Ng'wanamalundi
JF-Expert Member
- Feb 4, 2008
- 1,203
- 1,422
Hoja safi sana ulizozisema zenye mantiki.Mbona mkuu wa nchi yetu kama anafanya ndivyo sivyo? Kuongoza nchi kumbe kazi sana. Upo nje kwenye ziara ya kikazi alafu unaeleza kwenye media kubwa kama NY times kuwa mtangulizi wako alikuwa stubborn, hii inaleta picha gani?
Hukuwa na raha wakati unafanya nae kazi pamoja kiasi cha kumchukia kwa kutofuata ushauri wako wakati wewe ulipokuwa msaidizi wake?
Ulifanya nae kazi huku ukiwa na kinyongo maana alikuwa mkaidi?
Ina maana ulikuwa unacheka nae hadharani lakini moyoni humtaki sababu ni stubborn?
Lakini mbona hata Mwl Nyerere inasemekana wazi kabisa alikuwa mkaidi juu ya kufuata ushauri wa wasaidizi wake mpaka ilifikaia hatua akaitwa baba haambiliki, hatujawahi kusikia Mzee Mwinyi au Mkapa wakimnanga huko mamtoni?
Inasemekana alishauriwa masuala mengi tu na akakaidi, mfano aliambiwa asihamishe watu kwenye miji yao kwa ajili ya vijiji vya ujamaa lakini akawahamisha. Jambo ambalo lilileta lawama kubwa. Lakini hatikusikia akipondwa huko nje. Alishauriwa asiijifanye yeye ni superpower wa Afrika lakini akakag'ag'ania kupeleka majeshi Msumbiji, Zimbabwe na Uganda ,mataokeo yake Tanzania ikakwama kiuchumi.
Tunajichafua sisi Watanzania huku wazungu wakitucheka.
Kwanza kabisa, hakuna haja ya kwenda kusema mambo ya nchi nje ya nchi yako. Unafanya hivyo ili iweje? Warithi wa uongozi Marekani au Uingereza hawaendi nchi za nje na kuanza kuwasuta watangulizi wao. Kuna video kadhaa zinazosambaa mitandaoni zikimuonyesha Samia akiwa Makamu wa Rais akisifia mipango iliyokuwa ikitekelezwa wakati wa Magufuli, kama vile suala la machinga; kukataza uagizaji wa sukari kutoka nje; kusitisha bandari ya Bagamoyo; wafanyakazi hewa; wafanyakazi wasiokidhi kiwango cha elimu; wanafunzi wanaozaa; wananchi kuunganishiwa umeme kwa Sh. 27,000 tu; n.k. Ina maana kusifia huko ilikuwa ni unafiki tu kiasi kwamba baada tu ya kutwaa madaraka unarudisha wafanyakazi waliokuwa hawana elimu ya kutosha; unaamuru sukari iagizwe kutoka nje; unasema Tanesco hawawezi kuunganisha umeme kwa Sh. 27,000; n.k. Kama hizo ndiyo zilikuwa fikra zake tangu awali, ilibidi amwambie Rais, yeye akiwa mshauri wake mkuu.
Mtoa hoja umemkariri Mwalimu kwamba alikuwa 'haambiliki'. Mwalimu alikuwa anakusikiliza umridhishe kwa hoja ndipo abadilishe msimamo wake. Kwa mfano alimuondoa Profesa Justinian Rweyemamu, bingwa wa taaluma ya uchumi, kutoka Chuo Kikuu na kumfanya mshauri wake wa mambo ya uchumi. Profesa hakudumu sana katika wadhifa huo mpya kwa sababu hawakukubaliana na baadhi ya mambo aliyokuwa akimshauri Rais. Kwa kuwa Profesa aliamini anayoyafahamu na hakutaka unafiki, alimwambia wazi mwalimu kwamba anaachia ngazi; wakashikana mkono wa kwaheri na Profesa akaenda Marekani kufundisha uchumi Chuo Kikuu cha Havard. Vipi Samia alishindwa kuachia ngazi ya Umakamu wa Rais kama alikuwa hakubaliani na aliyokuwa akiyafanya Rais Magufuli? Mbaya zaidi ni kule kukosoa ukiwa nje ya nchi. Huu ni ukosefu wa uzalendo.
Baada ya kutwaa madaraka, Rais Chiluba alikuwa akiropoka mengi kumsuta mtangulizi wake Rais Kaunda wa Zambia. Alifikia hata kusema kwamba Kaunda alikuwa amejenga mahandaki chini ya Ikulu ya kuhifadhia maiti za wapinzani wake aliokuwa akiwaua. Bahati mbaya hakutoa hata mfupa mmoja wa mtu aliyeuawa. Baadaye ndipo usalama wa taifa wakamjulisha kwamba aliyokuwa akidhania ni makaburi ya wanaouawa ni tahadhari tu kwa usama wa Rais, akiwemo yeye mwenyewe. Ndipo akameza uropokaji wake.