Hayati Magufuli alikuwa Rais mwovu, Samia Suluhu ni Rais dhaifu. Binafsi heri Rais dhaifu kuliko mwovu

Hayati Magufuli alikuwa Rais mwovu, Samia Suluhu ni Rais dhaifu. Binafsi heri Rais dhaifu kuliko mwovu

Kuhusu yeye alikuwa wapi kipindi cha Jiwe hilo haina haja kupatiwa majibu
Vice president kwa katiba yetu ni kama sanamu tu. Hana authority ya aina yotote

Authority aliyonayo ni ya kujiuvuru ! Hakufanya hivyo !
 
Did he kill you?
Ungeweza kuuliza swali kwa akili zaidi. Swali lako ni upuuzi mtupu.

Hivi hata wanaposema Hitler aliua wayahudi, ni marehemu wa kiyahudi ndio waliotamka? Hata polisi wanaposema kuwa kuna raia fulani ameuawa na majambazi, ni yule marehemu ndiyo huwa anatamka kuwa, mimi nimeuawa na majambazi? Hivi huyo unayemwuliza, kuwa alimwua yeye, kwa akili yako unaamini kuwa kama ingekuwa ni yeye ndiye aliyeuawa, angekuja kufufukia JF aje kulalamika? Kuuliza swali la kijinga kama hilo, unaonekana ama JF ina wagonjwa wa akili au huna swali, umeamua kuandika tu. Jifunzeni kujenga hoja na siyo kuropoka, mnaharibu jukwaa.

Ukiuuliza swali kama hili unaonekana ni mtu aliyekosa kabisa uelewa hata ule wa binadamu mwenye akili ndogo kabisa.

Tafuta swali lisilodhalilisha ubinadamu wako.
 
Bado hamjachoka na propaganda za kumchafua marehemu?
Kila mkipima mnaona bado anapendwa hivyo kuongesa kasi ya uongo wenu.
Eti Rais wa ovyo na mwovu.

Kipindi cha Magu ndiyo sheria ziliheshimiwa kupita vipindi vyote! Siyo sheria za barabarani, sheria za kulipa kodi, sheria za kazi nk. Ndiyo kipindi nilishuhudia hata mahakimu wanahakikisha kesi zinaisha ndani ya muda waliowekewa! Polisi walikuwa na nidhamu! Ukiingia ofisi za umma unasikilizwa. Magu tutamkumbuka daima.

Akiongea dunia inasikiliza. Siyo Afrika tu, Ulaya na marekani, walifuatilia mwamba anaongea nini. Ni kutokana na umakini wake na kutokubali kuchezewa chezewa. Watanzania wengi walimpenda ndiyo maana alichaguliwavkwa wingi kwenye uchaguzi ukiacha hizo porojo zenu za wizi wa kura za akina Mdee!
Tuongee mambo mengine lakini kusema kuwa marehemu Magufuli alipendwa sana, huo ni uwongo wa hali ya juu. Kama una uhakika unapendwa huwezi kuhangaika kuwaangamiza wanaokukosoa wala huwezi kuminya uhuru wa vyombo vya habari.

Kusema kuwa Magufuli alichaguliwa kwa kura nyingi, nao ni uwongo wa hali ya juu. Kama kweli alikuwa ana uhakika wa kuchaguliwa, asingevuruga uchaguzi. Licha ya vitisho, propaganda nyingi, bado yeye mwenyewe kuna maeneo alishuhudia kuwa watu wengi hata waliohudhuria mikutano yake ya kampeni, walikuwa hawamtaki. Kule Njombe mpaka alilazimika kupiga magoti baada ya watu kutotaka hata kuitikia salamu zake.

Magufuli kwenye demokrasia, kuheshimu uhuru na haki za raia, sera za uchumi, alikuwa zero. Score pekee aliyokuwa nayo, ambayo angepata over 80% ni uthubutu. Tatizo alikuwa na uthubutu mpaka kwenye mambo mengine ambayo hayakuwa sahihi.

Utawala wa Samia, ni kama ulivyokuwa wa Kikwete. Utawala wa Kikwete ulikosa uthubutu, ulikuwa na unafiki mwingi kwenye mambo mengi:

1) Alikuwa ni mtu wa kuuma na kupuliza. Alijifanya mwanademokrasia lakini wapinzani na baadhi ya waandishi wa habari walioandika ukweli, waliuawa, na hakuchukua hatua zozote za maana.

