Haya mafuriko ya leo Ifakara ni hatari

Hatari sana 🙄 !
 
Mwenge ulishatoka Ars cku nyingi hata Kilimanjaro umeshapita uko Tanga.
 
Mafuriko yametufedhehesha mno mwaka huu
 
Sijaupatia picha mto Lumemo kwa namna ulivyofurika! Maana kila maji yanapojaa kwenye huo mto, basi mafuriko lazima yaukumbe huo mji wa Ifakara.
Mto Lumemo umemwaga sio mchezo ni balaa!! Kifupi kama unatokea Kibaoni kuja mjini, kuanzia ilipo Villa Lodge kote maji yamefurika balaa.

Njoo mpaka Kona ya Jerusalem kote huko ni maji tu, kama unafahamu barabara ya kwenda PK arena nako ni maji yanapita juu ya barabara kama mto..

Sogea mbele kama unaenda Ester Petrol station huko kote ni maji.. wenyeji wanasema imewahi kutokea muda mrefu.. kifupi Ifakara imeloa sasa yote tisa huko wanaita Katindiuka ndo mziki mnene
 
Dah! Huko Katindiuka tangu enzi hizo! Mvua kidogo tu, hakupitiki.
 
Unasema iliwahi kutokea zaidi ya hii
Yeah, El nino ya 1995s mpaka 2000s mwanzoni ilikuwa kiboko na funga kazi. Zama hizo hamna mitandao ya kijamii lakini kila kona ya nchi iliipata habari yake!

Ule ukame siyo mchezo!Halafu hii ya sasa hivi ndani yake kuna masika yaani kama inafuata majira yake ya kawaida.

Nb: Hii ni masika au El nino??
 

Elnino ni hali ya hewa inayofanya kuwe na ongezeko kubwa la mvua kuliko ujazo unaorekondiwa kwa msimu. Mfano mvua za mwaka jana kipindi chote cha masika ujazo wake sio sawa na huu.

Sasa sina hakika kama hizi mvua ni za Elnino ama la.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…