Halima Mdee na wenzake Washinda kesi dhidi ya CHADEMA. Waendelea kuwa wanachama wa CHADEMA. Kuendelea na Ubunge wao

Halima Mdee na wenzake Washinda kesi dhidi ya CHADEMA. Waendelea kuwa wanachama wa CHADEMA. Kuendelea na Ubunge wao

Kwa hivyo watu wanne ndio CHADEMA. Nilitegemea ungeniletea list ya Baraza la wadhamini, kamati kuu, Halmashauri kuu, viongozi wa Kanda etc. Unalitea majina ya watu walishastaafu Tena hawana maamuzi kwenye chama.
Heeeee ,endelea kuamini kuwa mbowe anaweza fanya maamuzi yoyote bila baraka ya baba mkwe
 
Braza sawa ila nasukumwa kuamin hivyo. Mdee hana ubavu huu wa kuipelekesha chadema. Alishindwa Zitto, nin Mdee? Huu mchezo Mbowe ndio Refa anajua kinachoendelea
Mbowe ndiyo anaiendesha mahakama,au umeamua kuanika matope yako hadharani?
Chadema ina wapumbavu wengi
Unaonekana una akili sana,hebi tuambie umesaidia nini nchi hii kwa akili yako?
Acha ushamba
 
Mimi nilishtuka Sana kipindi kile Halina Mdee na wenzake wanaapishwa. Halina Mdee anamshukuru Sana mwenyekiti wake wa chama kwa kuwakubalia. Ingawa chama kilikanusha , ila nilipata wasiwasi Sana
Mbowe kakiua chama ambacho kakipigania maisha yake yote, hadi kakifikisha kwenye hatua nzuri kabisa ya watu kuanza kukifikiria kuwa mbadala wa CCM.
Inashangaza kidogo mtu kama Mbowe kumalizia juhudi zake namna hii.
Anajuwa mwenyewe anayofanya. Lakini ni dhahiri kuwa hana dhamira ya kuiona Tanzania ikiwa huru.

Ile kesi ya 'ugaidi' pamoja na kuwa na ujinga mwingi ndani yake, naona ilimtikisa sana huyu jamaa. Na ukiongeza na jinsi waTanzania walivyo kosa vugu vugu la kuwaunga mkono CHADEMA wakati viongozi wao walipokuwa wakisurubishwa, pengine hasira za kuona watu wanaopiganiwa haki hawastuki, ikawa kichocheo cha kusema 'potelea mbali'!

Uongozi wa kujitoa mhanga, na kupigania haki hauwi hivyo. Kama unaamini jambo, unalisimamia bila kujali hao unaowapigania wameonyesha dalili gani.

Watu kutojitokeza kwenye maswala ya namna hiyo hakuna maana hawaungi juhudi zako.
 
Kwa hivyo watu wanne ndio CHADEMA. Nilitegemea ungeniletea list ya Baraza la wadhamini, kamati kuu, Halmashauri kuu, viongozi wa Kanda etc. Unalitea majina ya watu walishastaafu Tena hawana maamuzi kwenye chama.
Ukitaka kukijua hiki chama vizuri fuatilia movement za mzee mbowe na chawa wake Godblss Lema
 
Kumfukuza mwanachama wa chama chochote kile siyo kama kumfukuza mfanya kazi.

Hususan ikiwa anatowa michango ya chama ya hali na mali.

Wanachama huwa wanafinywa kiaina wajiudhuru wenyewe.

Sasa jigubeli kama halima mdee utalifinya nini ambacho halijawahi kufinywa?
Naona hukumu imejikita kwenye technicality zaidi kuliko kwenye kufukuzwa uanachama. Sijasoma hukumu nzima kuona mambo yaliyokuwa raised na Chadema yamejibiwa je maana kulikuwa lile la kufoji sahihi na barua nadhani. Je, mahakama imesema ilikuwa sahihi au imesemaje? Kama kuna mwenye hukumu nzima angeiweka hapa na ingetusaidia sana.
 
Bado ni wanchama baada ya baraza kuu kunajisi maamuzi ya kamati kuu

Acha uongo na mahakama yako. Baraza kuu lilikuwa linasikiliza rufaa ya akina mdee wakililia uanachama wao, kwa maana hiyo walikuwa sio Wanachama. Hata Kama Baraza kuu lime error.
 
Badala ya kujadili hukumu baadhi ya watu wanaanza kumjadili Mbowe as if kesi ilikuwa ikimhusu yeye binafsi. Sijui ni kwa sababu ni kwa baadhi ya wachangiajia kutojua namna ya kujadili hoja?
 
Hivi ile michango wanayokamua wananchi maskini kwenye mikutano unafikiri ni hela ndogo?embu fikiria ruzuku ya bilion mbili kila mwezi na hata ofisi hawana ?cdm ni zaidi ya ngombe wa maziwa.

Aiseeh! Tangu lini CHADEMA ikapokea bilioni mbili kwa mwezi?. Kwanza unajua hata CCM yenyewe haipokei Ruzuku ya bilioni mbili kwa mwezi?. Tuache kutunga mambo ya uongo
 
Ukitaka kukijua hiki chama vizuri fuatilia movement za mzee mbowe na chawa wake Godblss Lema

Nenda ukafuatilie waasisi wa CHADEMA ni akina nani, achana na stori za akina Lema waliohamia juzi kutoka TLP. Wajute kwanza waasisi wa CHADEMA usipende kuongea mambo juujuu. Na kwa taarifa yako CHADEMA ilianza kuungwa mkono Kigoma baada ya kuwa chama Cha kwanza Cha upinzani kushinda ubunge mwaka 1992.
 
Aiseeh! Tangu lini CHADEMA ikapokea bilioni mbili kwa mwezi?. Kwanza unajua hata CCM yenyewe haipokei Ruzuku ya bilioni mbili kwa mwezi?. Tuache kutunga mambo ya uongo
Wewe unajua wanapokea shilingi ngapi tusahihishe Mangi wangu Mkuu
 
Nenda ukafuatilie waasisi wa CHADEMA ni akina nani, achana na stori za akina Lema waliohamia juzi kutoka TLP. Wajute kwanza waasisi wa CHADEMA usipende kuongea mambo juujuu. Na kwa taarifa yako CHADEMA ilianza kuungwa mkono Kigoma baada ya kuwa chama Cha kwanza Cha upinzani kushinda ubunge mwaka 1992.
Edwin Mtei ndio mwanachama namba moja Bosi
 
Ukisoma vizuri hukumu utaona kwamba mahakama imejikita kwenye technicality zaidi kuliko kwenye kufukuzwa uanachama. Sijasoma hukumu nzima kuona mambo yaliyokuwa raised na Chadema yamejibiwa je maana kulikuwa lile la kufoji sahihi na barua nadhani. Je, mahakama imesema ilikuwa sahihi au imesemaje?

Mahakama imetumia nguvu nyingi kuwakingia kifua akina Halima Mdee. Yani mahakama ilikuwa upande wao. Akina Halima walikuwa sio wananchama wa CHADEMA wakakata rufaa Baraza kuu, Baraza kuu likabariki uamuzi wa kamati kuu. Ila mahakama inasema wajumbe wa kamati kuu ndio walikuwa wajumbe wa Baraza kuu hivyo waliadhiri maamuzi. Sasa itakuwaje mjumbe wa kamati kuu bila kuwa mjumbe wa Halmashauri kuu?.
 
Back
Top Bottom