Hawa ndio Wenye Kurithi Pepo ya Firdaus

Mkuu ,uislam ulikuwepo kabla ya ujio wa Mtume Muhammad SAW.

kwamba waislam wa mwanzo hawakujua juu ya uwepo wa hizo pepo kwa vile tu Mtume Muhammad alikuwa hajazaliwa?
Mkuu iko hivi kama ambavyo Allah ameleta Sheria tofauti katika vipindi tofauti,na ndo hivyo hivyo kuna mambo aliamua aje ayatolee ufafanuzi mwishoni baada ya ujumbe wake kukamilika.

Na Muhammad ndio Mtume wa mwisho hivyo yeye alipewa jukumu la kueleza kinaga ubaga Kwa mapana yake pepo ni ya namna gani na jahanamu ni ya namna gani na mambo mengine mbali mbali.

Lakini kumbuka katika umma zote zilizo pita walikuwa wanaambiwa hakika kuna siku ya mwisho ambayo watu watahukumiwa Kwa mazuri Yao na mabaya Yao pia

Kwahiyo hata umma zilizo pita walijua kutakuwa na pepo na Moto.

Shukrani.
 
Mbona wewe unajenga hoja hata unatamani kujifunza,hao wenzio wanakazhifi na kubeza na kukebehi ni waislam Kama wewe au wanakosa Moja ya sifa tajwa?
Asante mkuu Kwa maoni yako

Unajua binadamu tunatofautiana katika kuyachukulia mambo,kuna mwingine huwa mwepesi Sana kuchukulia mambo personal na mtu kama huyu atajilinda Kwa kukutukana badala ya kuangalia hoja na kuijibu.

Kwahiyo tuvumiliane Tu ndio ubinadamu huo
 
bhachu

Mkuu ningetarajia kutoka kwako uje na hizo satanic verses kisha uniambie imekuwaje Mtume wenu akapokea hizi kutoka Kwa shetani? Hapo nadhani ningekuwa katika position nzuri kujieleza


Shukrani
 
Sawa jumatatu turudi kazini
 
Waterbender

Jamani Wahusika mods tunashindwa kukoti mtu nadhani kuna shida

Mkuu waterbender ukishakuwa peponi kuna mambo mengi mazur mazuri pambana ufike kwanza
 
maramojatu

Nimeshindwa kukoti naona kuna tatizo

Umetaka ufafanuzi juu ya sadaka na zaka

Sadaka na zaka ni kitu kimoja Kwa maana zote ni sadaka,lakini kuna tofauti Kati Yao.

Zaka ni haki maalum ambayo inatakiwa itolewe Kwa wasiojiweza na wote wale ambao wanastahiki kupata zaka,na hutoa mtu mwenye uwezo Kwa hesabu maalumu.

Kwa mfano kuna zaka ya mazao mara nyingi huwa ni nafaka,Kwa mfano kama umevuna magunia Mia Moja ya mpunga basi unatakiwa utoe moja ya Kumi,Kwa maana hapo utatoa magunia Kumi kama zaka yako,na zaka inatakasa Mali ya mja,huo ni mfano mmoja,na kuna zaka ya wanyama vile vile.

Lakini kuna zaka ya Mali au pesa,hii ina kiwango maalum na wakati maalum

Kiwango chake ni mpaka Mali yako ifikie thamani ya gramu 85 za dhahabu ndio unatakiwa utoe zaka na iwe Mali hiyo imekaa mwaka mzima Bila kutumika.

Mfano thamani ya gramu 85 ni kama 9,000,000 hivi ikae mwaka mzima Tu Bila kuitumia halafu unatoa asilimia Kumi ya pesa hiyo ambayo ni Sawa na 900,000 Kwa mwaka mzima.

Kwahiyo Kwa kifupi zaka INA hesabu maalum na kutolewa Kwa kiwango maalum kimahesabu

Wakati

Sadaka haina kiwango maalum na inaweza kutolewa wakati wowote ule

Shukrani.
 
Huku
Duniani tu tunaishi kwa madaraja, madarasani madaraja je wale waliofuzu kukibwa hawastahili kulipwa ujira mkubwa na mola mlezi?
 
Akhy ni moja ya kumi? Kuna shekh niliwahi kumsikiliza alisema sijui kile kiasi unakigawanya mara nne kama sio nane sasa ile moja ya nane ndo unatoa zaka, elimu hii ya zaka sijawahi kuisoma kwa mazingatio
 
Mitume wote wamekuja na ujumbe mmoja, watu wamuabudu allah na waache ushirikina licha ya utofauti wa sheria baina yao.

"Na tumekuteremshia wewe kwa haki kitabu hiki {quran} kinachovisadikisha vilivyotangulia kabla yake katika vitabu na kuvichunga. Basi hukumu baina yao kwa aliyo yateremsha allah wala usifuate matamanio yao kuiacha haki iliyokujia. Kila mmoja katika nyinyi tumemuwekea sheria yake na mwenendo wake. Na lau kama allah angelitaka angeliwafanya nyote kuwa ni umma mmoja, lakini ni kwaajili ya kukujaribuni kwa aliyokupeni, basi shindaneni katika mambo ya kheri, ni kwa allah tu marejeo yenu nyote, na atakuja kuwaambieni yale mliyokuwa mkitofautiana juu yake."

QUR'AN 5:48
 
Mkuu iko hivi

Mwanadamu anahasika Kwa mambo mawili la kumfurahisha au kumchukiza.

Hata wewe kama uko kazini utaambiwa ima ufanye vizur upate promotion au uharibu ufukuzwe kazi,naamini utajua wapi PA kuchagua.

Kwahiyo Dini haikutishi Ila unaambiwa ukweli kuwa kuna njia mbili za kufuata ima ufanye vizur upate pepo au ufanye vibaya upate Moto.

Sasa nyie ambao mnapenda free lunch ndio mnaona Dini zinawabana.

Pambana hakuna pepo ya bure
 
Akhy ni moja ya kumi? Kuna shekh niliwahi kumsikiliza alisema sijui kile kiasi unakigawanya mara nne kama sio nane sasa ile moja ya nane ndo unatoa zaka, elimu hii ya zaka sijawahi kuisoma kwa mazingatio
Ukhty ni asilimia Kumi

Kuna masheikh wengine utasikia wanasema ukiwa na milioni moja waeza Toa zaka,kitu ambacho sio Sawa lazima kuna hesabu ifikie Kwa kulinganisha na thamani ya dhahabu kwasasa wanasema ni gramu 85 za dhahabu lakini hii ni Kwa pesa.

Sio mbaya ukhty ukifanya home work huenda tukapata jingine la kujifunza
 
Nachoshukuru Mungu mi jina langu lipo huko,wewe je umeshaliona lako bloangu kama halipo niongengee nae YEYE akujumuishe?
Kama mambo yangekuwa rahisi kiasi Hicho basi hakuna ambaye angeingia Motoni hata mmoja mkuu

Kumbuka Nabii Nuhu mwanae alizingua lakini Mungu akamwambia achana nae huyo ameshapotea,pamoja na kumuombea msamaha.

Je Mimi na wewe itakuwaje mkuu

Tupambane mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…