HATARI: Zama za Wakatoliki kuendelea kutubu mbele ya Padri zimepitwa na wakati

HATARI: Zama za Wakatoliki kuendelea kutubu mbele ya Padri zimepitwa na wakati

Kwahyo Mungu anahitaji msimamizi hapo katikati ili asamehe? (padri).

Yani nataka kujua kabisa core function ya padri hapo maana umesema hasamehi
Haya mambo magumu sana mkuu 😆 😆 😆

Mtu anaweza kusema OK, tumu-exclude huyo padre na ushiriki wake wote, twende kwenye logic.

Kwann unaabudu na kutubu dhambi kwa Mungu ambaye hujawahi kumwona wala aliyekurithisha hajawahi kumwona? Ulimwaminije bila clear proof?
 
Haya mambo magumu sana mkuu 😆 😆 😆

Mtu anaweza kusema OK, tumu-exclude huyo padre na ushiriki wake wote, twende kwenye logic.

Kwann unaabudu na kutubu dhambi kwa Mungu ambaye hujawahi kumwona wala hakuna aliyekurithisha hajawahi kumwona? Ulimwaminije bila clear proof?
Mkuu definition ya imani.
Ni kuwa na uhakika wa jambo bila kuwa na ushahidi.
 
Matahira hayo achana nayo
Sasa atheist akikuita taahira kwa kumuabudu Mungu ambaye hujawahi kumwona na maandiko yenu yanasema hakuna atakayemwona mpaka afe utakataa?

Mambo ya IMANI yanahitaji uvumilivu na kuchukuliana.
 
Mkuu definition ya imani.
Ni kuwa na uhakika wa jambo bila kuwa na ushahidi.
Na ukumbuke yeye uliyemuuliza atakwambia ni swala la kiimani, na hivyo hawezi kukupa jibu, na wewe hutoweza kumpa jibu. Mtabaki tu kwenye never ending arguments.

Ukimweka atheist, Muslim, na Christian kwenye hoja man to man, down the line wataishia kupigana ngumi kama hawana uvumilivu.

Kwenye imani logic ni out of context.

Ndo maana now days ma-atheist ni wengi sana.
 
Ndugu yangu umeelewa mada?
Mada ni kama kuna mantiki ya kuendelea na utaratibu wa mkatoliki kutubu mbele ya Padri wakati mapadri wengi wana sifa mbaya, wasiotunza siri nk
Mada nimeipata nimeandika kwa wale ambao wameongelea mengine nje ya mada hii
Binafsi kutubu mbele ya padri mwisho ilikuwa kwenye sakramenti ya kipaimara sijawahi rudia mpaka kesho
 
Wewe nishakuelewa mkuu nyinyi ndio wale wale mnaojifanya mnalipamba kanisa mkiwa nje ila mkiingia ndani mnalichafua tena mnalichafua vibaya, sikuandika kupata chochote hata bando nililojiunga nimenunua kwa pesa yangu sijakuomba hata senti moja na kingine sijajiunga JF kwa sababu ya kupata likes pale ninapoandika jambo, maelezo yako yanaonyesha ni jinsi gan ulivyo narrow minded, uwe na mipaka katika kile unachokiandika alafu unazidi kuwaaibisha na wengine kwa kujionyesha jinsi mlivyo, mnapenda
sana kuonekanaa nyinyi ndio wakweli zaidi ila wengine ni waongo, that's bad biblia haifundishi hivyo labda hio kampuni yenu ndio inayowafundisha hivyo
Obviously ume-panic!!!

Hii ni mara ya tatu kama siyo ya pili kuni-quote kwa post hii hii moja Ila unisamehe mimi kwa kukupa wakati mgumu kupita uwezo wako,kingine unajieleza sana mzee hii siyo dalili nzuri humu kwenye post yako umezungumza habari za vocha sijui hujajiunga JF mara hujaniomba hata cent blah blah blahs humu sote tupo kuelimishana na kueleweshana vizuri tukiwa tunaandika ukweli maana maandishi tunayoandika hapa yatabaki vizazi na vizazi.

NB;Humo kwenye bold,hata mimi nilikuwa na uwezo wa kuandika hivyo hivyo lakini nimekusamehe tunatofautiana uelewa may be challenges kwako unazichukulia ni matusi???sijui!
 
Umungu wa kujifanya watakatifu nina uhakika watakuwa mfano shetani atakuwa anaamrisha majeshi yake

Mgeuze tumchome na tackle
 
Kaka Glenn,

Swala la imani ni swala pana sana.

Mfano. Wayahudi bado wanaamini katika torati, na hawakubali hata kidogo kwamba YESU alishakuja.

