Hata Mwl Nyerere ilifikia kipindi akaitwa kiongozi asiyeambilika, lakini hatujawahi kusikia viongozi waliomfuata wakimkosoa hadharani ughaibuni

Hoja safi sana ulizozisema zenye mantiki.

Kwanza kabisa, hakuna haja ya kwenda kusema mambo ya nchi nje ya nchi yako. Unafanya hivyo ili iweje? Warithi wa uongozi Marekani au Uingereza hawaendi nchi za nje na kuanza kuwasuta watangulizi wao. Kuna video kadhaa zinazosambaa mitandaoni zikimuonyesha Samia akiwa Makamu wa Rais akisifia mipango iliyokuwa ikitekelezwa wakati wa Magufuli, kama vile suala la machinga; kukataza uagizaji wa sukari kutoka nje; kusitisha bandari ya Bagamoyo; wafanyakazi hewa; wafanyakazi wasiokidhi kiwango cha elimu; wanafunzi wanaozaa; wananchi kuunganishiwa umeme kwa Sh. 27,000 tu; n.k. Ina maana kusifia huko ilikuwa ni unafiki tu kiasi kwamba baada tu ya kutwaa madaraka unarudisha wafanyakazi waliokuwa hawana elimu ya kutosha; unaamuru sukari iagizwe kutoka nje; unasema Tanesco hawawezi kuunganisha umeme kwa Sh. 27,000; n.k. Kama hizo ndiyo zilikuwa fikra zake tangu awali, ilibidi amwambie Rais, yeye akiwa mshauri wake mkuu.

Mtoa hoja umemkariri Mwalimu kwamba alikuwa 'haambiliki'. Mwalimu alikuwa anakusikiliza umridhishe kwa hoja ndipo abadilishe msimamo wake. Kwa mfano alimuondoa Profesa Justinian Rweyemamu, bingwa wa taaluma ya uchumi, kutoka Chuo Kikuu na kumfanya mshauri wake wa mambo ya uchumi. Profesa hakudumu sana katika wadhifa huo mpya kwa sababu hawakukubaliana na baadhi ya mambo aliyokuwa akimshauri Rais. Kwa kuwa Profesa aliamini anayoyafahamu na hakutaka unafiki, alimwambia wazi mwalimu kwamba anaachia ngazi; wakashikana mkono wa kwaheri na Profesa akaenda Marekani kufundisha uchumi Chuo Kikuu cha Havard. Vipi Samia alishindwa kuachia ngazi ya Umakamu wa Rais kama alikuwa hakubaliani na aliyokuwa akiyafanya Rais Magufuli? Mbaya zaidi ni kule kukosoa ukiwa nje ya nchi. Huu ni ukosefu wa uzalendo.

Baada ya kutwaa madaraka, Rais Chiluba alikuwa akiropoka mengi kumsuta mtangulizi wake Rais Kaunda wa Zambia. Alifikia hata kusema kwamba Kaunda alikuwa amejenga mahandaki chini ya Ikulu ya kuhifadhia maiti za wapinzani wake aliokuwa akiwaua. Bahati mbaya hakutoa hata mfupa mmoja wa mtu aliyeuawa. Baadaye ndipo usalama wa taifa wakamjulisha kwamba aliyokuwa akidhania ni makaburi ya wanaouawa ni tahadhari tu kwa usama wa Rais, akiwemo yeye mwenyewe. Ndipo akameza uropokaji wake.
 
Tumuache Rais Samia aseme anavyotaka na aseme popote, hivyo anatupa nafasi ya kujua yeye ni nani kwa undani! Maana tangu mwanzo alikuwa amefichama. Wananchi hatukumjua vizuri - alijificha kivulini mwa JPM, jinsi anavyoendelea kuwa huru na kujiamini, wananchi tutamuelewa. Na tuta penda au tutamchukia.
 
We wa ajabu sana....unamzungumziaje MTU aliyepigania Uhuru wetu na aliyenyima Uhuru kwa wananchi tena ngoz moja.Hapana,hapana mkuu
 
... hiki ulichoeleza hapa ndio ilikuwa sifa kuu ya Jiwe.
 
Kawaida ya marais wote waislamu tulionao tz wanapenda kusujudia wazungu "mabeberu" kama mungu wao...kwao wabeberu ni ALLAH
 

Nenda taratibu. Marekani na Ulaya viongozi wanakosoana kwenye international media kwa hoja nzito na propaganda zilizopimwa huku dunia nzima ikifuatilia. Hawahitaji kwenda nje kusemana vibaya. Na misingi ya taifa haitikisiki.

Btw, Magufuli alipokuwa akiwananga maRais wa awamu zilizotangulia hadharani kwa kulea ufisadi, habari hizo hata video clips zilikuwa zinakusanywa, zinatafsiriwa na kuchapishwa kwenye international media. Bunge letu tu linasikilizwa vizuri sana. Of course hawategemei kitu cha maana toka huko lakini wanaambulia angalau vicomedi vya kutengenezea habari nyepesi nyepesi.

Ni ujinga kufikiri kuna “private space” hapa duniani ya kufichia uozo. Kama kuaminishana kuwa Lissu alitoa siri ndipo ndege yetu ikakamatwa huko Canada. Uongozi au utendaji mbovu hauwezi kuwa siri za taifa.
 
Unapoandika utumbo huu kumbuka yafuatayo;
1. Wewe mwenyewe ni mtoto wa mwanamke

2. Angela Merkel katawala Germany zaidi ya miaka 16 na kuifanya Germany Taifa linaloongoza kiuchumi kwa Ulaya

3. UK ilikuwa mwanamama PM kuanzia 1979 hadi 1990

4. Israel ilikuwa na Golda Meir 1969-74

5. Cleopatra alikuwa mtawala wa Egypt mwaka 51-30 BC
 
Acheni yote yazungumzwe yaani mema na mabaya , huruma au dhuruma nk.
 
Angalau Nyerere alikuwa na utu…
 
Maza siyo mtanzania ni mzanzibar akimaliza muda wake atakimbia na kutuacha na shida zetu
 
Dikteta alikuwa na chuki sn
 
Naelewa sasa kwa nini emotional intelligence ni muhimu kwa viongozi wote.
 
Huwezi kulinganisha huyu wa kwetu na hao.

Kama ilivyo kwa jinsia zote, kuna exceptional cases. Ndio hao unaowataja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…