Asalaam,
Ndoa yangu ilikua nzuri saana kwasababu tulianza tukiwa vijana wadogo maskini, kutokana na hivyo tuli inspire vijana wengi na ndoa nyingi kusimamia.
Tuka barikiwa watoto wazuri. Mungu alitubariki na unafuu wa maisha wa kupata tunachokita kwa level ya maisha ya kawaida. Basi ghafla maisha yakabadilika nikaanza kupitia magumu kiuchumi hata jero mtihani kupata.
Balaa lilianza hapo kudharaulika, kununiwa, Visa vya kila aina mpaka hatimaye Mimi ndiye nikawa "mama wa nyumbani" na yeye akawa anarudi nyumbani ka guest house ni kulala tuu bila kujali hata watoto wanna hali gani.
Biashara nimemfungulia mwenyewe, na hata kodi nimekua nikimsaidia kulipa. Pamoja sasa Sina shughuli maalumu lakini Mungu ananisaidia kumudu kutimiza mahitaji muhimu ya familia yangu.
Sasa amepata mwanaume mwingine na amenidhibitishia na nilipohitaji aende kwao akapumzika akaniambia hawezi atabaki Dar aendeleze maisha yake kwakua anashida saana ya hela. Kumbe nia yake ni kuendelea kuishi na huyu mwanaume.
Leo nimedhibitisha. Ndoa yangu haitakuwepo tena baada ya kukamilisha taratibu za kisheria.
Roho inauma kwakua sikutegemea kama wanangu wataishi na mzazi mmoja.
Wanaume tutafute hela, ndo thamani yetu!
#Mwanamkemkwelinimamayakotuu
Jiandae, ukifanikiwa kuimarika kiuchumi tena, atakuja akiomba radhi kwa jicho legevu na machozi mengi, sura yenye huruma na kukwambia ni shetani tu alimpitia!
Nakumbuka miaka kadhaa iliyopita, kaka yangu alilazimika kuvunja nyumba yake bila kupenda!
Wakwe zake walikuwa na ngumu ya maisha, walitaka kuuza shamba ili wanunue bati,(nyumba yao ilikuwa mbovu sana, enzi hizo ni Kijiji,Mlowo Mbozi mkoani Songwe,wakati huo ni Mbeya)
Baada ya wakwe kufanya hesabu wakabaini pesa ya shamba haitoshelezi idadi ya bati wanazohitaji, wakamuomba brother, awanunulie bati then wampe shamba!
Brother kuonyesha ukidume akawanunulia bati, mbao, misumari na fundi akamlipa (wakamshukuru mno na kumuona mkombozi wa familia kwani kwa bei ya shamba kwa wakati huo wasingeweza kununua vyote hivyo).
Baada ya miaka mingi kupita, lile shamba liligeuka Lulu, kwani thamani yake imekuwa kubwa kiasi kwamba watu walikuwa wanatoa offer za mamilioni, kwani palifaa sana kwa biashara, baba mkwe hakuwa na shida alikuwa ameshahamia mashambani huko...
Shida ikawa mke wa brother na mama mkwe, walipata tamaa baada ya tajiri mmoja kuwaambia atapanunua kwa Million 80, wakaliamsha dude wanataka sehemu yao, ndani pakawa hapakaliki, brother ajanusurika kuuawa kwa kuwekewa sumu na mkewe, (hapo walikuwa na watoto 3)
Shem alipogundua issue ya sumu imeshtukiwa aliamua kutoroka kuelekea kusikojulikana,brother kwa hasira aling'oa tofali zote,bati zote akaacha kiwanja tu, mke aliporudi hakukuta nyumba,maajabu zaidi ni jamaa aliykuwa tayari kununua lile eneo alifariki kwa ajali ya gari (hiece ilikuwa inaitwa MTIMA, iliua abiria wote)
Shem akakosa pa kuishi, bro akaanza kujenga upya sehemu nyingine, na huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa mpya wa maisha yake.