HATARI: Zama za Wakatoliki kuendelea kutubu mbele ya Padri zimepitwa na wakati

HATARI: Zama za Wakatoliki kuendelea kutubu mbele ya Padri zimepitwa na wakati

Niliona nini? Hio ni Siri yangu..

Mpaka hapa chochote utakachokiandika ukiwa umebanwa na watu utakuwa umejitungia ilibidi useme straight uliona nini na nini toka mwanzo na hapa sote hatujulikani tunatumia fake IDs ni nani angekujua?
Huyu amekuja kuichafua dini na kanisa la roman Catholic
 
Hata hivyo utaratibu huo haukuwepo Kibiblia! Utaratibu huo ulifanywa ili kukamata waharifu wakati wa Utawala wa Kirumi! Pili ni utaratibu wa kumfanya mwenye dhambi afichiwe dhambi
Samahani kwa ntakayoyasema hapa hii inanihusu na nasema ukweli

Nakumbuka kuna kipindi nilikua napenda sana masuala ya upadre hususani ubraza na yale maisha ya utawa vile mapadri wanavyoishi yaan nilikua napenda sana ilinivutia kuona wale mabraza jinsi wanavyovaa na kupendeza zile nguo zao za kimisionari

Basi nikaenda kuomba kuanza kujifunza kusimamia kanisani pale mbele, enzi hizo nakumbuka nilikua mdogo sana nilikua km na miaka 7/8 hivi nilimwambia mzee mimi napenda sana kuhudumia kanisani mzee akakubari ila kipindi hicho mzee alikua busy sana kukaa nae mezani ilikua imezidi sana dakika 5 yeye ni mtu wa kazi na kazi na yeye muda wa kukaa na sisi labda wiki end

Basi nikapeleka barua kwenye jumuiya kutoka kanisani ikaenda ikasainiwa na mwenyekiti safi nikarudisha kanisani nikaanza mafundisho ya kutumikia, I am telling you niliweza kuhudhulia wiki moja tu narudia tena nilihudhulia mafunzo ya kutumikia wiki moja tu baada ya hapo nilikaa pembeni mwenyewe yaani niliacha mwenyewe bila kulazimishwa na mtu

Mzee aliponiona sihudhurii tena yale mafundisho akaanza kunihoji vipi mboni hauendi tena kujifunza kutumikia kanisani, umeacha? Nikamwambia mzee nimegairisha sitaki tena kusikia habari za kutumikia kanisani, kuanzia hapo nikaanza kuchukia zile habari za kutumikia na wale mabraza pamoja na wale wanaotumikia kanisani nikawa siwakubari tena km jinsi nilivyokua nawakubari pale mwanzo kabla sijajiunga na mafundisho ya kutumikia kanisani

Niliona nini? Hio ni Siri yangu..
Aise hongera kwa kutoka kwenye tundu la Simba!
 
Sasa kama Padri ndio shahidi wakati natubu dhambi zangu kwa Mungu, je katika zama hizi za mapadri kujulikana wazi wachafu kitabia, nini mantiki yake yeye kuwa shahidi wa kutubu dhambi zangu?

Utakubaliana na mimi hapo zamani mapadri walionekana kama watu wema, wasafi kitabia na watu wenye uchaji wa Mungu
, hivyo muumini alipokuwa akitubu mbele ya Padri hakuwa na wasi wasi wowote kuhusu toba, maana anaye mshuhudia (Padri) ni mtu msafi. Katika zama hizi, huoni hilo la kutubu mbele ya Padri halina mantiki au kupitwa na wakati?
Kwanza tunakosea kusema mapadre,wangapi wamethibitika kufanya huu ujinga huu kwa mwaka huu?zipo sheria za Kanisa kudili na hao wenye mapungufu na zaidi zipo sheria zilizotungwa na viongozi wa serikali tunaoamini wamewekwa na Mungu hivyo ikithibitika padre amevunja moja wapo wa nguzo za Kanisa au jamii haraka sana anasimamishwa kufanya chochote kinachohusu Kanisa(refer tukio la Moshi) na waumini wanajua hivyo.

Hakuna wakati ambao binadamu ameweza kuuthibitisha wema wa binadamu mwenzake hata zamani walikuwa vivyo hivyo nafsi ya mtu kama ni chafu itakuwa hivyo muda ukifika so kwa wakati wao waliokuwepo waliona madhaifu haya,bado nafsi ya mtu inabaki kuwa nafsi ya mtu muhimu ni mimi kama muumini kutojihusisha na kuhukumu kitu ambacho sijaona akikifanya unless iwe hadharani kama hivi kwamba imethibitika kwa mamlaka zote za Kanisa na serikali kwamba ametenda uovu.

