njaa tunayopata leo inatokana kwa namna moja au nyingine kwa mikakati mibovu. Serikali nyingi za Afrika zimekuwa zinajali uwepo wa Serikali na Nchi. Sovereign State. Wanajali kukusanya mapato ili Serikali iweze kujiendesha, kiuhalisia wanakuwa wanafanya trial and err. Kuna Wachumi kama Ludwig Erhard, katika umahiri wake aliandika kwenye kitabu cha Mafanikio ya Uchumi "Economics of Success" alizungumzia hatma ya Urusi, alizungumzia mienendo pamoja na matatizo matatizo tunayoyapata leo Tanzania....kama livyokuwa urusi.... ....itakayowakabili....aliandika....

"Masharti ya matumizi mazuri ya kanuni ya upangaji tu hayapo duniani."

Naona mantiki unayotumia ni kuwa tunajiendea tu bila mpangilio. Ukumbuke tupo kwenye mpito kichumi..... Bwana Ludwig aliongeza....


"...Katika nyakati za kisasa zilizopangwa kuingilia kati(yaani copy and paste) kumevuruga uchumi. Wapangaji wako katika nafasi dhaifu kimantiki lakini zenye nguvu kimbinu." nafikiri bado tunahitaji muda....rome was not built overnight!



"Isipokuwa ukweli kwamba mfumo wa fedha uliokatishwa tamaa hufanya uchumi wa soko huria usifanye kazi bila mfumuko wa bei"

Tuna mfumuko wa bei na Ndio inayofanya Njaa iongezeke....yaani mateso yanayotokana na kuingia uchumi wa kati na wakibepari bila au kabla hatujawaandaa Wananchi.


Unaweza pitia huyu Raisi wa Senegal LS. Senghor akizungumzia haya.

Tuna kazi ndio, but its not as if one size fits all
 
Viongozi wa juu Serikalini wananufaika na Ugumu wa maisha wa Raia.

1. Unapolipa vat kwenye bidhaa madukani, Serikali inapata pesa za kununua mafuta kwenye V8 za viongozi.

2. Unaponunua Mchele 3,500 Kwa kilo, jua Basha anatunisha mfuko kwenye Kampuni zake za kuuza nafaka Kenya na somalia.

3. Unapolipa 55,000 nauli ya Dar Mwanza, Kuna kampuni ya mwigu na wenzie kupitia Mama Esther wanatajirika kupindukia.

4. Unaponunua maji 500 Kwa ndoo moja, uwe na HAKIKA Wizara ya maji wanatumia mwanya huo kuomba pesa hazina kutatua changamoto hiyo, na pesa zikitoka ZINAPIGWA.

5. Unaponunua bundle la internate Bei juu, Pena anapata posho Kutoka makampuni hayo, ananufaika na Bei ya vifurushi kuwa juu.

6. Unaponunua mafuta ya kupikia Lita Tano Kwa 30,000 uwe na HAKIKA Kuna TOZO na Kodi zaidi ya 5000 Kwa Kila dumu imeingia Serikalini na inatoka Kwa matumizi ya kawaida ya viongozi.

Serikali haiwezi kupunguza mzigo wanaoubeba raia, sababu kwao sisi ni chanzo Cha mapato Yao.

Tuungane kudai KATIBA mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA Ili kuondoa mifumo kandamizi inayoumiza wengi kuhudumia Wachache.

Amen
 
Kama unapokea 400,000 na matumizi ni 870,000 Kwa mwezi, na huachi KAZI na unaishi, ni dhahiri unaiibia Serikali, au mwajiri ukipata mwanya lazima unapiga.

Serikali inawafundisha watu WIZI wa bila kukusudia.
 
Huo mfano wako sio maisha ya Watzn wengi,so chapa kazi acha ulalamishi usio na msingi au wewe hujamsikia Ndugai?

Mwisho unataka Rais achukue hatua zipi labda?
 
Ukisema hawajali basi una matatizo makubwa haifai hata kukuelezea zaidi
 
Zinaukweli au hazina??
Maisha ni individuals cases na ndio maana huwezi Kuta maeneo ya starehe hakuna watu,sadaka kupungua,fundi cherehani kuacha kushona nguo,magari yakipungua barabarani Wala sherehe so usilete neno Jumuishi ndio maana Huwa zinkawa kelele no one cares Kwa sababu hazina ukweli
 
Ndugu yangu panda mazao mvua ziko Katikati ya msimu Sasa,sijui wewe unazungumzia mvua zipi
 
Gharama za maisha zimepanda ni matarajio yangu serikali ingekua imeshapeleka muswada wa kuongeza mishahara ya wafanyakazi. Na ni mategemeo yangu bajeti mpya itakwenda kuongeza mishahara na kima cha chini
Wasio wafanyakazi na ambao Wana toil zaidi inakuaje?
 
Bro unapigia mbuzi gitaa una hoja nzuri sana.

Hapa tegemea kejeli na shombo za kuambiwa mfumuko wa bei ulaya ni mkubwa kuliko TZ..

Kiufupi Samia alifail from day one japo kuna watu hawataki kuamini ni Raisi asiyekuwa na msimamo wala Dira.
Tusichoshane hamia ambako maisha ni nafuu,ulaya ni mbali hapa hapa Afrika
 
Sasa yule mama Samia kweli unadhani hata anaelewa mfumuko wa bei ni nini? Yani kiongozi mkubwa wa nchi watu wamemuokota okota tu huko majalalani ndio autoe umma wa watanzania kwenye umasikini? Mipango endelevu ya taifa husukwa na watu smart sio hawa wakina babu tale, msukuma, shangazi, na wakina Amos Makala
 
Hakuna mtawala wa kiafrica anaeweza mletea maendeleo mwafrika, ongezeni tu ubunifu wa kupambana
Hata Kwa wazungu hakuna mtawala anayekuletea wewe maisha.

Mumeambiwa ombeni fursa za Kilimo tena Kwa kubebwa na Serikali hamtaki,Sasa mnataka muwe Mawaziri au? Mnaambiwa nendeni Halmashauri mpewe mikopo isiyo na riba hamtaki, sehemu zingine wananunuliwa Vitendea kazi kama magari,bajaji,mashine za matofali ila hamtaki Sasa msaidiwaje?

Chadema watawasaidia?
 
Lakini kwenye mfumo wa kibepari hakuna anaelala njaa.
Ulaya kula sio ishu.
Ni uhakika sababu kwenye ubepari ajira tele
Hizo Ajira tele ziko wapi? Husikii wakilalama maisha magumu Hadi Wanaandamana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…