Huyu amekuja kuichafua dini na kanisa la roman CatholicNiliona nini? Hio ni Siri yangu..
Mpaka hapa chochote utakachokiandika ukiwa umebanwa na watu utakuwa umejitungia ilibidi useme straight uliona nini na nini toka mwanzo na hapa sote hatujulikani tunatumia fake IDs ni nani angekujua?
Mkuu gorokko naona unatafuta shari 😆 😆 😆Kuna kitu ulipitishiwa ukaona hata sintoweza kulimudu acha nitulie umefanya vyema mno
Aise hongera kwa kutoka kwenye tundu la Simba!Samahani kwa ntakayoyasema hapa hii inanihusu na nasema ukweli
Nakumbuka kuna kipindi nilikua napenda sana masuala ya upadre hususani ubraza na yale maisha ya utawa vile mapadri wanavyoishi yaan nilikua napenda sana ilinivutia kuona wale mabraza jinsi wanavyovaa na kupendeza zile nguo zao za kimisionari
Basi nikaenda kuomba kuanza kujifunza kusimamia kanisani pale mbele, enzi hizo nakumbuka nilikua mdogo sana nilikua km na miaka 7/8 hivi nilimwambia mzee mimi napenda sana kuhudumia kanisani mzee akakubari ila kipindi hicho mzee alikua busy sana kukaa nae mezani ilikua imezidi sana dakika 5 yeye ni mtu wa kazi na kazi na yeye muda wa kukaa na sisi labda wiki end
Basi nikapeleka barua kwenye jumuiya kutoka kanisani ikaenda ikasainiwa na mwenyekiti safi nikarudisha kanisani nikaanza mafundisho ya kutumikia, I am telling you niliweza kuhudhulia wiki moja tu narudia tena nilihudhulia mafunzo ya kutumikia wiki moja tu baada ya hapo nilikaa pembeni mwenyewe yaani niliacha mwenyewe bila kulazimishwa na mtu
Mzee aliponiona sihudhurii tena yale mafundisho akaanza kunihoji vipi mboni hauendi tena kujifunza kutumikia kanisani, umeacha? Nikamwambia mzee nimegairisha sitaki tena kusikia habari za kutumikia kanisani, kuanzia hapo nikaanza kuchukia zile habari za kutumikia na wale mabraza pamoja na wale wanaotumikia kanisani nikawa siwakubari tena km jinsi nilivyokua nawakubari pale mwanzo kabla sijajiunga na mafundisho ya kutumikia kanisani
Niliona nini? Hio ni Siri yangu..
Sawa mkuu,Aise hongera kwa kutoka kwenye tundu la Simba
Kwanza tunakosea kusema mapadre,wangapi wamethibitika kufanya huu ujinga huu kwa mwaka huu?zipo sheria za Kanisa kudili na hao wenye mapungufu na zaidi zipo sheria zilizotungwa na viongozi wa serikali tunaoamini wamewekwa na Mungu hivyo ikithibitika padre amevunja moja wapo wa nguzo za Kanisa au jamii haraka sana anasimamishwa kufanya chochote kinachohusu Kanisa(refer tukio la Moshi) na waumini wanajua hivyo.Sasa kama Padri ndio shahidi wakati natubu dhambi zangu kwa Mungu, je katika zama hizi za mapadri kujulikana wazi wachafu kitabia, nini mantiki yake yeye kuwa shahidi wa kutubu dhambi zangu?
Utakubaliana na mimi hapo zamani mapadri walionekana kama watu wema, wasafi kitabia na watu wenye uchaji wa Mungu
, hivyo muumini alipokuwa akitubu mbele ya Padri hakuwa na wasi wasi wowote kuhusu toba, maana anaye mshuhudia (Padri) ni mtu msafi. Katika zama hizi, huoni hilo la kutubu mbele ya Padri halina mantiki au kupitwa na wakati?
Ngoja basi kwanza aisee we jamaa m'bishi!!!Acha kujifanya kwamba wewe ndio unaejua sana unazidi kujipaka kinyesi unajichafua mwenyewe, narudia tena nyinyi mnaojifanya mnalipamba kanisa mkiwa nje nyinyi nyinyi ndio wa kwanza kulichafua kanisa mnapokua ndani tena mnalichafua vibaya, ndani ya kanisa kuna machafu mengi yanafanyika ila wapo wanaofunika na kuacha maisha mengine yaendelee ila kila mtu akiamua kusema yatasemwa mengi
Na hakuna nilipopanic ila wewe unajiona na unajifanya kana kwamba kila kitu unakijua yaan unachukulia km wengine hakuna wanachokijua mazwazwa tu, unakosea mkuu tena unakosea pakubwa
Umbile lako linatosha kuwa clear proof(Entry 1 of 3) 1a : the cogency of evidence that compels acceptance by the mind of a truth or a fact. b : the process or an instance of establishing the validity of a statement especially by derivation from other statements in accordance with principles of reasoning. 2 obsolete : experience
Ulimtaja yesu na wayahudi..wayahudi hawatambui chochote kuhusu yesu,ndiyo maana walihakikisha anatundikwa msalabaniNdo maana nikasema haya mambo watu wanabishania wakidhani ni maraisi sana, lakini ni mapana na mazito sana.