Mambo ya kiimani hayana ”wakati huu au wakati ule”Zama za mababu wa imani walikuwepo watu waliojulikana ni watenda maovu refer Yonah kupewa kazi na Mungu na kukataa katakata Daud kuwa mfalme na kuonekana maovu yake ktk ya ufalme wake kiasi cha kufikia kudhulumu maisha ya askari wake mtiifu kisa kumtamani mkewe lakini bado Mungu aliwatumia so ni kusema bado wapo mapadre hata kama wataanguka ktk maovu (mara nyingi kwa siri maana mpaka kuyajua haya ni Mungu tu aamue kuujulisha umma maovu yake) bado Mungu atawatumia kadiri itakavyompendeza.
 
Acha kujifanya kwamba wewe ndio unaejua sana unazidi kujipaka kinyesi unajichafua mwenyewe, narudia tena nyinyi mnaojifanya mnalipamba kanisa mkiwa nje nyinyi nyinyi ndio wa kwanza kulichafua kanisa mnapokua ndani tena mnalichafua vibaya, ndani ya kanisa kuna machafu mengi yanafanyika ila wapo wanaofunika na kuacha maisha mengine yaendelee ila kila mtu akiamua kusema yatasemwa mengi

Na hakuna nilipopanic ila wewe unajiona na unajifanya kana kwamba kila kitu unakijua yaan unachukulia km wengine hakuna wanachokijua mazwazwa tu, unakosea mkuu tena unakosea pakubwa
Ngoja basi kwanza aisee we jamaa m'bishi!!!

Au ndugu yangu we Muha?🤣
 
(Entry 1 of 3) 1a : the cogency of evidence that compels acceptance by the mind of a truth or a fact. b : the process or an instance of establishing the validity of a statement especially by derivation from other statements in accordance with principles of reasoning. 2 obsolete : experience
Umbile lako linatosha kuwa clear proof
 
Ndo maana nikasema haya mambo watu wanabishania wakidhani ni maraisi sana, lakini ni mapana na mazito sana.
Ulimtaja yesu na wayahudi..wayahudi hawatambui chochote kuhusu yesu,ndiyo maana walihakikisha anatundikwa msalabani
 
Si huwa anakujibu pale umesamehewa..so kawasiliana na mungu au yeye ndiyo kasamehe
Husema “umesamehewa dhambi zako " hii inasimama kumaanisha kwamba kupitia yeye (wakati huo huinua mkono kama kukubariki) Mungu amenena na wewe muumini na amepokea toba yako na Padre hukwambia nenda kasali sala fulani ili kujitakasa,haya ni mambo ya kiimani sheikh watu tunajua na tunazingatia.

Kama wewe pale imam anaposema "Tumswalie Mtume" kwani anakuwa amewasiliana na Mungu kwamba Mungu ajiandae kupokea sala za waumini fulani muda huu wanataka kumswalia mtume?
 
Bado ukipeleka hoja yako kwenye context pana lina-fit.

Imani haiambatani na Logic hata kidogo. And this is fact.

Ukiweka logic kwenye imani utakuwa atheist in seconds.

Kanisa katoliki au waislamu wanaamini katika misingi yao ya kiimani, na katika kanisa katoliki as far as I know wanaamini katika kuungama kwa dhambi. Hii ni sehemu ya imani yao.

A point of contention ni padre, ok, tumweke huyo padre ambaye anashiriki kwenye hiyo process ya kitubio out of the equation, na tu-deal na Mungu mwenyewe.

Atheist atakuja na kuuliza, inakuwaje kama muumini unaomba uondolewe dhambi na Mungu ambaye hata sura yake huijui, na hajawahi onekana na binadamu yoyote, na hakuna anayeweza kuthibitisha kuwa yupo? From a logical point of view atakuwa very correct, lakini ukienda kwenye hoja ya kiimani anaweza asiwe sahihi sana.

Watu wote wanaoamini katika Mungu kama wakatoliki watatetea uwepo wa Mungu kama swala la kiimani, na wakishasema ni swala la kiimani huwezi pata a logical answer, Never.

With regard to this question, wakatoliki watasema kuungama kupitia padre ni swala la imani yao, na wakiingia katika imani, manake hakuna logical answer.
Haya mambo ukifikiria sana kichwa kinaweza pasuka
Binafsi nimesoma shule zinazoongozwa na katoliki wenyewe wanakuambia kabisa hizi imani zipo kila mtu na yake ila binadamu wote ni wamoja na tusiache hizi dini zitutenganishe
 
Martin Luther aliona mengi mpaka akaamua kutoka huko katoliki
 
Haya mambo ukifikiria sana kichwa kinaweza pasuka
Binafsi nimesoma shule zinazoongozwa na katoliki wenyewe wanakuambia kabisa hizi imani zipo kila mtu na yake ila binadamu wote ni wamoja na tusiache hizi dini zitutenganishe
Wakatoliki to a greater extent wanaweza kwa sababu ni very practicle.

