FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Sasa wewe mwenyewe una uhakika hujajaa adui ujinga?Yaani ujinga huu umeenda hadi kwa viongozi, mfano hii SGR badala ya kuanza kutumika kwa abiria ingeanzia kutumika kwa mizigo , tungekua tumetengeneza bandari kavu kubwa sana pale morogoro na tabora na chalinze ili mizigo yote ya bamdarini ipokelewe huko, ili kupunguza msongamano bandarini na jijini. SGR ingerudisha pesa zetu haraka kuliko kubeba watu wenye shangazikaja wanaowahi kwenda kufanya uziznzi morogoro na Dodoma. Wafanyakazi waliokuwa wameajiliwa kwenye makapuni ya Shabiby, Abood, BM , Elsaid nk wataenda wapi?
Kwa kukujuza tu, lengo kuu la hii reli ni mizigo. Kuna hesabu zake na "operation" ya mizigo ni ngumu zaidi ya abiria, abiria hachungwi, mizigo ni lazima ihakikishe wapakiaji, upakuwaji, usalama wake kabla ya kuhufashiwa, usalama utapo hifadhiwa. Kwa ufupi kama ulivyonavyo unapoipakilia uwe navyo unapoipakulia.
Kwa Tanzania inabidi uanze "from scratch", bandarini kwenyewe inapotakiwa mizigo itoke na kuingia ndiyo kwanza DP World na Aidan wanapaweka sawa.
Tutafika tu huko, bandari kavu ya Kwala mbpona umeisahau, ipo pale lakini haina chombo hata kimoja cha kuteremshia mizigo.
Mlolongo wa "logistics" za mizigo ni mrefu sana kijana, unawezq ukaharibu kabisa badala ya kutengeneza, twende nao kwa wakati wake. Nadhani haupo mbali kuanza.