2) Uswahiba wa kifamilia ndani ya Serikali haukuwa tofauti sana na wa awamu ya 5.

3) Wizi, ulaji rushwa na ufisadi, ulivumiliwa sana, na hasa ulipofanywa na zile familia za karibu naye.

Tukitaka kuwa wakweli, tawala zilizoongoza kwa rushwa, ni utawala wa Ali Hassan Mwinyi na Kikwete.

Utawala ulioongoza kwa wizi, kwa hali inavyoenda itakuwa ni huu wa Samia na Magufuli. Utawala wa Magufuli wizi ulikuwa ni kwa wale aliowaruhusu yeye. Wewe kama hujaruhusiwa, ukaiba, utaona cha mtemakuni. Kwa hiyo ulikuwa ni wizi wa wateule wachache.

Utawala ambao ulikuwa na kiwango kidogo cha rushwa na wizi, ni utawala wa Nyerere na Mkapa.
 
Duh Mkapa huyu wa IPTL,Kagoda,meremeta, kiwira ,Rada n.k ur not serious wewe
 
Kila mwenye akili timamu anajua kuwa Magufuli alikuwa Rais wa hovyo na mwovu. RAIS ambaye alikuwa anakiri hadharani kuwa pesa za serikali ni pesa zake. Alikuwa akisema "pesa zangu". Alikuwa na uhuru wa kuchota mihera ya serikali na kuigawa kwa siri na hadharani ili ajiimarishe kisiasa.

RAIS Samia ni Rais muadilifu haswa , tatizo ni kwamba amekuwa dhaifu kupitiliza.

Kitendo cha kuongea na waajiriwa wake wezi na kuwaambia wampishe nao kumgomea hiyo ni dhahiri kuwa Samia ni dhaifu dhaifu dhaifu. Alishindwa hata kuwataja majina au vyeo vyeo.

Na wasaidizi wake bila shaka hawajitambui au yawezekana nao wanakula pamoja na mafisadi. Walishindwa hata kuandika barua za kuwatengua ambao Samia alisema wampishe.

Power ya Samia ni ndogo sana yawezekana ni ndogo kuliko ya OCD wa wilaya ya Kaliua au Ubungo.
Unaweza kututajua uovu wa J.P.M Aliokufanyia Hadi uko radhi kuongozwa na mtu dhaifu sana kwa kauli Yako

Pia ukumbuke hii ni nchi sio kikundi Cha vikoba na Rais ni mkuu wa majeshi a.k.a Amri jeshi mkuu

We kwa akili Yako ya uchawa unataka kama nchi iwe na amri jeshi dhaifu kweli una akili kweli
Mnapenda na kuchukia Hadi mnakuwa vipofu
 
Bado hamjachoka na propaganda za kumchafua marehemu?
Kila mkipima mnaona bado anapendwa hivyo kuongesa kasi ya uongo wenu.
Eti Rais wa ovyo na mwovu.

Kipindi cha Magu ndiyo sheria ziliheshimiwa kupita vipindi vyote! Siyo sheria za barabarani, sheria za kulipa kodi, sheria za kazi nk. Ndiyo kipindi nilishuhudia hata mahakimu wanahakikisha kesi zinaisha ndani ya muda waliowekewa! Polisi walikuwa na nidhamu! Ukiingia ofisi za umma unasikilizwa. Magu tutamkumbuka daima.

Akiongea dunia inasikiliza. Siyo Afrika tu, Ulaya na marekani, walifuatilia mwamba anaongea nini. Ni kutokana na umakini wake na kutokubali kuchezewa chezewa. Watanzania wengi walimpenda ndiyo maana alichaguliwavkwa wingi kwenye uchaguzi ukiacha hizo porojo zenu za wizi wa kura za akina Mdee!
Ni kweli kwamba hata nje ya Tanzania, watu walikuwa wanafuatilia sana matamko yake, hasa watu wa makampuni yaliyowekeza Tanzania. Lakini nje ya Tanzania, wengi walikuwa wanamwona kama mtu ambaye hakuwa sawasawa. Kwa hiyo ufuatiliaji wa hotuba zake haukuwa kwenye positive side.