Changamoto kubwa ya Romans kutoka makanisa mengine ni kuamini kwao kwamba IMANI lazima iendane na KAZI, "SALA na KAZI".

Huu mwenendo wao unawafanya waonekane na wengine kama watu wasiokuwa na imani.

Wengine wanaamini katika miujiza, lakini wakatoliki wanafundishwa usipofanya KAZI utalala njaa. Kilochowasaidia ROMANS ni ELIMU.

Hata ukiwasikia mashekhe wanawasifia kwenye hilo.
 
Nakuwa na uhakika kabisa nimesamehewa dhambi zangu nilizoungama, ndio maana natamka kwa kujiamini kabisa niliungama nikatimiza malipizi, na hamna sentensi inayonifariji kama, kwa mamlaka niliyopewa nami nakuondolea dhambi zako kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu
 
Naomba kueleweshwa inamaana unapoenda kumwambia zambi zako padre huwa unataka yeye ndio akuombee kwa mumbu usamehewe au yeye ndio anasamehe hayo maovu uliyofanya.???? Na je haya ni mafundisho kutoka kwa nani???
 
Tafuta pesa acha kuingilia imani za watu hakuna hata mmoja mwenye uhakika dini ipi sahihi.Hata wao ni binadamu wana mapungufu yao
 
Hata kwa sisi upande wa waislam tumepiteza imani kwa Masheikh na viongozi wetu wa dini.. Asilimia kubwa ni washenz na wanaongoza kwa ushenzi na wanaficha maovu yao kwenye dini.. Kila siku unasikia cases za walimu wa madrasa kuwalawiti wanafunzi wao haijalishi jinsia
 
Tatizo kubwa Sana..
Usimuabudu binadam
Binadam hatuaminiki na sio wakamilifu na watakatifu, kwanini ukamtubie mtu et akuombee.. Nonsense kabisa.

Dini uchafu umezidi Sana tulio na neema ya kujua Mungu anataka Nini huwezi kusumbuka na Dini..

Hi yote inatokana na ujinga na umasikini lazima utakuwa mtumwa wa dini.

Ukiamini huko utapata baraka, miujiza, kwenda mbinguni( wakati unafanya mabaya hiyo mbingu gani) kupona magonjwa( mengine Ni sababu ya afya na lishe duni, kazi ngumu n.k badala ya kwenda hospital unaenda kanisani ukiona bado unaenda kwa waganga au unakuwa unafanya vyote kwa pamoja yaani unafiki).

Viongozi wa dini nao ni tatizo kuwakalisha waumini muda wote kanisani ili wapate pesa, uzinzi, hawafundishi watu kuishi maisha mema na kutenda wema kwa wengine. Wanacho waza ni vipi michango itolewe n.k

Watanzania ujinga na umasikini unatupeleka pabaya Sana.

kwani kutubu ni kumuabudu binadamu tena[emoji23][emoji1787][emoji23][emoji23]....ukiwa na philosophy, psychology, bible knowledge, na vingine itakusaidia sana kujudge hivi vitu..ila kama una engineering itakupa shida
 
Husema “umesamehewa dhambi zako " hii inasimama kumaanisha kwamba kupitia yeye (wakati huo huinua mkono kama kukubariki) Mungu amenena na wewe muumini na amepokea toba yako na Padre hukwambia nenda kasali sala fulani ili kujitakasa,haya ni mambo ya kiimani sheikh watu tunajua na tunazingatia.

Kama wewe pale imam anaposema "Tumswalie Mtume" kwani anakuwa amewasiliana na Mungu kwamba Mungu ajiandae kupokea sala za waumini fulani muda huu wanataka kumswalia mtume?
Maelezo yako ni illogical..hayana mantiki,na mfano wa kumswalia mtume ndiyo umedhihirisha upopoma...umeshasamehewa naye hawasiliani na mungu Kama wote tulivyo na hakika,maana yake yeye ndiye anayesamehe dhambi
 
Najuta sana kwa kupiga magoti na kuungama mbele ya binadamu mwenzangu. Ni enzi za utoto bila kujua dini ni nini. Ni mbinu tu za hao Wayahudi kuteka mawazo ya watu kisaikologia. Mf. Ukipanga mbinu za kupindua serikali na baadae ukaacha na kuungama, si jamaa atapeleka jina lako Ikulu? Kulikuwa na adhabu ya kutumbukiza pesa Fulani ili usamehewe!!

[emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji1787] kwa haya mawazo yako sizani kama huo utoto ulishatoka...
 
Back
Top Bottom