HATARI: Zama za Wakatoliki kuendelea kutubu mbele ya Padri zimepitwa na wakati

HATARI: Zama za Wakatoliki kuendelea kutubu mbele ya Padri zimepitwa na wakati

Ukimuambia Padre.. Yeye kwa Mamlaka aliyo nayo.. Anakuondolea hiyo dhambi.. Papo hapo na anakupa "adhabu" kwa jina la malipizi ili iondoke kabisa.

JE, UNAJUA SAKRAMENTI MBILI ZA UPONYAJI KATIKA KANISA KATOLIKI?

Licha ya neema isiyo na kikomo iliyopewa kupitia uhusiano wetu wa kibinafsi na Utatu katika Sakramenti za Kuanzishwa, tunaendelea kutenda dhambi na bado tunakutana na magonjwa na kifo. Kwa sababu hii, Mungu anakuja kwetu na uponyaji katika njia mbili za ziada na za kipekee.

KITUBIO:
sakramenti ya kukiri, toba na upatanisho hutupatia kukutana kipekee na Mungu katika dhambi yetu. Mungu anatupenda sana hata amekuja kutupatanisha na sisi. Na alifanya hivyo akijua kabisa kuwa sisi ni wenye dhambi wanaohitaji msamaha na rehema.

Kukiri ni fursa ya kukutana kwa kweli na kibinafsi na Mungu katikati ya dhambi. Ni njia ya Mungu kutuambia kuwa yeye mwenyewe anataka kutuambia kuwa anatusamehe. Tunapokiri dhambi zetu na kupokea kufutwa, tunapaswa kuona kwamba hii ni kitendo cha Mungu ambaye anakuja kwetu, anasikiliza dhambi zetu, akazifuta na kisha kutuambia tuende na tusifanye dhambi tena.

Kwa hivyo unapoenda kukiri, hakikisha unaiona kama mkutano wa kibinafsi na Mungu wetu mwenye rehema. Hakikisha kumsikia akiongea na wewe na kujua kuwa ni Mungu anayeingia ndani ya roho yako kwa kufuta dhambi zako zote.

MPAKO WA WAGONJWA:
Mungu huwajali na kuwajali wanyonge, wagonjwa, wanaoteseka na wanaokufa. Hatuko peke yetu katika wakati huu. Katika sakramenti hii, lazima tujitahidi kuona Mungu huyu wa kibinafsi akija kwetu kwa huruma kututunza. Lazima tumsikie akisema yuko karibu. Lazima tumruhusu abadilishe mateso yetu, alete uponyaji anayotaka (haswa uponyaji wa kiroho) na, wakati wetu utakapokuja, tumruhusu atayarishe roho yetu kikamilifu kukutana naye mbinguni.

Ikiwa unajikuta unahitaji sakramenti hii, hakikisha unaiona kama Mungu huyu wa kibinafsi ambaye anakuja kwako wakati wa hitaji la kukupa nguvu, rehema na huruma. Yesu anajua mateso na kifo ni nini. Aliishi nao. Na anataka kuwa huko kwa ajili yako wakati huu.

“Yesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, ‘Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako’... ‘Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi’ - amwambia yule mwenye kupooza - ‘Ondoka, ujitwike kitanda chako, uende nyumbani kwako’. Akaondoka, akaenda zake nyumbani kwake. Makutano walipomwona, walishikwa na hofu, wakamtukuza Mungu, aliyewapa watu amri ya namna hii” (Injili ya Mathayo 9:2,6-8).

Credit :#RmSautiYaFaraja
Nilikiwa sijui hili...Kumbe Padri anayo pawa ya kusamehe dhambi?
Au kwakuwa Yesu alisamehe basi padri nayeye ana status ya Yesu?
 
Kwani ulikuwa unapata faida gani kuandika ambayo huyajui just kupata likes kutoka kwa watu ambao wala wasingekusaidia japo hata chupa ya maji???
Wewe nishakuelewa mkuu nyinyi ndio wale wale mnaojifanya mnalipamba kanisa mkiwa nje ila mkiingia ndani mnalichafua tena mnalichafua vibaya, sikuandika kupata chochote hata bando nililojiunga nimenunua kwa pesa yangu sijakuomba hata senti moja na kingine sijajiunga JF kwa sababu ya kupata likes pale ninapoandika jambo, maelezo yako yanaonyesha ni jinsi gan ulivyo narrow minded, uwe na mipaka katika kile unachokiandika alafu unazidi kuwaaibisha na wengine kwa kujionyesha jinsi mlivyo, mnapenda
sana kuonekanaa nyinyi ndio wakweli zaidi ila wengine ni waongo, that's bad biblia haifundishi hivyo labda hio kampuni yenu ndio inayowafundisha hivyo
 
Sawa, kwahyo anayesamehe dhambi ni Mungu au padri?
Anayesamehe dhambi ni Mungu kazi ya Padre ni kuwa shahidi na kusimama kama muongozaji tu that's why ukishamaliza anakwambia nenda kasali sala moja mbili tatu the rest yanabaki kwa Mungu mwenyewe.
 
