Hapa Makongoro Nyerere kaamua kusema ukweli mbele ya Rais bila kupepesa macho

Makongoro alienda vita ya Uganda bila hata baba yake kujua, Makongoro alijiunga na upinzani NCCR na kupata Ubunge.

Makongoro aliwahi kukataa ubunge wa kuteuliwa na Mkapa.

Kama jina la Nyerere ndio linambeba mbona lisiwabebe hao watoto wengine wa Nyerere?
 

Hapo kawapelekea ujumbe wenzake wa mbeleko za chuma. Anawauliza wameifanyia nini nchi? Pia kasema ukweli mtoto hachagui Baba. Mbona watoto wa Walimu wakiwa Walimu watu hawapigi kelele wanabakia kusifia yaani huyu kama Baba yake? Au kwa vile wamefaulu mitihani ya uwalimu?
 
Nadhani wengi hamjamuelewa Makongoro. Alicho maanisha ni kwamba kuna mambo mengi wamayafanya lakini hayajulikani, hayaandikwi popote..hivyo watu wanadhani wako hapo walipo kwa sababu ni mtoto wa fulani.
Wewe ndiye umeelewa hivyo? Bila yeye kusema hilo unafikiri hawa wanao ramba asali kwa urefu wa kamba zao wangeweza sema hilo?
 
Halafu Jaji Warioba kama vipi atusaidie kupata Katiba yetu. Tumechoka kupigwa kalenda na Wanasiasa! Na hasa wale wa kutoka CCM.
 
🀣🀣🀣
KIDUMU CCM

#Siempre JMTπŸ™
 
Jamaa haaminiki masihara mengi
 
Mwl alizingatia sana suala la uwanadamu na akiona kuwa huna uwanadamu alikuwa hasiti kama akipata nafasi kumuambia mteuaji huyo hana uwanadamu. Katika wateuliwa ni nani hana uanadamu na kwa nini?
 
CCM ni ukoo wa kambale, baba, mama, watoto wote misharubu
 
Mheshimiwa, hivi unawafahamu vizuri wale form four failures kweli? Wale wapumbavu wanaweza kushindwa kuelezea maana ya PGO! Ila siyo kupiga watu virungu na kuwaua.

Sasa usawa huu unavunjwa miguu, kiuno, au kuuwawa kabisa! Nani atawalea watoto wangu wadogo? Hii ndiyo sababu wengi tunaogopa kuingia mitaani kuidai hiyo Katiba Mpya. Labda wabadilishe mitaala yao kwanza. Hii ya sasa nguvu zinatumika sana kuliko akili.
 
Halafu Jaji Warioba kama vipi atusaidie kupata Katiba yetu. Tumechoka kupigwa kalenda na Wanasiasa! Na hasa wale wa kutoka CCM.
Tupiganie katika constitution iwe inamshitaki mtawala na asiwepo mtu ambaye sheria haimgusi. Hiki kitu muhimu sana. Kapigania katiba ya kwanza hicho kifungu hakikuwepo. Je katiba ya pili kitakuwepo? Bila hicho kifungu kuwekwa katika katiba ni sawa na mechi bila refa.

Halafu mchakato wa katiba ni msamiati wa kupotosha tuu. Wewe weka wasomi wawili tuu wa sheria halafu tuwape imprest na posho ya nguvu. Amin amin nawaambia, wiki moja tuu utapata katiba nzuri sana kupita ya mataifa makubwa.

Hili neno "mchakato wa katiba" halina mantiki yeyote kisheria. Wewe sema kuundwa kwa katiba mpya na wataalamu wa wizara ya sheria linaeleweka.
 
Watu wanafadhiliana!! Kwa kujuana!! Ujumbe umefika!
 
Duh!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…