kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Watumishi wenye ajira na ujira ni miongoni vya vyanzo vikuu vya kusambaza fedha kwenye jamii wakati wanapofanya matumizi na manunuzi yao kwa kutumia mishahara yao wanayopata kila mwezi.. Kundi hili linalipwa mishahara isiyolingana na uhalisia wa upandaji wa Bei, hivyo kufanya ununuzi mdogo sana wa huduma na bidhaa, hali inayosababisha mzunguuko mdogo wa fedha ndani ya jamii na kusababisha Hali mbaya sana ndani ya familia na mtu mmojammoja kwenye taifa.
Kandarasi kubwa sekta ya ujenzi kupewa wageni. Eneo hili pia linasababisha mzunguuko wa fedha ndani ya nchi kuwa mdogo kwakuwa fedha nyingi zinavuka mipaka na vibarua wazawa kupewa ujira mdogo sana kwenye kandarasi hizi za wageni. Wageni wanaangalia serikali inawalipaje watu wake.
Kandarasi za wazawa kukopwa au kucheleweshewa malipo hii ndio mbaya kabisaaaaaa, maana wazawa wanashindwa kukuza mitaji na kusababisha kuwalipa fedha kidoogo sana vibarua wao.
Ukosefu wa masoko ya uhakika ya mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na uchimbaji. Idadi kubwa sana ya wakulima, wafugaji hawana uhakika wa masoko na Bei ya mazao yao. Serikali utaisikia inahangaika na ukanda fulani TU na mazao fulani TU kwenye Kanda fulani TU na kusahau kwamba nchi nzima watu wake wanategemea kilimo na ufugaji na uvuvi. Hii nayo inasababisha hali ngumu sana katikati Kila kaya na kila mtu, wakulima na wafugaji wanauza kwa hasara. Serikali inafurahia Hali hii kisiasa eti inapunguza mfumuko wa Bei kwakutumia jasho la wakulima na wafugaji maskini kabisa.
Matokeo ya haya yote ni kuwa na jamii inayohangaika na kutapatapa isijue nini cha kufanya. Jamii ambayo kama akitokea mtu wa kuwasemea haya mateso yao kwa uwazi mbele ya camera ataitwa mchochezi, anatumiwa na pengine kunyamazishwa kwa njia mbalimbali kuanzia kununuliwa hadi kuumizwa ili Hali iendelee hivihivi milele.
Hali imesababisha kuwa na jamii ambayo:
1. Ina wezi wengi wa muda na mali za mwajili na jirani. Kila mtu ni mwizi kwa kiwango chake.
2. Ina wategemezi wengi. 90% ya wanajamii wote ni tegemezi.
3. In waongo wengi, wasomi wanaongoza kwa woga.
4. Ina migogoro mingi sana ndani familia, jamii na makazini
5. Ina watu wajanjajanja wasiokuwa na morali ya kazi
Uchaguzi ujao tunataka kuchagua watu wanaokerwa na Hali hii katika ngazi zote za uongozi na uchaguzi bila kujali chama, jinsia, kabila Wala dini ya mtu. Wananchi wanahitaji mitaji, maji ya kumwagilia, pembejeo, maghala, masoko na Bei nzuri ya mazao yao. Wafanyakazi wanahitaji ujira utakaotosha kuwahudumia wenzao vizuri na bashasha. Mwajili afahamu mtumishi wake analala wapi, anasafirije kwenda na kurudi kazini, atakula nini akiwa kazini na atafanyaje kazi zake.