Harusi ya Majizzo, Millard Ayo: Vijana matajiri hawapendi kuchezea pesa zao wala kusumbua watu na michango

Harusi ya Majizzo, Millard Ayo: Vijana matajiri hawapendi kuchezea pesa zao wala kusumbua watu na michango

Nilishaliongelea hili swala. Mambo ya kuchangishana yanakera mno! Tena unakuta lijitu hata hamna mazoea, kama mpo ofisi moja linajinunisha ovyo sometimes linakwamisha mishe za kazi.

Then ghafla likitaka kuoa au kuolewa linajifanya liko poa linajichekesha chekesha ovyo na kuanzisha shobo, linakuvutia timing likupe kadi ya mchango ulichangie. Sifanyi upumbavu huo!!!
 
Hili suala ni mapenzi ya mtu. Kama ameamua kufanya harusi kubwa ama la....
Kuhusu michango ni hiari yako kutoa ama la....
Kama hutaki kutoa ww sema live kuwa hutoi au huna hela sio unapigiwa simu ooh nitatoa mwisho wa mwezi ukitafutwa mwisho wa mwezi unaona usumbufu. We sema tu jamani Mimi nimebanwa Sina hela uone Kama utasumbuliwa.
 
Huyo kijana ni msomi wa level gani ya elimu? Aache ujinga wa kusumbua watu ili wamchangie kufanya harusi kwa kutegemea mifuko ya watu. Kwani akioa kimya kimya padri/mchungaji atamtenga na kumfukuza kanisani kisa kaoa gizani? Huu utamaduni wa kuchangia hurusi umepitwa na wakati na unaonekana ni usumbufu kuombaomba hela kwa watu wakati suala la kuoa ni la mtu binafsi na ni hiari. Hayo ni matumizi mabaya ya hela za watu, ni ufahari, anasa na starehe. Kwani bila michango ndoa hifungwi?
 
Huyo kijana ni msomi wa level gani ya elimu? Aache ujinga wa kusumbua watu ili wamchangie kufanya harusi kwa kutegemea mifuko ya watu. Kwani akioa kimya kimya padri/mchungaji atamtenga na kumfukuza kanisani kisa kaoa gizani? Huu utamaduni wa kuchangia hurusi umepitwa na wakati na unaonekana ni usumbufu kuombaomba hela kwa watu wakati suala la kuoa ni la mtu binafsi na ni hiari. Hayo ni matumizi mabaya ya hela za watu, ni ufahari, anasa na starehe. Kwani bila michango ndoa hifungwi?
Tena wale wanaojiita wasomi ndiyo wapenda kuchangiwa
 
Hawa makapuku ndo wanaotulazimisha michango ya double na single alafu ndani ya mwezi wanaachana...

Saivi mkiachana tunakuja kudai michango tuliyowapa
kuna msela mmoja aliwaingiza chaka wachangiaji, alikusanya michango ya harusi akafungua duka kwa kugeuza michango ya harusi kuwa mtaji wa biashara. Harusi alienda kufungia bomani, yeye, mke wake na mashahidi wawili mchezo ukaisha hapo
 
Inatokea nachaguliwa kuwa mwenyekiti wa kikao cha kamati ya harusi. Swali la kwanza huwa nawauliza waoaji, unataka kufanya harusi ya gharama kiasi gani? Akitaja gharama kubwa huku yeye hana uwezo wa kuchangia hata robo najiuzulu hapohapo kikaoni wateue mwenyekiti mwingine anayekubaliana na ujinga wa muoaji.
 
Saa nyingine utakuta hutaki kabisa hayo mambo ila familia zinalazimisha hasa mama. Sisi mama zetu na dada huwa wana mitazamo tofauti sana. Siku ya graduation yangu nilimpa dada Tsh laki 3 aniandalie tu msosi kidogo na vinywaji kwa ajili ya familia na watu wengine wachache. Mama sikumshirikisha kwasababu najua tusingeelewana. Siku ya Graduation baada ya pilika za pale chuo ndo ninatoka niende home nashangaa kuona kundi kubwa la ndugu, marafiki na jamaa wamejitokeza. Nashangaa zaidi naambiwa panda gari hili limeandaliwa kwa ajili yako. Badala ya kuelekea nyumbani tukaelekea kwenye ukumbi fulani kuna hadi Muziki umeandaliwa. Yaani ni sherehe kubwa ya zaidi ya milioni kwa wakati ule. Kumbe mama na dada waliamua kutonishirikisha kabisa kwenye mipango yao na kuamua kufanya kila kitu wenyewe kwa gharama zao.
 
Kuna jamaa yangu wakati tuko chuo alikuja kunipiga kirungu cha elf 5 akasema atanirudishia kipindi icho na kaa geto alone pasi ndefu kawaida alaf kaja kunikopa kanililia shida siunajua watoto wa dar es salaam wanavyojua kujiposition kapuku ila hataki kukubali sasa najiuliza huyu amependeza alaf hata buku hana alaf anatumia simu ya bei alaf na mimi sielewi imabidi nimpe buku 5 yangu ya bajeti sasa imefika kipindi cha kurudisha kila nikimcheck ananiletea zengwe ooohh na wewe mpaka 5000 unaidai aiseee ikabidi nikaushe tu…
Sasa juzi kanitafuta anataka kuoa eet ni mchangie nikaitikia tu sawa nikajisemea tu kimoyo moyo yani huyu elf tano yangu hakunirudishia leo nimchangie af anapost mapicha akiwa kaenda sijui SA mara yuko mlimani city anakula nyama tu shwain zake bado niko nawaza hapa nimchangie nikijumlisha na ile deni langu yani awee ameshinda yeye alaf pia sina uhakika kama kweli anaoa maana jamaa ni janja janja sana any way ngoja nikilewa ntajua
 
Hakuna dhambi ukiamua kuoa, huko huko mlipokubaliana muishi mume na mke hata kama mlikutana vichakani mkaanza kunyanduana shahidi ni Mungu ndiye aliyeshuhudia mkianzisha mahusiano ya kuunda familia. Hizi zingine ni mambo ya ziada tu, kupeana mi certificate ni utaratibu tu usio na lazima. Mara vifijo na nderemo kwenye nyumba za ibada na ukumbini, hizo ni show tu zisizo na maana, ni fasheni tu. Ndoa ni muunganiko wa nafsi kati ya mwanaume na mwanamke walioungana kuishi pamoja katika hali zao za maisha. Maisha ni yao yawe ya shida au raha wamekubaliana wakabiliane na hali hizo. Hayo mambo ya shamrashamra za gharama ni anasa na starehe tu. Sasa starehe zako uwasumbue wengine wakuchangie? Jamii ya kipuuzi ndiyo hukubaliana na mambo ya kupuuzi yafanyike
 
Back
Top Bottom