Uchaguzi 2020 Halima Mdee, fedha za mfuko wa jimbo umepeleka wapi?

Uchaguzi 2020 Halima Mdee, fedha za mfuko wa jimbo umepeleka wapi?

Ndungu zangu wana jamvi habari za muda huu.

Leo nimepata wasaha wa kupitia Kitabu cha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya jimbo la kawe (2015-2020)
kilichoandikwa na aliyekuwa mbunge wetu Halima James Mdee.

Nimeshtushwa sana na nilichokiona kwenye kitabu hiki, naomba kuwashirikisha kitu ambacho kimepelekea nishtuke mimi kama mkazi wa jimbo la Kawe na mnufaika wa fedha za mfuko wa jimbo.

Kwenye kipengele kinachosomeka Taarifa ya Miradi ya Maendeleo ya Fedha za mfuko wa Jimbo.

Jina la Mradi: Kujenga Kivuko cha waenda kwa miguu Soko la Samaki Ununio

Mwaka 2017/18- (Uk.25 )

Tsh. Mil 5,000,000/= zilitengwa kwa ajili ya mradi huo wa kivuko cha waenda kwa miguu kilichopo karibu na soko la samaki la ununio.

Mwaka 2018//19- (Uk.27)

Mradi huo huo unaonekana katika ukurasa namba 27 huku ukitengewa Kiasi cha Tsh Mil 13,500,000/= lakini utekelezaji wake kama ilivyoandikwa kwenye kitabu hiki bado ulikuwa katika hatua za awali za manunuzi.

Mwaka 2019/20 - (Uk.31)

Mradi huo huo tena unaonekana kutengewa kiasi cha Tshs Mil 20,000,000/= kwenye page no 31. Huku mbunge wetu akijinadi kwenye kitabu hiki kuwa mradi huo umekamilika.

Lakini kiuhalisia kabisa ni kwamba mradi huo hadi ninavyoandika thread hii , haujakamilika na hautumiki hata na mkazi mmoja wa ununio na kata nzima ya kunduchi kwa ujumla.

Kwa hiyo mradi mmoja wa kivuko cha waenda kwa miguu soko la samaki ununio umegharimu Jumla ya kiasi cha Tshs Mil 38,500,000/= ndani ya kipindi cha miaka 2 (2018-2020) , ambazo ni fedha zinazosimamiwa na kutolewa na Ofisi ya Mbunge ambaye ni Mh.Halima Mdee.

Kwa tafsiri nyepesi kabisa inaonyesha hakukua na usimamizi mzuri wa fedha za jimbo la Kawe chini ya dada yetu Halima.

Ndugu zangu wana Jamvi nimeattach hapa picha za mradi uliotajwa kwenye taarifa kama ulivyo kwa sasa.

Ally Ramadhan Salehe

Ununio Mwisho-Kunduchi
Kicheko kimerudi tena kwa wajasiriamali kawe
IMG-20200928-WA0075.jpg
IMG-20200928-WA0067.jpg
 
Mdee alikuwepo toka bunge la 9 akiwa viti maalum so hta akianguka atarudi bungeni tu by default sasa send off hiyo inatoka wapi?
Sasa Gwajima akianguka unadhani atateuliwa viti 10? Au ndio anaishi kwa aibu ya kuangushwa na binti mdogo.
Kwendraa kama kura ivi we mabinti wadogo unawajua kwel unaniletea pigo za kuwaita ajuza mabinti unafeli sana kwanza usibishane na mimi jifunze kwanza kutofautisha umri then urudi
Gwajima kaajiri wachumia tumbo kibao, kuna id kibao za kumpigia debe Gwajima, ila wote wanaimba single moja. Nawashauri pigeni hela za huyo boya maana hiki ni kipi cha kula hela za Mabwege, lakini mtashangaa matokeo. Mbinu pekee ya ccm kushinda hilo jimbo ni kutoka na mabox ya kura kwa uratibu wa jeshi la polisi, na tume ya uchaguzi.
Mbona kama Gwajima anawatetemesha sana kubalini tu kawe halima hatumtaki tena
 
Kwa kweli fedha za mfuko wa Jimbo hakuna mbunge anaeweza kutolea maelezo ya kueleweka..Bora hata wa Upinzani Kuna kiasi kinaenda kwa wananchi Ila jwa wabunge wa CCM wananchi hawaoni hata mia.

