Hatimaye ndoa yangu imevunjika

Hatimaye ndoa yangu imevunjika

...Kuwa single father sio swala la kuhitaji kuhurumiwa!
Wa kuhurumiwa ni hicho kijibwa kilichhondoka!
Kwa nini Uhurumiwe?
Wewe umebaki na maisha yake. Wewe ndio umebaki na watoto watoto wako. Yeye ndiye kila akilala ni lazima awakumbuke watoto wake ambao amewatosa bila kosa lolote ila kwa sababu tu baba yao sasa hana mbele wala nyuma!!
Mkuu ajitahidi tu asonge mbele na maisha yake na watoto wake tu. Hao ndio ndugu zake. Huyo kidampa atarudi tu....!!
Upo sahihi ila nilikuwa namaanisha(kiutani) hawa wadada wa humu wachangamkie fursa
 
Nina rafiki yangu wa karibu, sio kuhadithiwa ni kushuhudia, alifanyiwa vituko hivo vya kufanya tendo la ndoa mpaka siku za hedhi kwa miezi 8 mfululizo. Siku walipoachana yule mwanamke akamtumia kipimo chake alichopima miezi 8 nyuma cha HIV kikisoma ameathirika pamoja na tarehe. Na akamuambia hakuanza dose za ARV kwa makusudi ili amgawie na yeye hayo maradhi.

Jamaa alichanganyikiwa akawa anaongea peke yake, ndugu na marafiki ilibidi tusaidiane kumpeleka kwa daktari wa saikolojia akatibiwe. Dokta alifanikiwa kumshawishi apime ili ajitambue kama ni muathirika aanze kutumia dawa, baada ya kupima kipimo kilitoka HIV NEGATIVE. Baada ya mwezi mmoja akapima tena akakutwa HIV NEGATIVE. Baada ya miezi mitatu akapimwa tena akakutwa HIV NEGATIVE.

Na yeye akamtumia vipimo vyote yule aliekua mke wake, haikupita miezi mitatu yule mwanamke alikonda na kuwa kama mdoli.

#Mungu yupo, halali wala hapumziki, na anawalinda waja wake kwa njama mbaya.

Aisee watu wabaya jamani dunia hii[emoji1381]‍♀️
 
Back
Top Bottom