Tatizo nyie ni watu wenye upeo wa kuangalia umbali wa vidole vya miguuni mwenu tu, au/na ni watu ambao hamjui kumu-interpret mtu.
Huyo Magufuli alikuwa wa namna hiyo ya kuwananga watangulizi wake, zile kauli za serikali yangu, serikali ya Magufuli, Mimi ndio jiwe, Mimi jembe na maneno mengine kama haya ni ishara ya kuwakosoa waliomtangulia.
Kama utakuwa na kumbukumbu hayati Mkapa aliwahi kumkemia kwa sababu hiyo, alimwambia kuwa wewe ni rahisi kwa ticket ya chama, chama kilikupendekeza ugombee haukugombea kama mgombea binafsi, serikali yako ni serikali ya wananchi na kwakuwa nchi hii ni ya vyama vingi ni serikali ya CCM.
Kwanini Dr. Magufu hakwenda kuwakosoa watangulizi wake Ulaya? Sababu kubwa aliogopa kwenda Ulaya na kwingeneko kwa kuwa kuongea kiingereza kwake ilikuwa ni shida mno, na kwa vile mwenyewe alijifahamu kuwa hata akiandikiwa mara nyingi alikuwa hasomi sana yaliondikwa. Lazima shida ingepatikana kwenye kuchomekea ambayo alitamani kuchomekea.