baunsamuoga
JF-Expert Member
- Apr 16, 2023
- 1,135
- 1,182
Tuliza boli, weka gambani, shusha chini dribo kidogo!
Kuna akili kidogo umebakiza kwenye ubongo wako tuwaongezee wenye nazo.?????Maelfu wanaojitokeza kwenye kampeni watapiga.... Nilitegemea watu hawatakua wanaenda hata kwenye kampeni lakini ndio kwanza wanajaa
Juzi jioni nikiwa naelekea nyumbani nilikuwa nasikiliza Clouds FM. Wana reporter wao huwa anatembea mtaani kuhoji watu. Alikuwa mitaani anahoji watu kuhusu uchaguzi. Maswali ya kawaida mfano vyama vinavyogomea,wagombea urais na wagombea wenza....Oh Lord vijana hawana clue uchaguzi lini. zaidi ya mama hawajui mgombea mwingine na hawana interest kabisa. Vijana wa umri kati ya 20-28. Hali inasikitisha. Lakini pamoja na kujua wagombea mimi binafsi siku hio wala sitapoteza muda wangu. nitakaa nyumbani nifanye kazi nyingine.Hakuna haja ya kupiga kura chini ya mazingira yaliyopo.
Ni kazi bure tu.
Kuna haja gani ya kupiga kura wakati wote tunajua matokeo yatakuwaje?
Hao wanaojaa kwenye mikutano wenyewe wanapewa supu na nani?Mbinu za kutumia ili wengi wakapige kura:
1. Supu ziwepo kila kituo cha kura. Ukishapiga kura, unapiga supu.
2. Wapiga kura waandaliwe mabasi mapya (Esther, Abood, New Force, etc) ya kuwapeleka vituoni na kuwarudisha makwao baadae. Malori na mafuso hapana kwa kweli.
3. Kila atakayepiga kura apewe posho dola 200 (TSh 500,000). 500,000 × 37M = bilioni 18.5. Inawezekana hasa ukizingatia zile 86B za harambee!!!
4. Wasanii wote Bongo wasambazwe standby vituoni ili kuwatumbuiza wapiga kura. Wale maarufu zaidi wawekwe sehemu zenye hamasa ndogo sana.
5. Wapiga kura wote wapewe free tickets za kuhudhuria mechi mojawapo muhimu za Simba vs Yanga.
NB: Halafu tena nikikumbuka kuhusu mifumo kusomana kama alivyosema Pole2, naona kabisa hapo juu nimepigaje kweli? Maana ukitiki umetiki, usipotiki umetiki.
cc:
ChoiceVariable
Tlaatlaah
Stuxnet
Pascal Mayalla
Lucas Mwashambwa
Dr wa Manesi
Salary Slip
Retired
Lord Denning
Maelfu wanaojitokeza kwenye kampeni watapiga.... Nilitegemea watu hawatakua wanaenda hata kwenye kampeni lakini ndio kwanza wanajaa
Namba zao za NIDA si wanazo CCM? Watapigishwa kura ya NDIYO wapende wasipende?Hamjambo!
Sijui hatua gani zichukuliwe lakini kwa ninachokion huku mitaani. Ni wazi siku ya uchaguzi itakuwa siku ya aina yake.
Mwaka 2020 nilibahatika siku ya uchaguzi kutembea kuanzia Arusha mjini, Moshi mjini, mwanga Mjini, Same Mjini mpaka nilipofika Makanya kwenye kituo changu cha kupigia kura nikapiga.
Muamko wa kupiga kura hiyo 2020 ulikuwa mdogo sana. Licha ya JPM kukubalika vilivyo.
Round hii nimefanya chunguzi zangu kwenye vijiwe vya Dsm baadhi ya maeneo ikiwemo Kariakoo, Sinza, Magomeni, Kimara, Ubungo na Mwenge. Vijana na watu wengi ukiwafuatilia hawana muamko wa kupiga Kura. Wanakuambia hataenda kupiga kura. Zaidi wengi wao ni wanaccm.
Unaweza hata wewe kufuatilia na kufanya utafiti kidogo.
Sijui kwa kweli!
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Na sio kwamba hawatokei kwakuwa hawataki kupiga kura bila sababu, bali wengi wao huwa hawaichagui ccm, lakini ccm huishia kuchezea matokeo ya kura halali. Katika mazingira yao watu wameishia kupuuza box la kura.Gharama kubwa zitatumika, maandalizi ya karatasi, vifaa, kalamu, n.k. alafu wapigaji kura hawatokei
Ni sawa na kwenda kuangalia mechi recorded kisha ukawa unashangilia kama ni Live.Sasa unaempigia kura nani ?mshindi ameshajulikana nikupoteza muda tu
Sio mshindi, ndio atakayetangazwa mshindi.Ila samia ndio mshindi Robert Heriel Mtibeli
Kwamba huko vijijini ndio bado kuna wajinga wasiojua kuwa kura ziko NIDA?Watu wengi watashiriki mkuu, weeengi tu. Wala usihofu. Najua, Mama Samia Hana bahati na hii mitandao kwa maana haters wake hawana kazi zinazohitaji majibu kwa watu kama yeye kwahiyo Wana muda mwingi wa kuwa mitandaoni na kumsagia kunguni kwa nguvu zao zote lakini amini nakuambia Kuna watu wengi tu Wala hawana shida na Samia. Ndo maana nakuambia, kama nao watapatwa na upepo wa upumbavu unaopulizwa na hao haters basi za vijijini pekee zitahesabiwa.......na kimsingi hizo ndo nyingi mara ELFU ukilinganisha na za mjini.
Nikijibu swali lako; ndiyo, nimewahi kuwa ukiranja wa darasa kwa miaka minne mfululizo.....darasa la 3 Hadi la 7.