Michango kwenye harusi yangu haikuzidi 7mil. Hii ni ile iliyokuwa counted for, mingine niliipiga juu kwa juu. Hii 7mil ilichangiwa na familia zisiozidi 10. Familia moja ilichangia 2mil, wapo waliochaangia 1mil, 500k, etc. Hizi ni familia ambazo nilishajitoa sana kwa hali na mali kwa issues zao bila kutegemea returns zozote.
Nilitangaza mara moja tu kwenye magroup ya primary, secondary na chuo. Sikuwahi mkumbusha mtu mchango, wale wa karibu walinitumia wenyewe bila kukumbushwa, ambao hawakutuma sikuwasumbua kwa message.
Week kabla ya harusi nilituma tena message kwenye magroup hayo kutoa offer ya kadi za bure kwa yule atayekuwa karibu. Waalikuja wachache sababu marafiki wengi wapo Dar na harusi ipo mkoani.
Gharama za harusi zilikuwa almost 6mil. Mainly chakula na vinywaji.
Mapambo 300k, cake 200k, ukumbi 300k, MC free, Camera man 200k, etc
Camera niliokodi Camera 2, moja ya Video, nyingine ya picha, nikawapa Deiwaka vijana wawili, kila mmoja akabeba ya kwake na accessories zake, shughuli ilivyoisha nikanyonya vilivyo vyangu, nikarudisha camera za watu.
Maisha ni kuchagua...Mungu anisaidie mtoto wangu aje kuwa na spirit kali zaidi yangu.