Haya ndiyo matokeo ya kupeleka wahuni bungeni. Wanajiona wana mamlaka kwenye kila jambo.

Attachments

  • 6405238-eae1ceee959bf6fd97d9fb2eab102cc4.mp4
    9.2 MB
Wala haihitaji kuwa na degree kujua haya. Nashangaa watu wanaomlaumu huyo ofisa na kumtrtea baba levo.
Bongo watu wanaishi kimazoea sana kiasi kwamba kuna mambo kibao yanaonekana ya kawaida lakini kiuhalisia yanavunja sheria. Siku agency zote zikiamua kutekeleza majukumu yao kwa asilimia 100, kutakuwa na vilio nchi nzima.
 
Hilo la Baba Level kusema ni "Nyie TRA huwa mnatudharau Wabunge"

ishanifanya nigundue kuwa kuna namna TRA wanawachukulia Wabunge na inawezekana wapo sahihi Kabisa, na hapo huyo jamaa wa TRA yeye amesimamia miiko ya kazi yake ya kujali Privacy ya Mwenye gari

Bora Ommy Dimpoz ndiye angekuwa anabishana nae na sio Mtu wa tatu kisa ni Mbunge
 
Huyo ofisa yuko sahihi. Hawezi kutoa taarifa za mteja kwa third party. Na kamwambia amuulize Ommy mwenyewe atampa taarifa.
Ofisa wa TRA yupo sahihi mno na ndio miongoni mwa ethics za kazi yake ila baba levo anatumia mihemko kutaka kujua taarifa binafsi za mtu mwingine kwa kisingizio cha ubunge. Baba levo kajidhalilisha sana.
 
Mkuu tunafanya kazi na TRA kila siku. Utaratibu wao haupo hivyo nna imani mteja wao ameshapewa sababu.
 
Hapa baba levo alikosea. Mtu anekwambia Mimi siruhusiwi kutoa taarifa za mteja. Muulize mteja mwenyewe akwambie then unaendeleaje kumuuliza mtu wakati ameshakueleza namna ya kupata taarifa.
Ni sawa na baba levo aende hospital amkute ommy anaumwa then amwambie daktari Mimi kama mbunge niambie ommy anaumwa nini?. Kisheria daktari atakataa kutoa taarifa za mgonjwa hata kama zimeulizwa na mbunge inabidi mgonjwa amwambie mwenyewe baba levo au atoe idhini ya kumwambia daktari toa taarifa zangu tu Haina shida Tena daktari anatakiwa awepo na ushahidi wa maandishi kuwa mgonjwa amekubari taarifa zake za Siri kwenda Kwa Fulani na uthibitisho ni huu hapa.
 
Hii ni shida Kwa kweli ingekuwa ni Mimi Sasa hivi tayari nipo kolokoloni huwezi ongea na Mimi kama mtoto wako namna hio Tena huku unanionyeshea na vidole. Shenzi kabisa alafu analalamika kuvunjiwa adabu yeye haoni kama amemvunjua mwenzie adabu pia.
 

View: https://youtu.be/gPQMqI_ge2A?si=9eHLwwk4LN_Ow0_e
Jipitishe hapa angalau itakusaidia kuongeza uelewa

Robert Heriel Mtibeli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…