Hawa mbu wa siku hizi ni Toleo Jipya au ni walewale wa zamani?

Hawa mbu wa siku hizi ni Toleo Jipya au ni walewale wa zamani?

Nauliza tu kwa kutaka kujua hawa mbu ninaowaona siku hizi ni toleo jipya au? Maana hata uwapulizie na nini hawafi
Juzi nilikua niko kiwanja mpaka mida ya saa nane usiku nikaona sms, nikafungua inasema "Oya hujarudi mpaka sahizi unategemea tutaishije na watoto wetu"?
 
Wanadai watu wenye miili yenye joto zaidi hushambuliwa na mbu zaidi .

Na wenye group o la damu.
Inaweza ikawa kweli aisee. Mie naweza nikakaa kieneo ambacho ni kama hakuna mbu(ni wachache mnoo) basi mie mbu wataning'ata na wenzangu hawasumbuliwi na mbu kabisa, mpaka wananishangaa.
Mimi ni group O

kwenye joto hapo sijui, ukiwa na joto inakuwaje!?
Ila ninavyojiona mimi ni tofauti aisee, joto Kidogo tu basi hapakaliki, kiasi natamani hata kuishi mikoa ya baridi tupu, naweza nikatoka mazoezini, nikatulia kidogo mwili upoe, nikaoga na mwili ukatoa jasho.. joto linanitesa sana.. mara nyingi mtu akinigusa ananiambia mwili wako una joto, wakati mie najionea kawaida tu,
Nishastaajabu sana sasa imekuwa kawaida.
 
Usiseme sana kuhusu joto, nasikia nyie wakaka wenye joto ni deal sana mnatafutwa na wadada mpaka wamama😆
 
Huwezi amin jana tu nilikua nawauliza watu wa home hili swali hawa mbu mbona kama wamevaa mask na helmet halafu wana meno ya vampire?
Kwanza wana mbio wanajua hadi kukata kona wanakuzunguka, 🤯

Pili ukiwapulizia dawa ni kama wanakucheki kwa hasira halafu wanakuja kukushambulia kwa nguvu🤕
Tatu hata uwapige kofi linadunda yaan mbu wanajua kupunch vibao😲

Nne wakikung'ata unahisi maumivu hadi kwenye utosi na lazima uvimbe🥹

Tano wana visasi ikitokea umemuua mmoja japo kwa mbinde, watakuvizia kwenye kona ukikatiza tu wanaanza kukushambulia na 'vimeno' vyao vya kivampire lazima utoke ndukiiii😮‍💨😷😨

Serikali ilitizame hili kwa upana
Chai
 
Back
Top Bottom