Hawa mbu wa siku hizi ni Toleo Jipya au ni walewale wa zamani?

Nauliza tu kwa kutaka kujua hawa mbu ninaowaona siku hizi ni toleo jipya au? Maana hata uwapulizie na nini hawafi
Juzi nilikua niko kiwanja mpaka mida ya saa nane usiku nikaona sms, nikafungua inasema "Oya hujarudi mpaka sahizi unategemea tutaishije na watoto wetu"?
 
Wanadai watu wenye miili yenye joto zaidi hushambuliwa na mbu zaidi .

Na wenye group o la damu.
Inaweza ikawa kweli aisee. Mie naweza nikakaa kieneo ambacho ni kama hakuna mbu(ni wachache mnoo) basi mie mbu wataning'ata na wenzangu hawasumbuliwi na mbu kabisa, mpaka wananishangaa.
Mimi ni group O

kwenye joto hapo sijui, ukiwa na joto inakuwaje!?
Ila ninavyojiona mimi ni tofauti aisee, joto Kidogo tu basi hapakaliki, kiasi natamani hata kuishi mikoa ya baridi tupu, naweza nikatoka mazoezini, nikatulia kidogo mwili upoe, nikaoga na mwili ukatoa jasho.. joto linanitesa sana.. mara nyingi mtu akinigusa ananiambia mwili wako una joto, wakati mie najionea kawaida tu,
Nishastaajabu sana sasa imekuwa kawaida.
 
Usiseme sana kuhusu joto, nasikia nyie wakaka wenye joto ni deal sana mnatafutwa na wadada mpaka wamama😆
 
Chai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…