GE2025 Hatua zisipochukuliwa kuna hatari siku ya uchaguzi ikawa siku ya aina yake. Watu hawatajitokeza kupiga Kura hasa maeneo ya mijini

GE2025 Hatua zisipochukuliwa kuna hatari siku ya uchaguzi ikawa siku ya aina yake. Watu hawatajitokeza kupiga Kura hasa maeneo ya mijini

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Inasikitisha maana wanaoenda kwenye kampeni ukiwaangalia vizuri sura zao hazina nuru, umaskini umewajaa yaani wamechoka ile chokest mbaya hadi huruma na ndo huwaambii kitu kuhusu CCM. Kweli uchawi upo
Hao wanabebwa na malori, wengine wanafunzi wanajazwa huko, kama SIO hivyo pangekua peupe, watu hawajajaa tuu imetumika pesa ndefu hapo
 
TZ ilivyo kubwa kura za kuiweka ccm madarakani zitakuwepo na ushahidi ni hawa wanaojaza mikutano, utawakataa vipi kuwa si wapiga kura na wapo eneo la tukio la kunadi sera ili wachague?

Kusema waliletwa kwa malori kujaza uwanja hiyo si hoja.

Hawa hapa wapiga kura:
View attachment 3465134
CCM inategemea Kura kuingia madarakani? Umenishangaza
 
Hamjambo!

Sijui hatua gani zichukuliwe lakini kwa ninachokion huku mitaani. Ni wazi siku ya uchaguzi itakuwa siku ya aina yake.

Mwaka 2020 nilibahatika siku ya uchaguzi kutembea kuanzia Arusha mjini, Moshi mjini, mwanga Mjini, Same Mjini mpaka nilipofika Makanya kwenye kituo changu cha kupigia kura nikapiga.

Muamko wa kupiga kura hiyo 2020 ulikuwa mdogo sana. Licha ya JPM kukubalika vilivyo.

Round hii nimefanya chunguzi zangu kwenye vijiwe vya Dsm baadhi ya maeneo ikiwemo Kariakoo, Sinza, Magomeni, Kimara, Ubungo na Mwenge. Vijana na watu wengi ukiwafuatilia hawana muamko wa kupiga Kura. Wanakuambia hataenda kupiga kura. Zaidi wengi wao ni wanaccm.

Unaweza hata wewe kufuatilia na kufanya utafiti kidogo.

Sijui kwa kweli!

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Possibility ni kubwa Kwa sababu wale wanaokubalika wamepigwa chini achilia mbali Chadomo.

Ona Hawa wa ACT waliokuwa wamewakalia kooni kina Ester Bulaya na Matiko wameenguliwa.

View: https://www.instagram.com/p/DOMHSPigmxZ/?igsh=MTRrMG04anY0Z2p6dA==

Kwa mazingira haya nani akapige kura? Labda Serikali (Tume & CCM) waweke viburudisho siku hiyo yaani maji ,soda na msosi watu wataenda kiasi.
 
Vijana wa chama cha majambazi kimoyomoyo wanajisemea

"hata msipopiga kura tutawapigia"
 
Sitapiga kura kwenye uchaguzi ambao atakaye tangazwa mshindi anajulikana. Yaani, kura yangu haiheshimiki kwa kiasi chochote kile.
Mwaka huu hakuna uchaguzi. Kuna kiini macho tu.
 
Wasimamizi wa uchaguzi mwaka huu wajipange maana watatiki kwa niaba na idadi ya watoro itakuwa kubwa sana
 
Ni kweli kabisa...ila tusiishie kugomea tu, movement kama NO REFORMS NO ELECTION ziungwe mkono kwa juhudi kubwa
 
Ni utaahira mkubwa sana kupoteza muda kupiga kura wakati matokeo tayari yameshapikwa wanasubiri kuyatangaza tu.
 
Back
Top Bottom