Kuna wakati marehemu alitoa hotuba, kesho yake, nikiwa Australia, kuna kampuni ilipanga ku-raise pesa kwenye stock market ya Sydney kwaajili ya mradi wa makaa ya mawe Mbinga (Ruvuma), shughuli ilisitishwa ghafla, watu wakaambiwa, 'Tanzania president has turned another Mugabe. Tanzania is no longer safer for foreign investments'. Zoezi likasitishwa moja kwa moja. Mpaka leo, huwezi ku-raise funds kwaajili ya kuwekeza Tanzania, na sababu kubwa ni kwamba japo utawala umebadilika, sheria hazijabadilika.
 
Nitajie taifa ambalo limeendelea bila kuwa na Kiongozi mwovu!
Nchi nyingi za Ulaya pamoja na Marekani zimeendelea kupitia unyang'anyi wa mali za mataifa masikini hasa barani Afrika.
Hakuna taifa lililoendea kwa viongozi wake kucheka na kima!
Msiwe mnalishwa maneno ya mitaani bila kutafakari. Marekani ilipora mali gani ya Afrika. Hata leo hii Marekani inapora mali gani toka Afrika?
 
Kuhusu yeye alikuwa wapi kipindi cha Jiwe hilo haina haja kupatiwa majibu
Vice president kwa katiba yetu ni kama sanamu tu. Hana authority ya aina yotote
Kwa nini asingejiudhulu
 
Tulishawaomba ushahidi wa uovu wake, cha ajabu kinachoelezwa ni tetesi tu na uzushi.
Hebu tuambieni kwa ushahidi halisi (vivid evidence) kwamba alikuwa mwovu

Ushahidi wa mwenye udhaifu najua uko dhahiri hata watoto wadogo wanaweza kuuonesha
1.5T ilipotea aliyeonyesha upotevu akatumbuliwa.
 
1.5T ilipotea aliyeonyesha upotevu akatumbuliwa.
Hilo tu ndo maana nasema wengi wenu humu ni bendera fuata upepo izo hela Kuna sehemu imetajwa kuwa magufuli kachukua
Hata Sasa watu wako bize kumsema Rais Samia Hana kosa hata Moja

Tujifunze kulaumu tasisi sio mtu binafsi kama watz inabidi muda wote tuilaum CCM ndo tumeipa dhamana ya kuiongoza nchi hii wao ndo wachukue hatua
 
alikuwa anakiri hadharani kuwa pesa za serikali ni pesa zake. Alikuwa akisema "pesa zangu".
Wewe ni ugomvi na chuki binafsi kwa Magufuli vinakusumbua.

Ulishawahi kusikia neno 'Mabilioni ya JK' ?
Au pesa za mama Samia je?..Mama amemwaga pesa!
Wakati mwingine tuache mihemko kwenye kujenga hoja.
 
Duh Mkapa huyu wa IPTL,Kagoda,meremeta, kiwira ,Rada n.k ur not serious wewe
Kampuni ya IPTL ilianzishwa wakati wa Mkapa lakini wizi ulikuja kutendeka wakati wa awamu ya Kikwete. Halikadhalika Kagoda na Meremeta.

Kwenye Radar, upo sahihi. Radar, uchafu ulifanyika wakati wa Mkapa ukimhusisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Kuja kujulikana kuwa kulikuwa na madudu yale ya rushwa, ilikuwa ni wakati wa Kikwete.

Kiwira upo sahihi. Tena ilihusisha familia yake. Japo ilipokuja kugundulika, Mkapa aligomba sana dhidi ya familia yake ma kuagiza Kiwira irudishwe Serikalini. Swali, ni je, hakujua? Au hakujua ilikuwa hairuhusiwi? Lakini hakukuibiwa pesa Kiwira bali mgodi ulinunuliwa na familia yake. Ni wakati ambao mashirika mbalimbali ya umma yalikuwa yanauzwa. Kosa lake kubwa lililokuwa likimwandama ni kukiuka maadili ya ofisi ya Rais yanayozuia Rais kufanya biashara akiwa bado ni Rais, lakini haikuwa wizi.
 
Back
Top Bottom