Wakijitahidi Sana wanachangia mifuko hamsini ya simenti biashara imeisha .

Hongera Halima Mdee kwa kujaribu kuonyesha kuwa fedha huwa zinawafikia wananchi wako.
 
MKANGANYIKO WA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA FEDHA YA MFUKO WA JIMBO LA KAWE ZAIDI YA SHS 126 MILLION ZIMEFUJWA….

Nimeipitia taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya fedha ya mfuko wa jimbo la Kawe iliyoandikwa na Halima Mdee (mbunge aliyemaliza muda wake) na kukugundua kuwa taarifa hiyo ni wizi mtupu. Taarifa hii inaonyesha ubadhirifu wa fedha za jimbo na inamwondolea sifa Halima Mdee kupewa hata dakika 1 ya ziada kuendelea kuwa mbunge wa Kawe. Taarifa hii ina uongo mwingi na inaonyesha kuwa kiasi cha zaidi ya Shs 126 milion zimefujwa na mpaka leo hazijatekeleza miradi iliyokusudiwa.

Taarifa hiyo ya mfuko wa jimbo inaonyesha kuwa jumla ya shs 330,067,914 ilipolekewa na kupelekwa kwenye kata kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali lakini kiasi kilichotumika (kwa mujibu wa taarifa hiyo ni Shs 203,917,913 tu. Kiasi cha Shs 126,150,000 hakijatumika mpaka leo na kwa mujibu wa taarifa hiyo kiasi hiki bado kiko kwenye akaunti za kata!!!! Wakati kiasi hiki kikiwa hakijatumika lakini miradi iliyokusudiwa kutekelezwa na fedha hii imejumuishwa katika idadi ya miradi iliyotekelezwa katika miaka 5 ya Halima kuwa mbunge!!! Je miradi hii ilitekelezwa kwa fedha ipi? Maana fedha iliyokusudiwa mpaka leo inasemekana iko kwenye akaunti benki!!! Na kama kweli fedha hiyo iko benki (kitu ambacho sidhani ni kweli) zinafanya nini benki mpaka sasa??? Kwa nini hazijapelekwa kutatua kero za wananchi?? Kama Halima ameshindwa kusimamia utekelezaji wa Shs 330 million alizopewa kwa ajili ya mfuko wa jimbo ili zitumike kutatua kero za wananchi basi hafai kuwa mbunge wetu wananchi wa jimbo la Kawe.

Kwa mfano:

1. Mwaka 2015/16 taarifa inasema shs 3,000,000 zilizopelekwa kwenye kata kwa ajili ya kuchonga barabara ya Gold star bado haijatumika na iko kwenye akaunti ya kata (Ukursasa wa 20) !!!! Yaani kwa miaka 4 hela hiyo imekaa kwenye akaunti ya kata bila kutumika??? Je ni kweli hela hiyo bado ipo kwenye akaunti??? Na kama kweli ipo, je kwa nini haijatumika kwa ajili ya kazi iliyokusudiwa????

2. Mwaka 2016/17 kiasi cha shs 3,000,000 kwa ajili ya kujenga kivuko mbezi shule (ukurasa wa 22) bado iko kwenye akaunti na haijatumika!!!! Pia shs 5,000,000 (ukurasa wa 23) kwa ajili ya kumailizia kituo cha polisi Maputo bado iko kwenye akaunti ya kata na haijatumika!!! Yaani kwa miaka zaidi ya 3 pesa ya mradi kiasi cha shs 8,000,000 bado imekaa kwenye akaunti??? Je fedha hii kweli ipo??? Kwa nini haijatumika kwa muda wote huo???

