Hatimaye ndoa yangu imevunjika

Ndo maana nikasema hizi stori za kuskilizaga upande mmmoja hazinaga mizania.

Watu wamemhukumu mke wake kana kwamba alkua mkosaji sana.

Binafs naona jamaa alipata mke bora sana,
Ni wanawake wachche sana wanaweza kufunguka kua hawaridhishwi kitandani, wengi wanafake ili maisha yaende.

Mwanamke mpaka anafkia hatua anajichua na anakueleza wazi bila kuficha, ni jinsi gani anampenda na kumthamini jamaa.

Ila badala ya jamaa kufayia kazi yale mapungufu yeye kaenda kukitembeza nje, yote kwa sababu pesa ipo.

Bahati mbaya,
Michepuko nayo inaweza kukiona kibamia ukishafulia, ila ukiwa unahonga pesa wala hajali.
 
Ntaanzaje kwanza kumliza mke wangu?ndio Mana nikiwa nasoma visa vya wake za watu humu huwa namuona mke wangu ni wa pekee Sana
 
Hakika umeongeza kitu kikubwa sana katika maisha yako. Amini nakwambia unapokwenda ni bora kuliko ulikotoka. Mwenyezi akujalie uvumilivu zaidi.
 
Pole sana lakini usishangae baada ya siku si nyingi maisha yako yakawa mazuri na yeye definately kwa kuwa alikokwenda amekwenda kwa tamaa zake, maisha yatakuwa magumu na atakutafuta kukuomba msamaa. Atasema shetani alinipitia.
 
Ni kweli,Mimi nilioa Sina kazi na sikuwa hata na hela,mpenzi wangu(mke kwa Sasa) akasema usiogope tukifunga ndoa baraka zitakuja na kweli Mungu ametubariki.Huyu mwanamke nimeishi naye maisha magumu jaman khaaa
Ole wako umuache sasa 😅😅😅
 
Hahahah mkuu shukuru mungu umepata mke aisee! Kuna wanawake wana upendo sana jamani 😀😀😀 mungu azidi kumbariki huyo mwanamke maana msoto uliompitisha still akawa na adabu inaonesha jinsi gani ambavyo yupo loyal kwako!
 
Kwa maoni yangu kile kitendo cha kwenda kwa mwanamme mwingine kama mwenye kuleta mada anasema kweli basi haya uliyosema sikubaliani nayo. Angesema anakwenda kupanga na kuendelea na maisha yake basi ningkubaliana na usemi wako huu.
 
Ntaanzaje kwanza kumliza mke wangu?ndio Mana nikiwa nasoma visa vya wake za watu humu huwa namuona mke wangu ni wa pekee Sana
Aminaaaa.... mshikilie sana. Usimkose ukaja kutana na akina magige. Utaumbuka msibani kwako. Tutatupa shada lake na tutaimba injili iende mbere[emoji4][emoji23][emoji23]
 
Aminaaaa.... mshikilie sana. Usimkose ukaja kutana na akina magige. Utaumbuka msibani kwako. Tutatupa shada lake na tutaimba injili iende mbere[emoji4][emoji23][emoji23]
Unajua unaweza sema nakuza Mambo,huyu mwanamke ni wa ajabu Sana Yan kipindi anafanya kazi mi nazurura na bahasha tu lkn Kama anataka kutoa hela kwenye akaunt yake(ya mshahara) basi lazima anipe taarifa,Yan hela ni zake lkn ananiomba atoe,just imagine.Hii imenifanya niwe muwazi Sana kwake anajua mshahara wangu na kadi za atm tunaweka pamoja na namba za Siri tumepeana.
 
Usifanye maisha kuwa magumu we mpe pole kwanza ,nani ana makosa sio big deal wewe kujua maana haitaji upatanisho wako
 
Jiandae, ukifanikiwa kuimarika kiuchumi tena, atakuja akiomba radhi kwa jicho legevu na machozi mengi, sura yenye huruma na kukwambia ni shetani tu alimpitia!

Nakumbuka miaka kadhaa iliyopita, kaka yangu alilazimika kuvunja nyumba yake bila kupenda!