Nini kilikufanya kuacha kuungama mbele ya Padri?
Kama kweli ni Mkatoliki ipo siku atafanya hivyo tu,hata mimi ni muda sijaungama ila najua napaswa kufanya hivyo na kuna siku nitafanya Mungu akipenda hata nikiwa ktk mazingira ya hatari
 
Hakuna binadamu asiyekuwa na dhambi na kila taasisi imejiwekea utaratibu wake jinsi ya ku-deal na hayo mambo.

Padre nae anaungama kwa padre mwenzake even Askofu akijihisi kuanguka nae anafanya vivyo hivyo hata Pope maana wote anytime anywhere wanawindwa.
Sasa waza haya mambo.
1. Ikiwa Padri wako ni mtenda dhambi kama wewe, unaendaje kutubu kwake? (Kwa mfano jana umegundua Padri wako kamtandika mimba binti yako na wamepanga kuitoa na wewe leo umetoka kula mzigo wa malaya fulani, sasa unataka kwenda kutubu dhambi ya uzinzi kwa Padri, unafanyaje?)

2. Leo umetenda dhambi ukiwa safarini na unajihisi kutubu, utasubiri ufike au urejee safari ndio ukatubu kwa Padri wako?
 
Kaka Glenn,

Swala la imani ni swala pana sana.

Mfano. Wayahudi bado wanaamini katika torati, na hawakubali hata kidogo kwamba YESU alishakuja.

Ila wanaamini YESU atakuja.

Kwa msingi huo, hawaamini kabisa agano jipya, katakata.

Na ukumbuke huko ndo chimbuko la imani.
Naelewa hilo mkuu
 
Anayesamehe dhambi ni Mungu kazi ya Padre ni kuwa shahidi na kusimama kama muongozaji tu that's why ukishamaliza anakwambia nenda kasali sala moja mbili tatu the rest yanabaki kwa Mungu mwenyewe.
Kwahyo Mungu anahitaji msimamizi hapo katikati ili asamehe? (padri).

Yani nataka kujua kabisa core function ya padri hapo maana umesema hasamehi
 
12yra anawekwa ulutani na kuhimili mambo ya padre? Mmh bila shaka huyo ni ibilisi ndani ya mwanadamu
Mkuu nimejiuliza sana.
Mtoto kama huyo anaingilowa yuko kimya tu?

Njiani katembea vizuri tu?

Mmmh nafikiri mtoto alishaonja mara nyingi na huenda huu sasa ulikuwa mpango wamshikishe jamaa adabu
 
Zama za kiimani kwa Kanisa Katoliki zimebadilika, maisha ya waumini na Mapadri ndani ya Kanisa Katoliki yamebadilika, na mifumo ya kimaisha imebadilika.
Vivyo hivyo kwa Uislam. Mambo ya kufundishia watoto Qaswida na Quaran kwenye Madrasa yamepitwa na wakati maana masheikh na ma-Ustaadh wanawazibua mpaka mitaro ya dawasco! Hatuna pa kukimbilia tena!
 
Kanisa katoliki limeshajiwekea misingi imara sana mbele ya jamii na njia moja wapo ni mafundisho yanayoanzia utotoni
Litakuwa na makandokando lkn waamini wengi bado watakuwa nalo tofauti na haya mengine yanayodakia watu juu kwa juu
Binafsi sijaenda kanisani na mwaka wa 3 😃 lkn kila ikifika j2 nafsi inaniambia ni siku ya ibada natakiwa niwe kanisani
 
Anayesamehe dhambi ni Mungu kazi ya Padre ni kuwa shahidi na kusimama kama muongozaji tu that's why ukishamaliza anakwambia nenda kasali sala moja mbili tatu the rest yanabaki kwa Mungu mwenyewe.
Sasa kama Padri ndio shahidi wakati natubu dhambi zangu kwa Mungu, je katika zama hizi za mapadri kujulikana wazi wachafu kitabia, nini mantiki yake yeye kuwa shahidi wa kutubu dhambi zangu?

