Hamas warusha makombora Tel Aviv, Israel wapagawa

Hamas warusha makombora Tel Aviv, Israel wapagawa

Wanaukumbi.

Wiki hii nzima Israeli imeteseka L baada ya L; kidiplomasia, kisiasa na kisheria - na sasa: jana askari wao walitekwa kama POWs, na leo Hamas inaonyesha uwezo wao wa kijeshi haujashushwa, kiasi kwamba wameweza kufyatua risasi huko Tel Aviv.

Nentanyahu na wenzake wanasema wananenda Rafah kumaliza vita, Hamas hawapo huko wapo maeneo mengine na leo wamerusha makombora yametua Tel Aviv

====

Al-Qassam launched about 10-12 long-range rockets, from Rafah, travelling 100-110km to hit Tel Aviv, after a hiatus of 4 months. The Iron dome failed to intercept the rockets, more than 8 direct impacts were made, causing material damage and the ignition of fire. 2 settlers were also injured.

Hamas hawana huruma na wapalestina kabisa dunia inawatetea rafah iachwe wenyewe wanatoa kibali kwa myahudi kuifumua rafah ngoja sasa papigwe kapeti bomu
 
Hamas Yuko kama mwanamke kwenye siku zake za hatar atafanya Kila namna ili mradi umtafune tu, hii ni aibu kwa ICJ maana walishawaamuru Israel wasiishambulie Rafah kuepuka maafa Leo Hamas wanarusha rockets kutokea Rafah hii inawapa kibali IDF kuifukumua Rafah wanavyotaka.
Nadhani wamefanya hivyo kutokana na kwamba Israel hakusitisha mashambulizi huko rafah hata baada ya kuzuiwa na icj
 
Muwashughulikie Alqassam Brigades sio raia wa Gaza.
Pekueni mahandaki msilipue hovyo majengo.
Hao alqassam brigades wanavaa kiraia kipindi cha mapigano wengine ni madokta hospitali za gaza, wengine ni UN na wanajichanganya na raia kiufupi raia wa gaza wanatumika kama humansheild
 
Hakuna operation ya kukamata gaidi eti unaua raia. Una bomb hospitals, shule, makanisa, misikiti. Hiyo ni failure ya Intelligence.

Israel wamedhihirisha ni jinsi gani walivyo wachovu kijeshi na kiintelijensia kwa upuuzi wanaofanya hapo Gaza.

Pamoja na mabilioni ya dollar wanayopokea kutoka kwa NATO lakini ni upuuzi tu hamna watu hapo.
Hivi msichokielewa nini mbona imeshawekwa wazi hamas wanatumia hospitali, shule, makanisa, misikiti kujificha na kuficha silaha zao hata israel imeweka huo ushahidi
 
Ni ama amani, au kushambuliana. Kama Hama wanarusha maroketi basi Israel nao wan haki ya kurusha makombora. Dunia inakosea sana inapoilaumu Israel tu na kuwaacha Hamas wafanye watakavyo. Ni ama walaaniwe wote, au waachwe wajiamulie wenyewe.
 
Hao alqassam brigades wanavaa kiraia kipindi cha mapigano wengine ni madokta hospitali za gaza, wengine ni UN na wanajichanganya na raia kiufupi raia wa gaza wanatumika kama humansheild
Unachokieleza IDF waliambiwa wathibitishe ila wakafeli.
Wamekagua kila kona hawakuona silaha hata hizo hospitali walizodai wanajificha.
Kuna madaktari wa UNRWA ambao wazungu walikana na wakatoa ushuhuda kuwa HAKUNA HOSPITALI WALA DAKTARI ANAYETUMIKA NA HAMAS.
We ni nani utoe shutuma hizi!?
 
Hivi msichokielewa nini mbona imeshawekwa wazi hamas wanatumia hospitali, shule, makanisa, misikiti kujificha na kuficha silaha zao hata israel imeweka huo ushahidi
ULETE HUO USHAHIDI HAPA.
ICJ iliwataka IDF wakapeleke ushahidi mahakamani wakaukosa.
Walipeleke staged video zinazoonesha kuna handaki linaelekea Alshifaa hospital,zikakaguliwa na kugundulika ni staged videos/video za kuhaririwa.
Au unachukulia sisi hatufuatilii mzeee!?
 
Muwashughulikie Alqassam Brigades sio raia wa Gaza.
Pekueni mahandaki msilipue hovyo majengo.
Wanashuglikiwa vizuri tu kwani huwa husomi mara kadhaa viongozi wao wakiuwawa na IDF?
 
Ila hamas wakirusha maroketi mnashangilia ila israel ikianza kushusha makombora hapo gaza hamchelewi kukimbilia ICJ na ICC na kuita mauaji ya halaiki gaza kutafuta huruma ya dunia
IDF ikalipue mahandaki na ikawatafute Hamas vichochoroni sio kulipua majengo ya kiraia.
 
