Hawa ni watu waliomdhihaki Mungu na kupatwa na shida

Nachozungumzia ni kuwa matatizo humkuta yeyote hiyo ni nature wala haitegemeani na jinsi unavyo mcha sana Mungu kwamba utakua upo salama.

Kwa hiyo hata kwa hao uliowataja ifahamike kiujumla kua walipata matatizo ya kawaida tu bila kuhusisha element za laana.

Ukiniruhusu nitumie mfano wako wa huyo mmiliki wa meli ya titanic na kwa namna ulivyoeleza kua Mungu alizamisha meli kwasababu ya maneno ya dhihaka aliyoyatoa huyo mmiliki basi mwishoni hata mimi nitakosa busara ya uvumilivu hata mimi pia nitamdhihaki Mungu huyo

Kwasababu ile meli ilivyozama haikumuua mmiliki pekee, iliua watu wengi wakiwemo watoto wadogo wasio na hatia.

Kwanini Mungu anakua mpumbavu na kukosa huruma kwa watoto wadogo kuwaangamiza kwenye dhambi ambayo hawajahusika?

Watoto walichangia vipi kwenye hiyo dhihaka?
 
Hizo ni conspiracy tu zinawekwa kwa lengo la kuwaogopesha watu wasijaribu kumdhihaki Mungu

Hii inafanana na ile ya kuwadanganya watu kua ukichana msaafu unageuka kiumbe cha ajabu.
 
Kwahio huyu Mungu ni Visasi na kuonyeshana Ubabe wa Nani zaidi ? Hilo ni jambo zuri lenye tija au la kuogopa na halifai...., Binadamu kama hao huku wakiwepo tunawaita madikteta wala hatuwasifii yaani bila kusifia anakunyoosha ?

Alafu sababu anajua kesho anajua kabisa utamdhihaki kwahio ameacha umdhihaki ili aonyeshe ubabe wake ? Kweli logic na Imani haiwezi kupikwa kwenye chungu kimoja
 
Namba 8 umetulisha tango pori chanzo cha kifo chake kilijulikana overdose ya madawa sasa Hao waliosema hawakupata chanzo waongo
 
Jibu hoja achana na vitisho!? Usiyaishi maisha ya kanisani, kila unachohubiriwa hutakiwi ku rethink logically wewe ni kusema Amen tu. Umiza kichwa hapo ndugu.
 
Na kwa nini asingemuua tu huyo mtengeneza meli na kuipindua meli halafu watu wote wakaopolewa wakiwa hai ili kuuonesha ukuu wake!?

Mambo ya imani haya ukiwa wa ndio, ndio utapelekwa hovyo mnoo
 
Hizo ni conspiracy tu zinawekwa kwa lengo la kuwaogopesha watu wasijaribu kumdhihaki Mungu

Hii inafanana na ile ya kuwadanganya watu kua ukichana msaafu unageuka kiumbe cha ajabu.
Hapo balance kdg sentensi kabla hali ya hewa haijachafuka humu😂

Ova
 
Jibu hoja achana na vitisho!? Usiyaishi maisha ya kanisani, kila unachohubiriwa hutakiwi ku rethink logically wewe ni kusema Amen tu. Umiza kichwa hapo ndugu.

Hoja ipi sijajibu?
Kutokuuliza maswali ndio unaona ni pungufu la kimungu?

Mbona ukitoka unaruhusiwa kuuliza?na kwenye semina, mafunzo mbalimbali unaruhusiwa kuuliza maswali?

Kwenye imani hatuhitaji kuthink logically we just believe.
 
Na kwa nini asingemuua tu huyo mtengeneza meli na kuipindua meli halafu watu wote wakaopolewa wakiwa hai ili kuuonesha ukuu wake!?

Mambo ya imani haya ukiwa wa ndio, ndio utapelekwa hovyo mnoo
Imani ni ndio ndio mzee.

Ni hakika ya mambo yatarajiwayo bayana yasiyoonekana.

Hatutumij logic.
 
HOJA YAKO INAWEZA KUWA NA MASHIKO KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE. HATA HIVYO, UTENDAJI WA MUNGU (WA IBRAHIMU, ISAKA, NA YAKOBO; BABA WA BWANA WETU NA MWOKOZI WETU YESU KRISTO) UMEBADILIKA KWA NAMNA FULANI KTK AGANO HILI JIPYA LA KWELI NA NEEMA AMBAPO UHUSIANO WA BINADAMU NA MUNGU UNAJENGWA KWA IMANI ILIYO JUU YA MSINGI WA UPENDO. SIYO KWA MSINGI WA SHERIA KAMA ILIVYOKUWA WAKATI WA AGANO LA KALE. KUMBUKA KTK AGANO HILI MUNGU AMEWEKA SIKU MOJA TU ATAKAYOWAHUKUMU WANADAMU. ALIYEISHI KWA KUMWABUDU MUNGU KTK ROHO NA KWELI (ALIYEOKOKA) - HUKUMU YA KUURITHI UFALME WA MUNGU; ALIYEISHI MAISHA YA DHAMBI - HUKUMU YA KWENDA KUTUMIKIA ADHABU YA MOTO JEHANAMU.
IKUMBUKWE, MUNGU SI MWEPESI WA HASIRA, YEYE HUVUMILIA ILI BINADAMU WOTE WAFIKIRIE TOBA. WATUBU. MUNGU NI MWENYE REHEMA NYINGI NA FADHILI ZAKE NI ZA MILELE.
KUMBUKA, MUNGU ANASAMEHE DHAMBI ZOOTE! ISIPOKUWA DHAMBI YA KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU. HIYO HAISAMEHEKE KTK ULIMWENGU HUU AU ULE UJAO.
CONCLUSION:
SIONI DHAMBI KUUBWA YA KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU WALIYOFANYA NDUGU HAWA HATA WAPATWE NA MAUTI NASI TUSINGIZIE KUWA NI MUNGU KAWAUA. HAPANA. DHAMBI ZAO WENYEWE NDIYO ZILIWAMALIZA. MWENYEZI MUNGU HAHUSIKI KABISAA! TENA NAWEZA THUBUTU KUSEMA NI SHETANI-IBILISI NDIYE ALIYEWAUA KABLA HAWAJATUBU ILI WAUNGANE NAYE JEHANAMU.
MASIMULIZI YA NAMNA HII YAKO INSPIRED NA SHETANI ILI WANADAMU TUTILIE MASHAKA JUU YA UPENDO WA BABA YETU ALIYE MBINGUNI KWETU; JEHOVAH ADONAI.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…