MKANGANYIKO WA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA FEDHA YA MFUKO WA JIMBO LA KAWE ZAIDI YA SHS 126 MILLION ZIMEFUJWA….
Nimeipitia taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya fedha ya mfuko wa jimbo la Kawe iliyoandikwa na Halima Mdee (mbunge aliyemaliza muda wake) na kukugundua kuwa taarifa hiyo ni wizi mtupu. Taarifa hii inaonyesha ubadhirifu wa fedha za jimbo na inamwondolea sifa Halima Mdee kupewa hata dakika 1 ya ziada kuendelea kuwa mbunge wa Kawe. Taarifa hii ina uongo mwingi na inaonyesha kuwa kiasi cha zaidi ya Shs 126 milion zimefujwa na mpaka leo hazijatekeleza miradi iliyokusudiwa.
Taarifa hiyo ya mfuko wa jimbo inaonyesha kuwa jumla ya shs 330,067,914 ilipolekewa na kupelekwa kwenye kata kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali lakini kiasi kilichotumika (kwa mujibu wa taarifa hiyo ni Shs 203,917,913 tu. Kiasi cha Shs 126,150,000 hakijatumika mpaka leo na kwa mujibu wa taarifa hiyo kiasi hiki bado kiko kwenye akaunti za kata!!!! Wakati kiasi hiki kikiwa hakijatumika lakini miradi iliyokusudiwa kutekelezwa na fedha hii imejumuishwa katika idadi ya miradi iliyotekelezwa katika miaka 5 ya Halima kuwa mbunge!!! Je miradi hii ilitekelezwa kwa fedha ipi? Maana fedha iliyokusudiwa mpaka leo inasemekana iko kwenye akaunti benki!!! Na kama kweli fedha hiyo iko benki (kitu ambacho sidhani ni kweli) zinafanya nini benki mpaka sasa??? Kwa nini hazijapelekwa kutatua kero za wananchi?? Kama Halima ameshindwa kusimamia utekelezaji wa Shs 330 million alizopewa kwa ajili ya mfuko wa jimbo ili zitumike kutatua kero za wananchi basi hafai kuwa mbunge wetu wananchi wa jimbo la Kawe.
Kwa mfano:
1. Mwaka 2015/16 taarifa inasema shs 3,000,000 zilizopelekwa kwenye kata kwa ajili ya kuchonga barabara ya Gold star bado haijatumika na iko kwenye akaunti ya kata (Ukursasa wa 20) !!!! Yaani kwa miaka 4 hela hiyo imekaa kwenye akaunti ya kata bila kutumika??? Je ni kweli hela hiyo bado ipo kwenye akaunti??? Na kama kweli ipo, je kwa nini haijatumika kwa ajili ya kazi iliyokusudiwa????
2. Mwaka 2016/17 kiasi cha shs 3,000,000 kwa ajili ya kujenga kivuko mbezi shule (ukurasa wa 22) bado iko kwenye akaunti na haijatumika!!!! Pia shs 5,000,000 (ukurasa wa 23) kwa ajili ya kumailizia kituo cha polisi Maputo bado iko kwenye akaunti ya kata na haijatumika!!! Yaani kwa miaka zaidi ya 3 pesa ya mradi kiasi cha shs 8,000,000 bado imekaa kwenye akaunti??? Je fedha hii kweli ipo??? Kwa nini haijatumika kwa muda wote huo???
3. Taarifa ya Halima inaonyesha Pesa ya mfuko wa jimbo kwa mwaka 2017/18 kiasi cha shs 20,000,000 (ukurasa wa 24) mpaka leo haijatumika na bado iko kwenye akaunti ya kata!!!! Mchanganuo wa pesa hii ambao mpaka leo inasemekana iko kwenye akaunti na haijatumika ni kama ifuatavyo: Shs 5 million kwa ajili ya kujenga kivuko cha waenda kwa miguu kata ya Mbezi juu; shs 10 million kwa ajili ya marekebisho ya barabara ya Mbezi mtoni na shs 5 million kwa ajili ya kujenga kivuko cha waenda kwa miguu soko la samaki Ununio. Je fedha hii kweli ipo??? Kwa nini haijatumika kwa muda wote huo???
4. Kwa mujibu wa taarifa ya Halima, mwaka 2018/19 kiasi cha shs 20 million (ukurasa wa 27) ya mfuko wa jimbo iliyopelekwa kwenye kata bado iko kwenye akaunti na haijafanya kazi iliyokusudiwa lakini kwa wakati huohuo ripoti inaonyesha kiasi kilichopo kwenye akaunti ni shs 67,550,000. Sasa sijui kipi ni kipi hapa???!!!! Je fedha ambayo haijatumika kwa mwaka 2018/19 ni shs 20,000,000 au shs 67,550,000? Ni wazi kuwa taarifa hii imepikwa tu na haina mantiki yeyote...
Mchanganuo wa fedha za mwaka 2017/18 katika ukurasa wa 27 hadi 29 unachanganya kweli kweli maana hauoani kabisa na summary katika ukurasa wa 27. Mchanganuo unaonyesha kuwa fedha iliyopelekwa akaunti ya kata ni shs 67,550,000 na haikutumika kabisa!!!! Yaani pesa yote hii mpaka leo bado iko kwenye akaunti za kata!!!! Ajabu kweli kweli...
5. Mwaka 2019/20 (ukurasa wa 30 hadi ukurasa wa 32) unaonyesha kiasi cha shs 27,600,000 zilizopelekwa kwenye kata hazijatumika mpaka leo na bado ziko kwenye akaunti ya kata!!! Mchanganuo wa pesa hii ambayo haijatumika ni kama ifuatavyo: Kujenga kivuko cha waenda kwa miguu mbezi shule (Shs 10 million); Kupanga mawe barabara ya Mbezi mtoni (Shs 15 million); kununua kompyuta ya ofisi ya kata ya Bunju (Shs 600,000); Kumwaga kifusi barabara ya Mbezi tangi bovu (Shs 2 million). Pesa yote hii kiasi cha shs 27,600,000 haijatumika tangu ipelekewe kwenye kata kama kweli ilipelekwa.
Halima amefuja shs 126 million? Kwa mujibu wa taarifa ya Halima; Fedha hii inasemekana kuwa iko kwenye akaunti za kata. Nimefatilia akaunti za kata zote za jimbo la Kawe lakini fedha hizi hazipo. Mtu aliyeshindwa kusimamia fedha yetu hafai kuwa mbunge wetu.