Ila wanaamini YESU atakuja.

Kwa msingi huo, hawaamini kabisa agano jipya, katakata.

Na ukumbuke huko ndo chimbuko la imani.
Wayahudi hawaamini yesu atakuja,wanamchukulia Kama mvurugaji,mtoto wa zinaa,wao wanamsubiri masihi wao
 
Anayesamehe dhambi ni Mungu kazi ya Padre ni kuwa shahidi na kusimama kama muongozaji tu that's why ukishamaliza anakwambia nenda kasali sala moja mbili tatu the rest yanabaki kwa Mungu mwenyewe.
Si huwa anakujibu pale umesamehewa..so kawasiliana na mungu au yeye ndiyo kasamehe
 
Haya mambo magumu sana mkuu 😆 😆 😆

Mtu anaweza kusema OK, tumu-exclude huyo padre na ushiriki wake wote, twende kwenye logic.

Kwann unaabudu na kutubu dhambi kwa Mungu ambaye hujawahi kumwona wala hakuna aliyekurithisha hajawahi kumwona? Ulimwaminije bila clear proof?
Clear proof ni nini!?
 
Wakatoliki unaweza ukawaponda weweeeee tukabaki tunakuangalia

Hatunaga shida na mtu.

Siwezi nikajiita mlokole halafu baadaye nakunywa pombe kwa kujificha.

Tumsifu Yesu Kristo
Milele Amina.

Msingi na wazo la mtoa hoja ni mtu aliyetazamia upande hasi,kuungama kwa padre Wakatoliki wenyewe hawana shida na shida iko kwa mkatoliki labda ambaye hajaelewa vizuri katekisimu yake ila kwa anayeelewa kuwa kitubio ni nini na kwanini hawezi patwa na ukakasi huo labda hilo ni maoni yake huyo na mawazo yake na jua ya kutenda yaliyo maovu sio Katoliki tu Sema jamii imekuwa ikiwa na mtazamo ambao hauna malengo yakukomesha ulawiti ama unyanyasaji wa watoto unaotoka kwa viongozi wa imani,ikitokea padre kulawiti basi imani nyingine wanafuraha nalo na ikijatokea mlokole kafanya baya basi na imani na madhehebu mengine watafurahi hilo na hivyo ni mwendelezo kwa kila imani.
 
mara hujaniomba hata cent blah blah blahs humu sote tupo kuelimishana na kueleweshana vizuri tukiwa tunaandika ukweli maana maandishi tunayoandika hapa yatabaki vizazi na vizazi.
Acha kujifanya kwamba wewe ndio unaejua sana unazidi kujipaka kinyesi unajichafua mwenyewe, narudia tena nyinyi mnaojifanya mnalipamba kanisa mkiwa nje nyinyi nyinyi ndio wa kwanza kulichafua kanisa mnapokua ndani tena mnalichafua vibaya, ndani ya kanisa kuna machafu mengi yanafanyika ila wapo wanaofunika na kuacha maisha mengine yaendelee ila kila mtu akiamua kusema yatasemwa mengi

Na hakuna nilipopanic ila wewe unajiona na unajifanya kana kwamba kila kitu unakijua yaan unachukulia km wengine hakuna wanachokijua mazwazwa tu, unakosea mkuu tena unakosea pakubwa
 
Mada nimeipata nimeandika kwa wale ambao wameongelea mengine nje ya mada hii
Binafsi kutubu mbele ya padri mwisho ilikuwa kwenye sakramenti ya kipaimara sijawahi rudia mpaka kesho
Bado ukipeleka hoja yako kwenye context pana lina-fit.

Imani haiambatani na Logic hata kidogo. And this is fact.

Ukiweka logic kwenye imani utakuwa atheist in seconds.

Kanisa katoliki au waislamu wanaamini katika misingi yao ya kiimani, na katika kanisa katoliki as far as I know wanaamini katika kuungama kwa dhambi. Hii ni sehemu ya imani yao.

A point of contention ni padre, ok, tumweke huyo padre ambaye anashiriki kwenye hiyo process ya kitubio out of the equation, na tu-deal na Mungu mwenyewe.

Atheist atakuja na kuuliza, inakuwaje kama muumini unaomba uondolewe dhambi na Mungu ambaye hata sura yake huijui, na hajawahi onekana na binadamu yoyote, na hakuna anayeweza kuthibitisha kuwa yupo? From a logical point of view atakuwa very correct, lakini ukienda kwenye hoja ya kiimani anaweza asiwe sahihi sana.