Utakubaliana na mimi hapo zamani mapadri walionekana kama watu wema, wasafi kitabia na watu wenye uchaji wa Mungu, hivyo muumini alipokuwa akitubu mbele ya Padri hakuwa na wasi wasi wowote kuhusu toba, maana anaye mshuhudia (Padri) ni mtu msafi. Katika zama hizi, huoni hilo la kutubu mbele ya Padri halina mantiki au kupitwa na wakati?
 
Vivyo hivyo kwa Uislam. Mambo ya kufundishia watoto Qaswida na Quaran kwenye Madrasa yamepitwa na wakati maana masheikh na ma-Ustaadh wanawazibua mpaka mitaro ya dawasco! Hatuna pa kukimbilia tena!
Watoto wa kiislamu ni muhimu wafundishwe dini, madrasa ni muhimu. Jambo la kuhimizwa kwa sasa ni hili;
1. Walimu wao waangaliwe kwa karibu.
2. Watoto waonywe na kufundishwa na wazazi wao kuhusu dalili ya mienendo mibaya na mazingira hatarishi popote pale watakapokuwa.
 
Sasa waza haya mambo.
1. Ikiwa Padri wako ni mtenda dhambi kama wewe, unaendaje kutubu kwake? (Kwa mfano jana umegundua Padri wako kamtandika mimba binti yako na wamepanga kuitoa na wewe leo umetoka kula mzigo wa malaya fulani, sasa unataka kwenda kutubu dhambi ya uzinzi kwa Padri, unafanyaje?)

2. Leo umetenda dhambi ukiwa safarini na unajihisi kutubu, utasubiri ufike au urejee safari ndio ukatubu kwa Padri wako?
Maswali ya imani wala hayahitaji logic mkuu,

Down the line, mtu anaweza kukuuliza na wewe unatubuje dhambi kwa Mungu ambaye hujawahi kumwona kwa macho yako? Kwa akili ya kawaida unaweza kujiona insane.
 
Zama za kiimani kwa Kanisa Katoliki zimebadilika, maisha ya waumini na Mapadri ndani ya Kanisa Katoliki yamebadilika, na mifumo ya kimaisha imebadilika.

Sio siri tena, Kutubu mbele ya Padri kwa sasa kumekuwa sumu ya kuwaumiza waumini au kitendawili chenye kukosa majibu.

Kiapo cha Upadri kutunza siri za waumini kimepoteza mwelekeo, Mapadri wamekosa uaminifu mbele ya waumini na mbele ya jamii, imani na amani baina yao haipo tena. Muumini anazini, padri naye anazini nani wamkutubisha mwenzie.

Muumini ametoa mimba na Padri amebaka mtoto anayemfundisha komunio, nani akatubu kwa mwenzie?

Muumini anayetafuta msaada wa kuokoa ndoa yake kwa kumwambia Padri naona alivyokosea, Padri anatumia mwanya huo kuzini na mkewe

Sasa huu ndio wakati muafaka zaidi kwa kila mtu kwenda kutubu kwa Mungu wake ili kila mtu apambane na dhambi zake kwa muumba wake?
hao jamaa wa hiyo imani ukiwashauri hata uwe mkristo mwenzao,wao hasira zao wanamalizia kutukana uislamu na Waislamu,watakuambia mara wavaa kobazi, Mara vipedo,

Cha msingi Ni kuwaacha tu hao viongozi wao wa dini wawafffire watoto zao na wake zao, pumbavu,
 
Kanisa katoliki limeshajiwekea misingi imara sana mbele ya jamii na njia moja wapo ni mafundisho yanayoanzia utotoni
Litakuwa na makandokando lkn waamini wengi bado watakuwa nalo tofauti na haya mengine yanayodakia watu juu kwa juu
Binafsi sijaenda kanisani na mwaka wa 3 😃 lkn kila ikifika j2 nafsi inaniambia ni siku ya ibada natakiwa niwe kanisani
Ndugu yangu umeelewa mada?
Mada ni kama kuna mantiki ya kuendelea na utaratibu wa mkatoliki kutubu mbele ya Padri wakati mapadri wengi wana sifa mbaya, wasiotunza siri nk
 
Back
Top Bottom