Wakwe zake walikuwa na ngumu ya maisha, walitaka kuuza shamba ili wanunue bati,(nyumba yao ilikuwa mbovu sana, enzi hizo ni Kijiji,Mlowo Mbozi mkoani Songwe,wakati huo ni Mbeya)

Baada ya wakwe kufanya hesabu wakabaini pesa ya shamba haitoshelezi idadi ya bati wanazohitaji, wakamuomba brother, awanunulie bati then wampe shamba!
Brother kuonyesha ukidume akawanunulia bati, mbao, misumari na fundi akamlipa (wakamshukuru mno na kumuona mkombozi wa familia kwani kwa bei ya shamba kwa wakati huo wasingeweza kununua vyote hivyo).

Baada ya miaka mingi kupita, lile shamba liligeuka Lulu, kwani thamani yake imekuwa kubwa kiasi kwamba watu walikuwa wanatoa offer za mamilioni, kwani palifaa sana kwa biashara, baba mkwe hakuwa na shida alikuwa ameshahamia mashambani huko...

Shida ikawa mke wa brother na mama mkwe, walipata tamaa baada ya tajiri mmoja kuwaambia atapanunua kwa Million 80, wakaliamsha dude wanataka sehemu yao, ndani pakawa hapakaliki, brother ajanusurika kuuawa kwa kuwekewa sumu na mkewe, (hapo walikuwa na watoto 3)

Shem alipogundua issue ya sumu imeshtukiwa aliamua kutoroka kuelekea kusikojulikana,brother kwa hasira aling'oa tofali zote,bati zote akaacha kiwanja tu, mke aliporudi hakukuta nyumba,maajabu zaidi ni jamaa aliykuwa tayari kununua lile eneo alifariki kwa ajali ya gari (hiece ilikuwa inaitwa MTIMA, iliua abiria wote)

Shem akakosa pa kuishi, bro akaanza kujenga upya sehemu nyingine, na huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa mpya wa maisha yake.
 
Mbona tuupo wengi tu[emoji28][emoji28]
Ila tuwe tunaongea lugha moja. Nikavumilia nikaona unaendelea na ujinga nakuacha.


Rafiki yangu ameolewa. Mpambanaji mno. Mumewe pia alikua poa. Akafukuzwaga kazi. Mke akawa anaitunza familia kwa mwaka mzima. Yaan kutoka moyoni. Baada ya mwaka jamaa mambo yakarudi kwenye form maradufu. Friend wangu alikua na benz. Mumewe akamsuprise na matako ya nyani as a suprise na kumshukuru saana. Nawapenda mno aisee. Wanaume wazuri wapo na wanajua kuappreciate. Na rafiki yangu ni mzurii huyoo. Ana tako kubwa ila ana akili huyu[emoji23][emoji23] May God bless her everyday... namuombea ndoa yake iwe ya baraka bila kikomo
 
Hapana usioe kwa tamaa Mimi nilio shepu kumbe kichwani box tupu
Usihuzunike sana mzeee pisi kali zinahitaji hela kwa maana alifata hela sasa zimeisha inabidi aangalie upande wa pili,hiyo ndo maana halisi ya pisi kali
 
Kuachwa!kuachwa!
Kuachwa ni shughuli pevu,
Ooh!mbaya zaidi kwa yule unayempenda,
Yeye ananenepa wewe unakonda,
Kwa mawazoooo!kwa mazoooo.
Pole sana baba J
 
Kabisa maana sio kwa mihasira hiyo
 
Wew ni mmoja wa wanaume walobahatika kupata wake wema

Vip hana mdogo wake unipasie mkuu?.....just kidding
 
Pole Mkuu!!! Ni UKWELI usiotia shaka kuwa MAMA mzazi ndiyo mwenye upendo wa dhati na kweli kwa sisi WANAUME katika Dunia hii, kwani MAMA atakupenda ktk hali zote yaani atakupenda ukiwa masikini au tajiri siku zote...

Kwa uzoefu mdogo nilionao, sidhani kama kuna mwanamke anampenda/ atampenda MME wake siku zote na kaika hali zote, kama wapo, basi kwenye [emoji817] hazidi mmoja.

Am very sorry kama ntakuwa nimewakwaza Dada/ wadogo zangu wa kike....
 
wewe utakuwa kati ya wanawake wachache wenye busara katika dunia hii. Hongera Mkuu...!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…