KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Mkuu 'SYLLOGIST', unashawishi sana pawe na mjadala makini juu ya watu aina ya Warioba.Hivyo basi, sio woga, sio heshima kibinafsi, sio kulinda watoto-huu mjadala mwingine- bali Heshima ya nchi yake na heshima ya Chama. Kama nilivyosema juu, Ni nguli wa Siasa za nyakati. Strategic.
Nimekusoma kwa uangalifu sana, lakini nikiri kabisa bado sijakuelewa barabara.
Hoja yako imejikita kwenye mhtasari wa mstari huo hapo juu, na hasa kwenye haya maneno "...Heshima ya nchi yake na heshima Chama." (?)
Kuhimiza uwepo wa Katiba Mpya ni kupingana na 'Heshima ya nchi'?
CCM kama chama, baada ya yote kilichokwishapitia chama hicho toka enzi za Mwinyi hadi leo hii, bado Mzee Warioba na wazee wengine, kweli bado wanaona kuna "Heshima" ndani ya chama hicho, inayowafanya wasiseme lolote juu yake, kweli?
Mkuu inawezekana sijaelewa vyema na kuzoea jinsi ya muwasilisho wako wa hoja, ndiyo sababu ninashindwa kukuelewa vizuri unachoandika hapa.
Lakini ninaheshimu sana ulivyowasilisha hoja zako. Natamani tu kama ningeelewa maana hasa ya unachonuia kueleza.
Kwa bahati nzuri, umemtaja pia Salim katika andiko lako, na kwa bahati nzuri, huyo pia nilisha mtaja pia ndani ya mijadala humu JF katika maudhui kama haya haya tunayoyajadili hapa leo.
Bado kabisa ninaamini kwa dhati ya moyo wangu kwamba watu wenye hadhi kama ya Warioba, hawana chochote cha kupoteza, ila wana kila kitu cha kuwapa heshima kubwa ndani ya Taifa hili, kama wangesimamia na kueleza wanachokiamini juu ya maslahi ya nchi hii.
Sielewi maana ya kuwa "Nguli wa Siasa za nyakati" zinavyosaidia chochote kwa ukimwa wake. "Strategic", kwa vipi? Hapa nadhani umeniuzia tu maneno bila ya kujali nitaelewa au la!