Mkuu huna unalolijia kuhusu yanayojiri

Israel ilisambaratisha muungano wa nchi za kiarabu kwasababu walikua wanapambana kwenye uwanja wa vita

Sasa hawa wakuitwa Hamas wanapambana wamezungukwa na raia, wanarusha makombora kwenye nyumba za watu shule misikiti hoapitali sokoni nk
Israel ikiwapiga inaua na raia kibao..... hapa ndio kunachangamoto

Israel inaweza kunyeshea nvua ya mabomu Rafah yote ikawa kifusi ila sasa itaua raia wangapi? Hapa tu inapiga kwa taadhari lakini bado raia wanakufa kama kuku
Upo kishabiki sana, na ndio maana sikuendelea kuisoma komenti yako, matango pori mmelishwa, nanyi kwa chuki zenu kwa dhidi ya waislamu mkaona muendelee kueneza propaganda hizo

Pole sana usie na utu wala huruma, ni heri ukachangie mada za wakongo wanaouwana, huku tuachie wenyewe.
 
Hamas hawana huruma na wapalestina kabisa dunia inawatetea rafah iachwe wenyewe wanatoa kibali kwa myahudi kuifumua rafah ngoja sasa papigwe kapeti bomu
Toka ICJ itoe tamko la IDF kujiondoa Gaza/Rafah je IDF ilishusha bendera za Israel na kuondoka Rafah!?
Hivi hujui kama jana tu kuna baadhi ya askari wa IDF na raia wa kizayuni wamevamia gari ya msaada na kumwaga vyakula na madawa vinavyopelekwa Gaza!?
 
wanarusha makonbora af wanajificha kwenye mashimo na misos wanayoiba kwenye maghala ya misaada wanaoteseka kwa njaa kiu na mabomu ni raia wao walioapa kuwalinda hawa jamaa wanaakili kama wadudu
 
Ni ama amani, au kushambuliana. Kama Hama wanarusha maroketi basi Israel nao wan haki ya kurusha makombora. Dunia inakosea sana inapoilaumu Israel tu na kuwaacha Hamas wafanye watakavyo. Ni ama walaaniwe wote, au waachwe wajiamulie wenyewe.
IDF iondoke Gaza na iache kushambulia magari ya misaada kwa kutumia Israel settlers.
Toka ICJ itoe tamko la IDF kutoka Rafah Israel haikutii na mbaya zaidi wanafanya unyanyasaji wa kimya kimya.
We ulitaka Hamas wafanyaje?
 
wanarusha makonbora af wanajificha kwenye mashimo na misos wanayoiba kwenye maghala ya misaada wanaoteseka kwa njaa kiu na mabomu ni raia wao walioapa kuwalinda hawa jamaa wanaakili kama wadudu
Lete ushahidi wa vyakula kuibiwa na Hamas!?
 
IDF iondoke Gaza na iache kushambulia magari ya misaada kwa kutumia Israel settlers.
Toka ICJ itoe tamko la IDF kutoka Rafah Israel haikutii na mbaya zaidi wanafanya unyanyasaji wa kimya kimya.
We ulitaka Hamas wafanyaje?
Na wewe unaanzia juu juu tu kama hao; ugonvi huu haukuanza juzi bali ulianza mwaka jana October 7th. kosa ni kule kujishahaulisha jinsi ugonvi ulivyoanza na kuanza kulaumu yatokanayo na ugomvi wenyewe.
 
Ni ama amani, au kushambuliana. Kama Hama wanarusha maroketi basi Israel nao wan haki ya kurusha makombora. Dunia inakosea sana inapoilaumu Israel tu na kuwaacha Hamas wafanye watakavyo. Ni ama walaaniwe wote, au waachwe wajiamulie wenyewe.
Israel ametangaza kutotambua kabisa taifa la palestina. Imagine mtu akukute kwako akutowe kwanguvu kwasababu anasema babu zake walikuwepo hapo miaka 3000 iliyopita.
 
Israel ni takataka tu. Kama inachukua karibia mwaka ku deal na wahuni walioko kwenye kamji kadogo kama kijiji siku wakikutana na jeshi kamili siwatasambazwa kama kinyesi tu.
Tatizo umetumia makamasi kufikiri badala ya akili.
Ungetumia akili ungeelewa kuwa hakuna vita rahisi kama ya nchi na nchi kuliko panya
 
Wanaukumbi.

Wiki hii nzima Israeli imeteseka L baada ya L; kidiplomasia, kisiasa na kisheria - na sasa: jana askari wao walitekwa kama POWs, na leo Hamas inaonyesha uwezo wao wa kijeshi haujashushwa, kiasi kwamba wameweza kufyatua risasi huko Tel Aviv.

Nentanyahu na wenzake wanasema wananenda Rafah kumaliza vita, Hamas hawapo huko wapo maeneo mengine na leo wamerusha makombora yametua Tel Aviv

====

Al-Qassam launched about 10-12 long-range rockets, from Rafah, travelling 100-110km to hit Tel Aviv, after a hiatus of 4 months. The Iron dome failed to intercept the rockets, more than 8 direct impacts were made, causing material damage and the ignition of fire. 2 settlers were also injured.

Bi hindu umeanza😂😂😂
 
Back
Top Bottom