Hawa watoto wa Nyerere sio chawa, hawajipendekezi kwa viongozi ili wapewe chakula, baba yao alishawakomaza waishi kibishi toka miaka hiyo. Kwa sasa watawala wanawapa madaraka ili kuficha aibu ya watoto wao au wa marafiki zao wanaowabeba.
Tatizo ni watoto wa hiki kizazi kipya, kilichozoeshwa kuwepo serikalini karibia awamu zote wakiulizwa waoneshe walichowahi kufanya hakuna, na wengi wao wamezoea kubebwa mpaka wanamkasirikia anapokuja asiewabeba, hawaoni aibu.
Wataanza kumchora kwa vikatuni twitter kama vile hii nchi ni ya baba yao, wanajiona wao tu, hawajui kuna watanzania wengine wengi wenye sifa na weledi wa kutosha kushika nafasi walizopo na waka deliver zaidi yao.
Kubebwa kumewapofusha akili zao hawaoni mbele tena, hata wakioneshwa udhaifu wao kiutendaji wanajibu tatizo ni uwaziri wao, ulafi wao umejaa mpaka kwenye akili zao sasa wanadhani kila mkosoaji wao anataka nafasi zao huku "wakiuota" urais.