Hapa Makongoro Nyerere kaamua kusema ukweli mbele ya Rais bila kupepesa macho

Hivyo basi, sio woga, sio heshima kibinafsi, sio kulinda watoto-huu mjadala mwingine- bali Heshima ya nchi yake na heshima ya Chama. Kama nilivyosema juu, Ni nguli wa Siasa za nyakati. Strategic.
Mkuu 'SYLLOGIST', unashawishi sana pawe na mjadala makini juu ya watu aina ya Warioba.

Nimekusoma kwa uangalifu sana, lakini nikiri kabisa bado sijakuelewa barabara.

Hoja yako imejikita kwenye mhtasari wa mstari huo hapo juu, na hasa kwenye haya maneno "...Heshima ya nchi yake na heshima Chama." (?)

Kuhimiza uwepo wa Katiba Mpya ni kupingana na 'Heshima ya nchi'?

CCM kama chama, baada ya yote kilichokwishapitia chama hicho toka enzi za Mwinyi hadi leo hii, bado Mzee Warioba na wazee wengine, kweli bado wanaona kuna "Heshima" ndani ya chama hicho, inayowafanya wasiseme lolote juu yake, kweli?

Mkuu inawezekana sijaelewa vyema na kuzoea jinsi ya muwasilisho wako wa hoja, ndiyo sababu ninashindwa kukuelewa vizuri unachoandika hapa.
Lakini ninaheshimu sana ulivyowasilisha hoja zako. Natamani tu kama ningeelewa maana hasa ya unachonuia kueleza.

Kwa bahati nzuri, umemtaja pia Salim katika andiko lako, na kwa bahati nzuri, huyo pia nilisha mtaja pia ndani ya mijadala humu JF katika maudhui kama haya haya tunayoyajadili hapa leo.

Bado kabisa ninaamini kwa dhati ya moyo wangu kwamba watu wenye hadhi kama ya Warioba, hawana chochote cha kupoteza, ila wana kila kitu cha kuwapa heshima kubwa ndani ya Taifa hili, kama wangesimamia na kueleza wanachokiamini juu ya maslahi ya nchi hii.

Sielewi maana ya kuwa "Nguli wa Siasa za nyakati" zinavyosaidia chochote kwa ukimwa wake. "Strategic", kwa vipi? Hapa nadhani umeniuzia tu maneno bila ya kujali nitaelewa au la!
 
watu wengi wamepima alichosema sio alichokunywa, kazi yetu nikutafakari watoto wengi wavingozi wamekuwepo ktk nyakati nyingi wamelifanyia nn taifa?

..Dr.Mwele Malecela aliitumikia Tz na kutuheshimisha kimataifa.
 
..kwa Mzee Warioba ni bora wananchi tuuwawe, tutekwe, tudhalilishwe, lakini serikali na watawala wasipoteze heshima yao.

Cc Kalamu1
Mkuu 'Joka', nimemsoma 'SYLLOGIST' juu ya jibu lake kwangu sikumwelewa.

Sasa nageukia kwenye haya yako, sifa uliyompa ya "ulainilaini" labda itanisaidia kumwelewa vizuri huyu mzee.

Nikimtazama wakati ule wa Kikwete, alipokuwa tayari kutoa hoja zake kwenye makongamano, hadi pale alipovamiwa na Bashite pale Ubungu Plaza, nashawishika kidogo kuamini unayoyasema juu ya hulka za "ulainilaini" wake.
Nakumbuka, baada ya msukosuko ule, huyu mzee hakusikika tena!

Sasa, hata kama ni kuogopa kufa, si watu hufa kila siku jameni?

Katika umri ule, akifa kwa sababu ya kutetea maslahi ya nchi yake, kuna kifo gani tena chenye heshima zaidi ya hicho?
 
Mkuu, kwanza kabisa, kabla ya yote, huwezi kumweka Mzee Warioba katika kundi hilo la "Lowasa na Sumaye", nadhani hata wewe mwenyewe utajishangaa kwa kufanya hivyo.

Halafu unasema:
Yaani Mzee Warioba ajitoe mhanga namna hii kweli, kwa lipi? Mbona mnamtwisha zigo mzee wa watu!

Kwanza ni kwa uwezo gani ambao pengine mnadhani anao?
Kwa "uwezo gani",? wewe unataka uwezo wa namna gani. Umesema mwenyewe nafasi alizokwishashika serikalini, una maana hakuonyesha uwezo wowote huko?

Sasa unabeza juu ya "Uenyekiti wake"..., wewe ulitakaje? Hakufanya kazi vizuri iliyoonekana kwa watu?

Halafu unazungumzia mambo ya ajabu sana: "uspecial wa kutingisha mhimili", kwako ina maana watu waache kusema au kufanya kitu chochote kwa vile kinahusu "Mhimili"? Mawazo gani haya!

Naona nimepoteza muda wangu kujibu mambo ya kipuuzi kabisa uliyoandika hapo juu.
 

..kwenye kongamano la kumbukumbu ya Maalim Seif Mzee Warioba au Butiku alikuwa anawasihi baadhi ya wachangiaji wasizungumze " kila kitu."

..kuna kongamano lingine wakati ule Dr.Slaa akiwa Katibu Mkuu wa Chadema, wazee hao tena walikuwa wanawapoza watu waliokuwa wakiikosoa serikali.

..Sidhani kama Mzee Warioba yuko tayari kubeba jukumu ambalo Watanzania wanamhitaji alibebe. Mzee yuko too loyal kwa Ccm na watawala ni si kwa wananchi.

..Mzee Warioba ni mtu mwema, lakini si mtu jasiri. Tanzania inahitaji Mzee jasiri.
 
Basi tuwataje kwa majina hawa watu, na dunia ijue.
Mwingine wa aina hiyo anaitwa Msekwa, Pius Msekwa. Kuna wengine wengi.
 
Pamoja na mapungufu yake hana majivuno hajui kuiba

Sasa akina nanihiiii dah wamegeuza nchi ya baba zao

Huwa najiuliza ni wao tu ndio wawe watawala majina yaleyale mambo mbofumbofu yale yale si walisomeshwa shule kwa kodi zetu Kwa nini hawafanyi kazi kama wengine? Kwa nini kodi zetu ziendelee kuwalea
 
Potelea mbali! kumwaga mchele kwenye kuku wengi kuna saa haina shida kabisa inaruhusiwa πŸ˜‚
Piga k.vant zako endelea kufunguka mzee wangu.
 
Anastahili PhD ya ujasiri, he is very clever
 
Kwamba ni kilaza na kabwebwa na umaarufu wa baba yake.. Hawa ndio wenye ccm yao wasiotaka kusikia kitu kinaitwa katiba mpya
 
Akijenga heshima... So what?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…