Mkuu Kalamu1,
Wacha tu nirukie...itifaki imezingatiwa
Ndio nashawishi mjadala makini juu ya 'wanasiasa' kama Jaji Warioba-Mh.Makamu wa kwanza wa Raisi na Waziri Mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mkuu 'SYLLOGIST', unashawishi sana pawe na mjadala makini juu ya watu aina ya Warioba.
Ndio.
Nimekusoma kwa uangalifu sana, lakini nikiri kabisa bado sijakuelewa barabara.
Kwa kutoweza kunielewea "barabara" kwa maoni yangu, hakumaanishi wala kusababisha wewe ni baradhuli-haujabisha ushwawishi wangu uliouona wewe.
Kweli kuna sababu nyingi tu za kuwa na umakini katika kujadili 'wanasiasa' kama Jaji J.S Warioba. Wangalau tunaafikiana hapo.
Hoja yako imejikita kwenye mhtasari wa mstari huo hapo juu, na hasa kwenye haya maneno "...Heshima ya nchi yake na heshima Chama." (?)
Nikusahihishe "...Heshima ya nchi yake na heshima ya chama"
Haswa, kwa maono yangu, amekuwa mstari wa mbele kwakuwa ni nyota wa heshima ya nchi na Chama chake CCM-sidhani utalipinga hili- mfano kumekuwa na mitiririko ya Viongozi wa juu, wa Vyama na Serikali wa nchi hii 'kwenda kwake' kwa sababu wanazozijua wao. Kwa maoni yangu, ni kwasababu ya tunu ya heshima ya nchi aliyokuwa nayo na unguli wa Kisiasa nje na ndani ya Chama chake cha CCM, pamoja na kuonekana utofauti wa mihimili na misimamo ya sasa ya CCM, Mzee Warioba, again, bado ni mmoja wa wengi mwenye mhimili na msimamo wa Kale wa CCM wa kujikomboa na fikra za kiafrika.
Kuhimiza uwepo wa Katiba Mpya ni kupingana na 'Heshima ya nchi'?
Hapo juu Mkuu Kalamu1 sijakuelewa, unauliza rhetorically? Je ni wewe unayohimiza au ni Jaji Warioba?-Au yeye Warioba kuhimiza katiba 'kwa mantiki ya "woga" wake-atakuwa anankinzana na utunzaji wa... Heshima yake ya Nchi na ya CCM? Sijui, lakini nafikiri unaweza kunielewesha.
CCM kama chama, baada ya yote kilichokwishapitia chama hicho toka enzi za Mwinyi hadi leo hii, bado Mzee Warioba na wazee wengine, kweli bado wanaona kuna "Heshima" ndani ya chama hicho, inayowafanya wasiseme lolote juu yake, kweli?
Kwangu mimi naona swali hili litanilengesha kujibu nisoyoyajua. Siwezi kukujibu-nafikiri ulielekeze kwa hao wazee-lakini inajulikana wapo wazee wengi tu amabao wanasema mengi(lolote) kuhusu 'Heshima' ya CCM
Mkuu inawezekana sijaelewa vyema na kuzoea jinsi ya muwasilisho wako wa hoja, ndiyo sababu ninashindwa kukuelewa vizuri unachoandika hapa.
Lakini ninaheshimu sana ulivyowasilisha hoja zako. Natamani tu kama ningeelewa maana hasa ya unachonuia kueleza.
Kutonielewa 'vyema' na muwasilisho wa "hoja" haukufanyi wewe ni baradhuli, kwani sio kawaida ya mijadala mitandaoni kuwasilisha hoja kwa mpangilio au kuwa na hitimisho linalofuata mantiki. Nilikurupuka.
Kwa bahati nzuri, umemtaja pia Salim katika andiko lako, na kwa bahati nzuri, huyo pia nilisha mtaja pia ndani ya mijadala humu JF katika maudhui kama haya haya tunayoyajadili hapa leo.
Bado kabisa ninaamini kwa dhati ya moyo wangu kwamba watu wenye hadhi kama ya Warioba, hawana chochote cha kupoteza, ila wana kila kitu cha kuwapa heshima kubwa ndani ya Taifa hili, kama wangesimamia na kueleza wanachokiamini juu ya maslahi ya nchi hii.
Sielewi maana ya kuwa "Nguli wa Siasa za nyakati" zinavyosaidia chochote kwa ukimwa wake.
Sawa.
"Strategic", kwa vipi? Hapa nadhani umeniuzia tu maneno bila ya kujali nitaelewa au la!
Ha ha naona ni kweli nilifanya bila ya kuzingatia, lakini sio kwa kusudi la kuuza neno au maneno. "Werevu' that is the word!🤔
Kalamu1 tukitumia kichwa cha bandiko na maudhui ya mleta mada-tuko nje. Tukubaliane hapo.
Kilicho kuwepo kwenye maudhui, kwa maoni yangu, ni tofauti na mjadala wetu hapa. (Kuhusu aina ya Wanasiasa kama Warioba)
Kitu tunaweza kuafiki ni kuwepo mjadala makini kuhusu "aina" ya watu au wanasiasa kama Warioba?
Naomba nikiri pia-Nilikurupuka na kuingilia swali uliloelekeza kwa JokaKuu bila ya kujijua-nilikurupuka! Sikuwa nimenuia hivyo, kuingilia hoja mlizoziibua kati yako na mzee JokaKuu. Kumradhi
Ukifika wakati muafaka niko tayari tukajadiliana, nje ya mada hii.
Ahsante