Hapa ndio ninapokuwa na walakini na uwepo wa Mungu

Ushahidi gani unataka na mateso yao unayaona?

Kuteseka kwao ni uthibitisho tosha kwamba Mungu Kashindwa kuwasaidia.

Huyo Mungu angekuwa anasaidia, Kusingekuwa na watu wanao teseka. Duniani.
Kushindwa kusaidia na kutosaidia tu ni tofauti, wewe unatuambia kashindwa kusaidia sasa labda ueleze kashindwa kwa namna ipi? Kwamba hana uwezo wa kusaidia au kaamua tu kutosaidia?
 
Kuna uhusiano gani wa kuwepo Mungu na hayo unayoyasema? Kwamba uwepo wa Mungu unategemea na yeye kutoa msaada?

Hebu nieleweshe.
Anakinzana na sifa zake mnazomwelezea:

1.Mwenye Upendo
Utaacha viumbe ulioumba mwenyewe wateseke ili hali unaweza kuwanasua kwenye huo mkwamo!

2.Mwenye Kusamehe
Alimtupa kuzimu shetani kwa kosa moja tu!

Fikiria hizo mbili, halafu tuambie huyu fictional character wenu kama sio fake ni nini?
 
Sasa akijitokeza hadharani na kila mtu akajua uwepo wake bila utata je hapo itakuwa suala la kuamini tena? Hebu nieleweshe.
Halitakuwa suala la kuamini tena.

Litakuwa suala la kujua kwa uhakika kabisa kwamba Mungu yupo.
 
Kushindwa kusaidia na kutosaidia tu ni tofauti, wewe unatuambia kashindwa kusaidia sasa labda ueleze kashindwa kwa namna ipi? Kwamba hana uwezo wa kusaidia au kaamua tu kutosaidia?
Mungu anaaminiwa kwamba ana uwezo wa kila kitu, Lakini Mungu huyo kashindwa kusaidia chochote kile. Hivyo Mungu mwenye uwezo wa kila kitu, Hayupo.

Mungu anaaminiwa kwamba ana upendo na huruma sana, Kama kaamua kutosaidia, Basi ni makusudi.

Na kwa maana hiyo, Mungu mwenye upendo na huruma, Hayupo.

Sifa za Mungu ndizo zinamfanya asiwepo.
 
1) Hii hoja ingekuwa na mashiko kama Mungu angekuwa ameahidi kwamba hatoacha wala kuruhusu kiumbe ateseke hapa duniani kwa sababu yeye ana upendo, kwa sababu yapo mambo mengine ambayo huonyesha hiyo sifa ya upendo wa Mungu.

2)Kuna visa vingi sana venye kuonyesha sifa ya Mungu ya kusamehe, na hadi sasa bado ipo ofa ya watu kusamehewa kwa sababu ya hiyo sifa ya kusamehe.

Ndio maana nashangaa kutumia hizo hoja kufanya hitimisho la kusema hakuna Mungu. Hizo sifa za Mungu zipo nyingi hili nalo mlizingatie.
 
Ngoja nukasevu mahali😀 😀
 
Mpumbavu husema moyoni, Hakuna Mungu; Ni wafisadi, na wametenda mambo ya kuchukiza, Hakuna atendaye mema. Zab 53:1
 
Hoja bado dhaifu, wapi Mungu aliahidi kusaidia?
Yani kwa sababu tu ana sifa ya upendo na uwezo ndio analazimika kusaidia kwa kila jambo kisa ana hizo sifa?

Halafu ipo mifano yenye kuonyesha uwepo hizo sifa, sasa utasemaje sifa zinamfanya asiwepo?
 
Halitakuwa suala la kuamini tena.

Litakuwa suala la kujua kwa uhakika kabisa kwamba Mungu yupo.
SUnaona sasa? lengo la Mungu ni imani watu kumuamini ila wewe unataka isiwe imani, ndio maana numekuwa nauliza kipi kinamfanya alazimike yeye kujionyesha?

Ndio maana yanaelezwa faida na hasara za kuamini na kutoamini.
 
Hoja bado dhaifu, wapi Mungu aliahidi kusaidia?
Yani kwa sababu tu ana sifa ya upendo na uwezo ndio analazimika kusaidia kwa kila jambo kisa ana hizo sifa?

Halafu ipo mifano yenye kuonyesha uwepo hizo sifa, sasa utasemaje sifa zinamfanya asiwepo?
Mungu hajawahi kuahidi kusaidia. Mungu hayupo.

Nimekujibu hivyo kulingana na wewe ulivyo niuliza swali lako kwenye post #81.

Uliuliza hivi "Mungu kashindwa kusaidia au kaamua kutosaidia"

Mungu hayupo kwa namna yoyote ile.

Kwanza, Hakuna uthibitisho wowote wa uwepo wake, yeye kama yeye. Ni imani tu zisizo na uthibitisho wowote ule.

Pili, Sifa anazosifiwa na kudaiwa kwamba huyo Mungu anazo, zinapingana waziwazi na uhalisia ulivyo.

Hivyo hakuna Mungu.
 
Hata kama ni mipango ya shetani ila watendaji ni binaadamu wenyewe, shetani hamforce mtu kufanya kitu.
HAA!! 🙄🙄 Hii mpya.

Ikiwa Shetani hamfosi mtu kufanya uovu, Je binadamu ametoa wapi akili ya kufanya maovu?
 
SUnaona sasa? lengo la Mungu ni imani watu kumuamini ila wewe unataka isiwe imani, ndio maana numekuwa nauliza kipi kinamfanya alazimike yeye kujionyesha?

Ndio maana yanaelezwa faida na hasara za kuamini na kutoamini.
Mimi sitaki isiwe imani.

Kuwa na imani na kuamini ni haki yako ya kikatiba kabisa. Unaweza kuchagua kuamini chochote utakacho hata mawe, miti, mapango, majabali n.k

Lakini ukianza kudai kwamba imani yako ina ukweli lazima uthibitishe hilo.
 
Mpumbavu husema moyoni, Hakuna Mungu; Ni wafisadi, na wametenda mambo ya kuchukiza, Hakuna atendaye mema. Zab 53:1
Huyo Mungu, Kwa nini aliumba binadamu wapumbavu wanaosema yeye hayupo?

Huyo Mungu, Alishindwaje kuumba binadamu wema tu watakao sema yeye yupo siku zote na wakati wote?

Hivi huyo Mungu anajielewa kweli?

Huyo Mungu kama aliumba binadamu wenye uwezo wa kusema yeye hayupo, Halafu anataka asemwe yupo, Basi Mungu huyo pia ni Mpumbavu sana.
 
Hakuna hizo hoja kabisa.
Hivyo visa vingi ni vipi?
Hakuna Mungu huu ndio ukweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…