3. Taarifa ya Halima inaonyesha Pesa ya mfuko wa jimbo kwa mwaka 2017/18 kiasi cha shs 20,000,000 (ukurasa wa 24) mpaka leo haijatumika na bado iko kwenye akaunti ya kata!!!! Mchanganuo wa pesa hii ambao mpaka leo inasemekana iko kwenye akaunti na haijatumika ni kama ifuatavyo: Shs 5 million kwa ajili ya kujenga kivuko cha waenda kwa miguu kata ya Mbezi juu; shs 10 million kwa ajili ya marekebisho ya barabara ya Mbezi mtoni na shs 5 million kwa ajili ya kujenga kivuko cha waenda kwa miguu soko la samaki Ununio. Je fedha hii kweli ipo??? Kwa nini haijatumika kwa muda wote huo???

4. Kwa mujibu wa taarifa ya Halima, mwaka 2018/19 kiasi cha shs 20 million (ukurasa wa 27) ya mfuko wa jimbo iliyopelekwa kwenye kata bado iko kwenye akaunti na haijafanya kazi iliyokusudiwa lakini kwa wakati huohuo ripoti inaonyesha kiasi kilichopo kwenye akaunti ni shs 67,550,000. Sasa sijui kipi ni kipi hapa???!!!! Je fedha ambayo haijatumika kwa mwaka 2018/19 ni shs 20,000,000 au shs 67,550,000? Ni wazi kuwa taarifa hii imepikwa tu na haina mantiki yeyote...

Mchanganuo wa fedha za mwaka 2017/18 katika ukurasa wa 27 hadi 29 unachanganya kweli kweli maana hauoani kabisa na summary katika ukurasa wa 27. Mchanganuo unaonyesha kuwa fedha iliyopelekwa akaunti ya kata ni shs 67,550,000 na haikutumika kabisa!!!! Yaani pesa yote hii mpaka leo bado iko kwenye akaunti za kata!!!! Ajabu kweli kweli...

5. Mwaka 2019/20 (ukurasa wa 30 hadi ukurasa wa 32) unaonyesha kiasi cha shs 27,600,000 zilizopelekwa kwenye kata hazijatumika mpaka leo na bado ziko kwenye akaunti ya kata!!! Mchanganuo wa pesa hii ambayo haijatumika ni kama ifuatavyo: Kujenga kivuko cha waenda kwa miguu mbezi shule (Shs 10 million); Kupanga mawe barabara ya Mbezi mtoni (Shs 15 million); kununua kompyuta ya ofisi ya kata ya Bunju (Shs 600,000); Kumwaga kifusi barabara ya Mbezi tangi bovu (Shs 2 million). Pesa yote hii kiasi cha shs 27,600,000 haijatumika tangu ipelekewe kwenye kata kama kweli ilipelekwa.

Halima amefuja shs 126 million? Kwa mujibu wa taarifa ya Halima; Fedha hii inasemekana kuwa iko kwenye akaunti za kata. Nimefatilia akaunti za kata zote za jimbo la Kawe lakini fedha hizi hazipo. Mtu aliyeshindwa kusimamia fedha yetu hafai kuwa mbunge wetu.
Wewe kuku jike! account za kata kwani zimefichwa kama vote 20? Si zipo wazi mbona unahukumu bila kuthibitisha. Nakutuma kama unatafuta fisadi mfuatilie yule anayekwiba na kuficha mahesamu ikulu vote 20. Jizi unalo jumba jeupe haya sukamataaaa!!
 