Husema “umesamehewa dhambi zako " hii inasimama kumaanisha kwamba kupitia yeye (wakati huo huinua mkono kama kukubariki) Mungu amenena na wewe muumini na amepokea toba yako na Padre hukwambia nenda kasali sala fulani ili kujitakasa,haya ni mambo ya kiimani sheikh watu tunajua na tunazingatia.Si huwa anakujibu pale umesamehewa..so kawasiliana na mungu au yeye ndiyo kasamehe
Haya mambo ukifikiria sana kichwa kinaweza pasukaBado ukipeleka hoja yako kwenye context pana lina-fit.
Imani haiambatani na Logic hata kidogo. And this is fact.
Ukiweka logic kwenye imani utakuwa atheist in seconds.
Kanisa katoliki au waislamu wanaamini katika misingi yao ya kiimani, na katika kanisa katoliki as far as I know wanaamini katika kuungama kwa dhambi. Hii ni sehemu ya imani yao.
A point of contention ni padre, ok, tumweke huyo padre ambaye anashiriki kwenye hiyo process ya kitubio out of the equation, na tu-deal na Mungu mwenyewe.
Atheist atakuja na kuuliza, inakuwaje kama muumini unaomba uondolewe dhambi na Mungu ambaye hata sura yake huijui, na hajawahi onekana na binadamu yoyote, na hakuna anayeweza kuthibitisha kuwa yupo? From a logical point of view atakuwa very correct, lakini ukienda kwenye hoja ya kiimani anaweza asiwe sahihi sana.
Watu wote wanaoamini katika Mungu kama wakatoliki watatetea uwepo wa Mungu kama swala la kiimani, na wakishasema ni swala la kiimani huwezi pata a logical answer, Never.
With regard to this question, wakatoliki watasema kuungama kupitia padre ni swala la imani yao, na wakiingia katika imani, manake hakuna logical answer.
Wakatoliki to a greater extent wanaweza kwa sababu ni very practicle.Haya mambo ukifikiria sana kichwa kinaweza pasuka
Binafsi nimesoma shule zinazoongozwa na katoliki wenyewe wanakuambia kabisa hizi imani zipo kila mtu na yake ila binadamu wote ni wamoja na tusiache hizi dini zitutenganishe
Tatizo kubwa Sana..
Usimuabudu binadam
Binadam hatuaminiki na sio wakamilifu na watakatifu, kwanini ukamtubie mtu et akuombee.. Nonsense kabisa.
Dini uchafu umezidi Sana tulio na neema ya kujua Mungu anataka Nini huwezi kusumbuka na Dini..
Hi yote inatokana na ujinga na umasikini lazima utakuwa mtumwa wa dini.
Ukiamini huko utapata baraka, miujiza, kwenda mbinguni( wakati unafanya mabaya hiyo mbingu gani) kupona magonjwa( mengine Ni sababu ya afya na lishe duni, kazi ngumu n.k badala ya kwenda hospital unaenda kanisani ukiona bado unaenda kwa waganga au unakuwa unafanya vyote kwa pamoja yaani unafiki).
Viongozi wa dini nao ni tatizo kuwakalisha waumini muda wote kanisani ili wapate pesa, uzinzi, hawafundishi watu kuishi maisha mema na kutenda wema kwa wengine. Wanacho waza ni vipi michango itolewe n.k
Watanzania ujinga na umasikini unatupeleka pabaya Sana.
Maelezo yako ni illogical..hayana mantiki,na mfano wa kumswalia mtume ndiyo umedhihirisha upopoma...umeshasamehewa naye hawasiliani na mungu Kama wote tulivyo na hakika,maana yake yeye ndiye anayesamehe dhambiHusema “umesamehewa dhambi zako " hii inasimama kumaanisha kwamba kupitia yeye (wakati huo huinua mkono kama kukubariki) Mungu amenena na wewe muumini na amepokea toba yako na Padre hukwambia nenda kasali sala fulani ili kujitakasa,haya ni mambo ya kiimani sheikh watu tunajua na tunazingatia.
Kama wewe pale imam anaposema "Tumswalie Mtume" kwani anakuwa amewasiliana na Mungu kwamba Mungu ajiandae kupokea sala za waumini fulani muda huu wanataka kumswalia mtume?
Najuta sana kwa kupiga magoti na kuungama mbele ya binadamu mwenzangu. Ni enzi za utoto bila kujua dini ni nini. Ni mbinu tu za hao Wayahudi kuteka mawazo ya watu kisaikologia. Mf. Ukipanga mbinu za kupindua serikali na baadae ukaacha na kuungama, si jamaa atapeleka jina lako Ikulu? Kulikuwa na adhabu ya kutumbukiza pesa Fulani ili usamehewe!!