Hawa ni watu waliomdhihaki Mungu na kupatwa na shida

Nakupa list ya wachungaji na masheikh ambao hawakumdhihaki Mungu na walipata shida na kufariki

1. TB JOSHUA
2. MAMA LWAKATALE
3. STEPHEN AKNOLA
4. ISSA TURAY
5. WILSON BADEJO

Sheikh nooren mohammed hakumdhihaki Mungu lakini alikufa kwa ajali mbaya sana.

Sheikh Saeed bin nahynan huyu kafa siku nne zilizopita naye kwa ajali mbaya sana na hakumdhihaki Allah

Rashid bin Mohammed naye alikufa kwa shambulio la moyo na hakuwahi mdhihaki Mungu.

Na sio tu hao wapo wengi sana wamekufa na wengine wakipata shida pasipo hata kumdhihaki Mungu.

Kinachokufanya uone hao watu uliowataja kua wamepatwa na shida kutokana na wao kumdhihaki Mungu ni kipi? Nani asiyepata tabu hapa ulimwenguni?

Huyo Mungu wako historia ya dini inaonesha yeye ndio alikua muanzilishi wa kupata tabu baada ya vita yake na shetani ambapo shetani alizua utata huko juu mpaka akafanikisha kusepa na robo tatu ya malaika unafikiri tabu aliyoipata huyo Mungu ilikua ndogo?

Kwa hiyo nayeye tuseme alimdhihaki nani mpaka ikamfika hiyo tabu?
Kikukwa cha kufahamu ni kwamba Mungu hadhihakiwi kwa namna yyt
 
Imani ni nini ?
Imani ni kukubali kitu bila uthibitisho.

Nikikubali kuwa wewe Mubarridi ni Mfalme wa Bahrain, bila uthibitisho, hiyo ni imani.

Kama kiukweli wewe si Mfalme wa Bahrain, imani hiyo kwamba wewe ni Mfalme wa Bahrain, haikufanyi wewe kuwa Mfalme wa Bahrain.

Tukichunguza na kuthibitisha kuwa kweli wewe ni Mfalme wa Bahrain, habari ya kwamba wewe ni Mfalme wa Bahrain inakuwa si imani tena, inakuwa fact iliyothibitishwa.
 
Unaamini unachoamini au umethibitisha?

Unaelewa kuwa kuamini si kuthibitisha?
Ha ha ha ha

Kwa mambo ya Mungu sihitaji uthibitisho wa kibinadamu.

Ninapoona tu kuwa mwanadamu hajaweza kuumba mtu na kumpa pumzi, hajaweza kuufanya mmea usikauke na kufa, hajaweza kuumba dunia nyingine, nathibitisha kuwa yupo mwenye nguvu kuliko wote.... Mungu.
 
Hapo ni sawa na wewe useme kwa kuwa hakuna kiwanda cha BMW Tanzania, basi BMW limetengenezwa na Mungu!
 
Imani ni kukubali kitu bila uthibitisho.
Marejeo ya hii maana ni kwa nani ? Nani amekwambia hii maana.

Sababu nikiipima kwa mzani wa maana ya maana hii maana haikai.
Nikikubali kuwa wewe Mubarridi ni Mfalme wa Bahrain, bila uthibitisho, hiyo ni imani.
Hiyo si imani. Bali umekubali jambo la uongo lisilokuwepo kwa ujinga wako.
Kama kiukweli wewe si Mfalme wa Bahrain, imani hiyo kwamba wewe ni Mfalme wa Bahrain, haikufanyi wewe kuwa Mfalme wa Bahrain.
Umerudia kile kile.
Tukichunguza na kuthibitisha kuwa kweli wewe ni Mfalme wa Bahrain, habari ya kwamba wewe ni Mfalme wa Bahrain inakuwa si imani tena, inakuwa fact iliyothibitishwa.
Sasa imani ina pande mbili uongo na kweli. Kuna imani ya kweli na kuna imani ya uongo.

Mfano mimi nina amini ya kuwa Ulimwengu umeumbwa na haujajiumba wala haujatokea pasi na chochote. Hii ni imani na ni uhalisia.
 
Marejeo ya hii maana ni kwa nani ? Nani amekwambia hii maana.

Sababu nikiipima kwa mzani wa maana ya maana hii maana haikai.

Hiyo si imani. Bali umekubali jambo la uongo lisilokuwepo kwa ujinga wako.

Umerudia kile kile.

Sasa imani ina pande mbili uongo na kweli. Kuna imani ya kweli na kuna imani ya uongo.

Mfano mimi nina amini ya kuwa Ulimwengu umeumbwa na haujajiumba wala haujatokea pasi na chochote. Hii ni imani na ni uhalisia.
Imani ni nini?
 
Hapo ni sawa na wewe useme kwa kuwa hakuna kiwanda cha BMW Tanzania, basi BMW limetengenezwa na Mungu!
Sasa niambie unafikiri dunia imeumbwa na nani? Au imetokeaje?

Na wewe umetoka wapi?

Mwanadamu wa kwanza alitoka wapi? Aliibuka tu?
 
Imani ni nini?
Imani ni tamko lenye asili ya Kiarabu lenye maana ya kusadiki kwa moyo juu ya jambo yaliyo fichikana na kutamka kwa ulimi juu ua uwepo wa jambo fulani na kutenda kwayo. Yaani kuifanyia kazi imani hiyo.
 
Kwa hiyo kabla ya Mwarabu kututawala hakukuwa na Imani!?
 
Imani ni tamko lenye asili ya Kiarabu lenye maana ya kusadiki kwa moyo juu ya jambo yaliyo fichikana na kutamka kwa ulimi juu ua uwepo wa jambo fulani na kutenda kwayo. Yaani kuifanyia kazi imani hiyo.
Imani si tamko lenye asili ya kiarabu.

Dhana ya imani ilikuwepo kabla ya kiarabu kuwepo.

Hjaelewa hata nilichokuuliza ni nini.
 
Back
Top Bottom