Hawa watu wanaondoka kawaida au kuna system inawaondoa kwa kutumia akili kubwa sana?

Hawa watu wanaondoka kawaida au kuna system inawaondoa kwa kutumia akili kubwa sana?

Habari Wakuu,

Inafika hatua naanza kujiuliza hawa watu wanaondoka katika mazingira ya kawaida tu au kuna system inawaondoa kwa kutumia mbinu zilizoenda shule?

Yaani Bwana yule na watu wake wa karibu wanaondoka mmoja baada ya mwingine huku yule mwingine akiponea chupuchupu baada ya kudaiwa kuugua Covid iliyomlaza kitandani na kulazimika kutumia mtungi kuokoa maisha yake ingawa leo kapanda cheo.

Naanza kujiuliza hii Covid ndio inatumika kuwaondoa maana kwa Bongo imekuwa ni too much katika kuondoa vigogo? Na kama ni Covid, mbona wanasita kuitaja? Au ndio wanatumia mwanya huu kuondoa ile inner circle yote ya Bwana Yule?

Yaani sasa napata mashaka kuwa huenda wanaishi na nyoka anaewagonga na kuwatemea sumu pasipo wao kujua. Nyoka huyo huenda asili yake ni humu humu ndani au katengenezwa kutoka huko nje ila kwa kushirikiana na wa ndani.

Hivi sasa hata ukiangalia baadhi ya picha zao za pamoja, utaona jinsi walivyopukutika mmoja baada ya mwingine mpaka unabaki kushangaa.

Kwa mtazamo wangu, hali hii sio ya kawaida wakuu unless ni hisia zangu tu.

Anyway, time will tell.
Hawaondoki hivi hivi, inasemekana kule juu yule jamaa amekwaa uteuzi, ameshakuwa kiongozi wa malaika, so anawaita washkaji zake mmoja baada ya mwingine wakaunde tena serikali ya kidikteta
 
Baada ya miaka 10 kuanzia sasa, panapo majaliwa yote yaliyomo sirini yatawekwa bayana...Hii aina mpya ya WMD itatumika sana.
Kuna watu wameungana kulipa KISASI ambacho wao wanakijua.
 
Ipo namna yani kama ni ugonjwa kwanini uwe na selective sampling? Yani ukaangalia wanaonyofolewa ni watu flani specific badala ya random! Ina maana hili tatizo liko kwa ajili ya watu maalum tu? Seems like theres a specific mission ya ki undercover
Wengi wao ni vijana wa 90s na walikuwa wazee wa mtelezo, konekti doti korona ikigusa kidogo tu basi.
 
kuna qicha moja inasamba sana kwenye mitando iko sytmatc ikianza na kijaz,stendi ya mwendazake,daralaja la aliyetutoka leo na the last one inafikirisha sana but wacha tuone
IMG_20210522_111131_196.jpg
 
mkuu pole Sanaa!!! naona bado una maumivu ya kufiwa,
ukumbuke pia mke wa Azory gwanda na familia yake Hadi leo Wana majonzi kiasi gani, na kina Ben saanane,na Wengine wengi,

Acha twende na Samia Hadi #2035* ameonyesha ana utu na mwenye huruma na hofu ya Mungu,
hata akija kuvurunda huko mbele,tunachotaka watu waishi kwa amani tu,mambo ya watu kuishi kwa hofu kwenye nchi yao ni upuuzi, sawa boss!!
Amani imekuwepo tangu 1961 haya ya watu kupotea yalianza na Nyerere na tutakufa tukiyaacha, wanapotea watu Russia na US sembuse TZ!.
 
Hawa virus washenzi kweli, siku hizi wanakula kimyakimya, ukianza kuhisi vibaya tu kwa heri, yule mama aliefariki ghafla akila futari hoteli gani sijui, ni uthibisho kuwa covid wako kazini na wanatafuna kimya kimya tu, siku hizi hukohoi wala kutoa mafua.

Kwa msiojua huu ugonjwa ni cardiovascular disease, sio Respiratory.
Labda tusaidie kujua maana hayo maneno mawili. CARDIOVASCULAR na RESPIRATORY
 
Habari Wakuu,

Inafika hatua naanza kujiuliza hawa watu wanaondoka katika mazingira ya kawaida tu au kuna system inawaondoa kwa kutumia mbinu zilizoenda shule?

Yaani Bwana yule na watu wake wa karibu wanaondoka mmoja baada ya mwingine huku yule mwingine akiponea chupuchupu baada ya kudaiwa kuugua Covid iliyomlaza kitandani na kulazimika kutumia mtungi kuokoa maisha yake ingawa leo kapanda cheo.

Naanza kujiuliza hii Covid ndio inatumika kuwaondoa maana kwa Bongo imekuwa ni too much katika kuondoa vigogo? Na kama ni Covid, mbona wanasita kuitaja? Au ndio wanatumia mwanya huu kuondoa ile inner circle yote ya Bwana Yule?

Yaani sasa napata mashaka kuwa huenda wanaishi na nyoka anaewagonga na kuwatemea sumu pasipo wao kujua. Nyoka huyo huenda asili yake ni humu humu ndani au katengenezwa kutoka huko nje ila kwa kushirikiana na wa ndani.

Hivi sasa hata ukiangalia baadhi ya picha zao za pamoja, utaona jinsi walivyopukutika mmoja baada ya mwingine mpaka unabaki kushangaa.

Kwa mtazamo wangu, hali hii sio ya kawaida wakuu unless ni hisia zangu tu.

Anyway, time will tell.
Bado yule kipara wa mjengoni
 
Magufuli, Kijazi na Mfugale Hawa watu kwa miaka 20 iliyopita wamefanya kazi kwa karibu sana kati ya TANROADS na Ujenzi. Hao wameshirikiana sana kugawana rushwa itokanayo na mikataba ya Ujenzi.

Ndiyo kisa wakawa wanabatiza madaraja kwa majina yao. Siyo ajabu kuona wote wanaondoka kwa COVID19
Safi sn mkuu
 
Maneno yote yamenyooka ila neno
System kwenye bandiko lako imenyifinya kwakuonyooka
 
Eti covid inabeba baba tuu familia yake hakuna anayepata hata mafua!.huu ni mchezo mchafu na Mungu atatulipia tuu mda si mrefu
😳 Ndiyo maana issues za kisiasa na utawala siyo za kushabikia kwa haraka, mwenye akili timamu unatulia kuangalia mchezo unavyokwenda.
 
Mkuu maneno yako ni mada inayojitegemea.

Kila mtu hakosi mema yake, JPM alimaliza matatizo yote ya ufisadi wa umeme ndani ya mwaka mmoja.

Kafufua shirika la reli linaendeshwa na wazalendo, kafufua shirika la ndege na zinakuja tatu siku zijazo.

Kawezesha madini kuchenjuliwa hapa hapa TZ.

Akaihamisha Dodoma serikali ndani ya miaka miwili waliomtangulia miaka 40 iliwashinda.

Hizo story nyingi za ukatili Ni za upande mmoja, ule wa pili haupo kwani anayesemwa yupo ndani ya ardhi kwa sasa.

Upande wa ufisadi na uonevu ambao hayati alipigana nao unao watetezi, wamejaa humu jukwaani.
Wajinga majizi na bendera fata upepo hawawezi kukuelewa
 
Back
Top Bottom