Harusi ya Majizzo, Millard Ayo: Vijana matajiri hawapendi kuchezea pesa zao wala kusumbua watu na michango

Harusi ya Majizzo, Millard Ayo: Vijana matajiri hawapendi kuchezea pesa zao wala kusumbua watu na michango

Najua wanawake wanapenda kuolewa kwa harusi kubwa kubwa.

Na maskini tupo weak sana kwa wanawake.

Tajiri hatingishwi na mwanamke.. mwanamke anafata anachotaka mwanaume na habishi maana anajua akigoma kumpata mwanaume tajiri sio kazi ndogo

Majizo hakutumia nguvu kumwambia lulu harusi ya mbwembwe sitaki. Maana lulu anajua akigoma kumpata mume kama majizo sio kazi ndogo.

Millard ayo nae hivyo hivyo mkewe amefata maelekezo tu.

Sisi maskini tunafosi kufanya wanawake wanachotaka cha harusi za show off kwa kubeba madeni ili wanawake zetu wajue tunawapenda wasitukimbie.

Ndio haya mambo ya kuadd watu magrupu ya michango kinguvu
Ulitaka mashoga waje kumuaibisha harusini
 
Pole mkuu. Mi waliniunga group la harusi simjui ata member mmoja wala bwana harusi.

Nikaahidi nitatoa laki 5 hafu nikaleft. Nilitafutwa aisee ova sio SMS sio kupigiwa. Akijitambulisha tu anakula block.
khakhakhaaaa!
 
Michango ya harusi sio lazima, huwezi kuoa kama huna hela. Binamu yangu mmoja hata miaka 30 hajafikisha, ashaoa mara tatu, harusi zote sherehe kubwa kubwa. Zile ni akili za kushikiwa na mamaake.
 
Habari wadau,

Nimeungwa group la harusi ghafla la kijana mfanyakazi mwenzangu anadai michango ya harusi yake.

Nimesoma Bajeti ya harusi yake ni milioni 25.

Nikawaza huyu jamaa ni maskini mwenzangu. Anategema ajira na mshahara ni wa kawaida tu.

Why ana akili ndogo namna hii ya kuchezea pesa.

Mbona vijana waliofanikiwa na wenye utajiri wa mali na utajiri wa watu na connections kali hawapendi mbwembwe wameoa kwa harusi za kimya kimya.

Millard Ayo ni kijana aliyefanikiwa mwenye utajiri wa kutosha tu. Marafiki anao kibao wa kuwachangisha, ila hakufanya hivyo wakati anaoa alioa kimya kimya harusi simple ya kwenda kanisani tu na mkewe kisha kila mtu kwake. Hakuna cha ukumbi wala cha Mc garab wala nani.

Majizo nae mmiliki wa efm hivyo hivyo alioa kimya kimya, yeye na lulu kanisani tu then kila mtu kwake.

Why na kina sisi vijana maskini hatujifunzi. Yaani mtu anachukua mkopo ofisini kwa ajili ya kufanikisha harusi.

Mtu anasumbua watu michango kisa harusi.

MASKINI TUNA UJINGA MWINGI SANA
solution ni kuto kuoa
 
Sema Milard saa nyingine anaboa. Yale maisha anayoishi ni ya kipumbavu sana. Kina Zuckerberg na mabilioni yao ya USD hawajibani kama yule jamaa. Wanasema kila mtu na furaha yake ila hela zinahitajigi kelele kidogo sometimes... mimi kwangu Millard sio mfano wa kuigwa kwenye hizi ishu za mapenzi na mahusiano.
Mbna unampangia maisha mwenzio?? Duuuh
 
Kumbe Millard ameoa?? Aisee limenipita hili..yani hata kupostiwa kwny page za umbea hakuna?
Kumbe hajamuoa Meena Ally
Picha zilirushwa mtandaoni, ila baadae ikasemekana ni tangazo, ndo nasikia hapa kumbe ni kweli kaoa.
 
Michango ya harusi sio lazima, huwezi kuoa kama huna hela. Binamu yangu mmoja hata miaka 30 hajafikisha, ashaoa mara tatu, harusi zote sherehe kubwa kubwa. Zile ni akili za kushikiwa na mamaake.
Basi wana pesa za kuchezea, ni imani gan gao? Islamic??
 
Back
Top Bottom