Watu wote wanaoamini katika Mungu kama wakatoliki watatetea uwepo wa Mungu kama swala la kiimani, na wakishasema ni swala la kiimani huwezi pata a logical answer, Never.

With regard to this question, wakatoliki watasema kuungama kupitia padre ni swala la imani yao, na wakiingia katika imani, manake hakuna logical answer.
 
Kitabu kila mwaka linakuja tolea jipya kama vitabu vya TIE halafu mnasema kimetoka kwa bwana kazi kweli kweli
 
Wayahudi hawaamini yesu atakuja,wanamchukulia Kama mvurugaji,mtoto wa zinaa,wao wanamsubiri masihi wao
Ndo maana nikasema haya mambo watu wanabishania wakidhani ni maraisi sana, lakini ni mapana na mazito sana.
 
Samahani kwa ntakayoyasema hapa hii inanihusu na nasema ukweli

Nakumbuka kuna kipindi nilikua napenda sana masuala ya upadre hususani ubraza na yale maisha ya utawa vile mapadri wanavyoishi yaan nilikua napenda sana ilinivutia kuona wale mabraza jinsi wanavyovaa na kupendeza zile nguo zao za kimisionari

Basi nikaenda kuomba kuanza kujifunza kusimamia kanisani pale mbele, enzi hizo nakumbuka nilikua mdogo sana nilikua km na miaka 7/8 hivi nilimwambia mzee mimi napenda sana kuhudumia kanisani mzee akakubari ila kipindi hicho mzee alikua busy sana kukaa nae mezani ilikua imezidi sana dakika 5 yeye ni mtu wa kazi na kazi na yeye muda wa kukaa na sisi labda wiki end

Basi nikapeleka barua kwenye jumuiya kutoka kanisani ikaenda ikasainiwa na mwenyekiti safi nikarudisha kanisani nikaanza mafundisho ya kutumikia, I am telling you niliweza kuhudhulia wiki moja tu narudia tena nilihudhulia mafunzo ya kutumikia wiki moja tu baada ya hapo nilikaa pembeni mwenyewe yaani niliacha mwenyewe bila kulazimishwa na mtu

Mzee aliponiona sihudhurii tena yale mafundisho akaanza kunihoji vipi mboni hauendi tena kujifunza kutumikia kanisani, umeacha? Nikamwambia mzee nimegairisha sitaki tena kusikia habari za kutumikia kanisani, kuanzia hapo nikaanza kuchukia zile habari za kutumikia na wale mabraza pamoja na wale wanaotumikia kanisani nikawa siwakubari tena km jinsi nilivyokua nawakubari pale mwanzo kabla sijajiunga na mafundisho ya kutumikia kanisani

Niliona nini? Hio ni Siri yangu..
Kuna kitu ulipitishiwa ukaona hata sintoweza kulimudu acha nitulie umefanya vyema mno
 
Clear proof ni nini!?

(Entry 1 of 3) 1a : the cogency of evidence that compels acceptance by the mind of a truth or a fact. b : the process or an instance of establishing the validity of a statement especially by derivation from other statements in accordance with principles of reasoning. 2 obsolete : experience
 
Kwa sasa Kesi za uchafu wa mapadri ni nyingi mnoo na ziko dunia nzima. Tuseme ukweli tu, mapadri wengi wa kizazi hiki hawajatulia. Kuna wazinzi, walevi, wafiraji, wabakaji, mafisadi mpaka wauaji. Kwangu mimi hilo sio la ajabu kwa sababu, mapadri ni watu sawa sawa na watu wengine, ni waumini kama maumini wengi, hivyo uchafu unaofanywa na watu wengine au waumini wengine unaweza kufanywa vile vile na Padri kwa kiwango kile kile au zaidi. Tatizo liko pale ambapo muumini anapolazimika kutubu dhambi zake mbele ya Padri ambaye naye ni mchafu. Hii unaiona ni sahihi?
Kama wewe ni mkatoliki na unauliza hilo swali basi nadhani unatakiwa kurudi mafundisho uanze kusoma katekismo. Hatutubu kwa padre Bali kwa Mungu na padre pale yupo kama shahidi na anatoa maelekezo ya malipizi kama alivyoambiwa mtume Petro kwamba atakalolifunga duniani na mbinguni limefungwa na atakalolifungua duniani mbinguni limefunguliwa.Umuhimu wa Padre unabaki palepale.Uchafu au skendo za baadhi yao hauondoi uhalali na umuhimu wao katika kutoa sakrament ya upatanisho. Kama ni hivyo basi hata kwenye kufungisha ndoa wasiwepo! Maana ni baina yenu wawili, au kwenye maazishi au shughuli zingine za kiroho.
 
Back
Top Bottom