Halima amezoea kulia lia ili wananchi wamuone huruma but siku hizi imekula kwake hakuna cha huruma ya wananchi wala nin tuonyeshe ulifanya nini kwanza bila uongo
 
Tarehe 28.10.2020, wananchi wa Tanzania watakuwa katika moja ya majukumu makubwa ambayo pia ni haki na wajibu wao kumchagua kiongozi wanayemtaka ambaye atawaongoza kwa kipindi cha miaka mitano mingine. Wakati kampeni zikiwa zinaendelea za urais, wabunge na madiwani; nikusogezee hali inavyoendelea katika jimbo la Kawe.

Jimbo limekuwa chini ya CHADEMA kwa miaka 10 likiongozwa na mbunge mwanamke Halima James Mdee. Kwa miaka 10 mambo yamekuwa mazuri kwake na huenda alijisahau kwamba maisha yanavyosonga mbele, uelewa unaongezeka, watu wanaendelea kupambanua akili zao na hivyo ni rahisi sana kugundua kuwa wamekuwa wakiibiwa kwa kipindi chote hicho.

Hii inaweka alama nyingine ambayo inaashiria kuwa huenda safari ya kisiasa kwa Halima Mdee ndani ya jimbo la Kawe imefikia mwisho na wananchi wako tayari kubadilisha hali zao kwa kumchagua mtu mwingine anayeonekana kuwa na ushawishi mkubwa na uwezekano wa kutatua matatizo yao.

Jambo linaloshangaza sana ni wanachama wa CHADEMA kuwa mstari wa mbele kuwashawishi wananchi wasimchague Halima kwa kile wanachokisema kuwa wao husahaulika baada tu ya uchaguzi. Hapa awali limeonekana wimbi kubwa la wanachama wa CHADEMA wakitimkia CCM na wote wana kauli moja,"HALIMA UMESAHAU NINI KAWE?, NI ZAMU YA GWAJIMA SASA.

Joseph Sospeter
Kawe-Ukwamani
Yaani umeandika kama bosi wako anavyoongea pumba mara ooh anataka suguliwe na Sugu!

Kwa sasa kipimo cha mwanaCCM halisi ni kutokuwa na akili!

HALIMA MDEE ATAENDELEA KUWA MWANASIASA hata iweje!
 
Mimi ni mwanakawe namtaka, na ninamkubali halima!
Simpendi tapeli Gwajima wala mwenyekiti wenu aliye mpitisha Gwajima kugombea kwa sababu ni kabila lake tu!
mhh unakaa kawe ya wapi ndugu mbona kama hoja za kawe huzijui!!!!! halima katutapeli sana Gwajima tumemchagua
 
Yaani umeandika kama bosi wako anavyoongea pumba mara ooh anataka suguliwe na Sugu!

Kwa sasa kipimo cha mwanaCCM halisi ni kutokuwa na akili!

HALIMA MDEE ATAENDELEA KUWA MWANASIASA hata iweje!
Sijakataa ila atakuwa ni mwanasiasa wa siasa za kilaghai
 
Kwani halima ndio anajenga?
Mbona mnakosa kabisa akili nyie ...
Haya mchagueni anaefufua walikufa, ili mbunge akifa amfufue!
Mmeishazoea kuishi bila vichwa
Babuuu una kichwa au boga?
Mbunge hajengi lakini ana ushawishi na anatakiwa kulobby kupata maendeleo ya jimbo laki.
Halima kutwa kuchwa ni kuingia selo ati anapambana na serikali!
Hatukuchagua mbunge aende kutuhadithi selo ulivyo!
Halima kichwa boga ka wewe ulivyo.
Halima MUST GO!
 
Mkuu
Danpol na Bujibuji hawa waleta Mada wote ni watu wa Gwajima km hawatoki Kanisani kwake basi ni yeye anawalipa, wameweka mada nyingi za uongo kumshambulia Halima Mdee wakati sio wapiga kura wa Kawe
angalia tarehe za kujiunga kwao JF ni kuanzia siku ya Kura za maoni ile July 2020
hizi Mada zao sasa zinachafua Jukwaa nasubiria mwezi huu bado siku 27
 
Back
Top Bottom