Hatimaye maigizo ya Makonda yamchosha Rais Samia

kaongea ukweli sana ila kuna watu hawampendi makufuli
 
Aliingia na approach mbaya na zaidi alikuwa anajibrand mwenyewe na sio chama.

Binafsi, nilimshangaa alipokuwa anaongea na kutoshia mawaziri yaani hadi PM anampoga Mkwara. Nilishtuka zaidi baada ya kuona juzi anatema pumba kwenye mapokezi ya ndege na kutoa tamko la kuwataka wana CCM wasiache kumuingiza Magufuli kwenye mafanikio ya Bi.Tozo.

Jamaa alijua turufu yake aliyokuwa nayo CCM ni JPM na alijitahidi kumuongelea kwenye kila jambo, alijifanya JPM ajaye.
 
Inategemea na aliyepo madarakani atalipokea vipi mzee
Nae hapendi kufanasishwa!
Basi ifutwe ile ya hayati alifanya bora kuliko wote labda sana mwalimu, kisha ijulishwe wa sasa ndie mbora kuliko wote wajao na waliopita.
 
Hili nimelielewa.....kwamba reference na jpm
Binafsi sikufuatilia mapokezi ya ndege ila niliona analiongea hilo wakati naangalia taarifa ya habari. Nilitafakari sana kwani nilishangaa pia. Hata wakati alipoteuliwa na kwenda Chato, sijajua lengo la kusema "bora nife ila sitaweza msaliti JPM" lilikuwa ni nini?

Kimsingi, anajua bado mzee anakumbukwa na kupendwa na watu, ye aliona karata pekee ya yeye kuingia kwenye mioyo ya watanzania ni JPM.
 
2025 itakuwa ngumu sana kwa wapinzani kwenye uchaguzi mkuu.
Uchaguzi wa wapi na kwa ajili ya nini? Yaani Makonda ndio wa kufanya uchaguzi uwe mgumu Arusha? Alishindwa Mzee Lowasa 2012 akiwa anampambania mkwewe SIOI SUMARI dhidi ya Nassari, Makonda atafanya nini? Hivi sijui mnajielewa kweli nyie vijana? Makonda si takataka kabisa ile.
 
Machalii wa R wataishi nae freshi tu maana jamaa amewekeza Arusha sana si mgeni kule.
Yale maduka yake ya kubadilisha fedha za kigeni atayasimamia vizuri na kwa ukaribu zaidi.
 
Kitu pekee ambacho jamaa hakujua ni kina nani wanaendesha nchi hasa! Ile juzi hotuba yake yakupokea ndege iliwavuruga sana watu... ukichanganya na kuwagusa akina Salaaah ndo kabisaaa!
Ile alijichanganya. Msimpambe, mwambieni ukweli anatakiwa ajue anaongea nini na hadhara gani. Sasa ile mikwara aliyokuwa anampiga PM pamoja na Mawaziri sijui atafanyaje kazi nao.
 
Maigizo .Kama kweli amemchoka angemuweka benchi tu.
 
Anataka kubebwa na Nyota ya Marehemu?
 
Wao watatumia mbinu zile zile ila sio kwa sababu ya Makonda.
 
Umewahi kushuhudia yanayoendelea kwenye chumba cha kuhesabia kura?

Hasa anapokuwepo mkuu wa mkoa, wilaya, OCD na RPC upande wa mgombea wa CCM?

Lowassa alikataa hata ushindi aliopatiwa mwaka 2015, hakuwa na baya yule mzee, unadhani Makonda, na genge lake watakataa ushindi wa kulazimisha 2025?
 
We kuna kitu unacho; hotuba ya kupokea ndege lilikuwa ndo boko la mwisho la Bashite; pale Mama lazima aliambiwa unataka huyu fala akutoboe jicho ndo uchukue hatua?
Hata kama wamemshusha cheo ila kwenye Ile hotuba "message sent and delivered"..
 
Maigizo .Kama kweli amemchoka angemuweka benchi tu.
Utaliuzi kundi kubwa la Sukuma gang.Bashite ni picha na alama kubwa ya Mungu wa Chato hajui mungu wake ameshapitwa na zama zake zinatakiwa kusahaulika na kuzikwa.

Magufuli hana faida katika siasa za sasa kumfufua na kumkuza maana yake ni kuendelea kumdidimiza Bi Mkubwa wa Magogoni.

Kuendelea kumtaja taja katika hadhara muhimu za kisiasa maana yake ni kumdidimiza aliyekalia kiti cha enzi kuu ambaye ndio mtoaji mkuu wa ajira zote za maana chamani na serikalini.
 
Ukidai wewe inatosha, acha kutegemea mwanaume mwingine akusaidie kudai haki zako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…