Wewe huna watu ukiona hivyo, kamati sisi tunakuwa hata 200 na kiwango cha kuanzia laki moja, na km huyo mtu mwanao sana unaweza kuchangia zaidi ya laki..!!
Ukiachana na kamati kuna zile kadi za single na doublé unaweza kupata hata watu 300.
Kamati ndio inabeba sherehe kuanzia ukumbi, mapambo, Mc, vyakula, vinywaji, usafiri, cake, mziki na hao maids ambao wanajumuishwa kwenye kamati ya burudani..!!
Bwana harusi atagharamia nguo zake na mkewe, saloon ya kumpamba bi harusi inaingizwa kwenye kamati ya mapambo..!!
Pesa za kamati zote zikishakamilika pesa inayobaki inakuwa zawadi kwa maharusi, ndio zile zawadi mnazoziona kamati inakabidhi.