Haya matukio yamenifanya nijitafakari upya tabia zangu

Mi pia ni introvert... and i hate it. Tatizo kubwa kabisa tulilonalo sisi ma introvert ni kwamba hatuna ile art of interaction. Tunapenda kukaa pekee. Mtu kama unakosa art of interaction hata connection hupati. Maisha sikuhizi yanahitaji connection, kazi, biashara mishe mbali mbali ya kimaisha inahitaji watu. But us we choose to be alone. Nimeanza kujifunza art of interaction taratibu lakin naona nashindwa. Ila tukiwa nyuma ya keybord tunamaneno mengi hatariπŸ˜…
 
Maisha ya kuwa mwenyewe mwenyewe ni mabaya sana ila wengi hawalioni hilo. Kuna kaka mmoja alihamia mtaani, hakuwa na muda hata na majirani zake ni yeye na mambo yake kivyake, alikutwa ndani kafariki baada ya kuanza kutoa harufu.
Changamana na watu unaoishi nao kama majirani japo msizoeane sana.
Watumiaji addicted wa simu wana hii changamoto sana.
 
Mambo ya kujifungia ndani siwezagi nimepanga na watu introvert lakini huwa na wachangamsha naweza enda hata kuwaazima kiberiti ili nisikie tu Sauti zao kuwa wamo ndani na ni wazima wakati kebriti ninacho ndani kwangu.
 
Kufa tutakufa, ila tunaangalia umekufa katika hali gani??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…