Hayati Magufuli anapotajwa kuwa Shujaa wa Afrika, maana yake nini?

Ebu tuambie mbeya katufanyia Nini?
 
Hoja inanguvu sana, ni kweli bora abaki aitwe shujaa wa tz, mashujaa wa historia fulani ambayo inachangia ustawi wa eneo, waweza kuwa shujaa wa bara, kanda, Nchi, mkoa, kabila, nk. Sifa ambazo hastahili ni kumchoma moto mbele ya Mungu.
 
Ni kweli lakini unapomsema marehemu ANAKUSIKIA?.
 
Magufuli enzi za uhai wake alionyesha mapungufu ya wazi alisema ataufuta upinzani na kweli aliufuta bungeni na nje ya bunge aliwasumbua sana wapinzani mpaka kutaka kuwauwa hizi sifa wanazompa ni unafiki uleule wa kumsifu marehemu hata akiwa jambazi
 
SHUJAA- ni mtu anaeshinda jambo fulani, mfano vita au ni mtu anaelikabili jambo lolote kwa ujasiri bila woga, mfano kudhiti ufisadi, madawa na nk..

magufuli anatajwa shujaa wa afrika coz kwa kipindi hiki hakuna rais afrika alieweza pigana kishujaa vita za kifisadi, madawa na nk.. kumfikia yeye.
 
Mi mwenyewe nilikuwa najiuliza swali hilo hilo
 
Magufuli enzi za uhai wake alionyesha mapungufu ya wazi alisema ataufuta upinzani na kweli aliufuta bungeni na nje ya bunge aliwasumbua sana wapinzani mpaka kutaka kuwauwa hizi sifa wanazompa ni unafiki uleule wa kumsifu marehemu hata akiwa jambazi
Sasa upinzani unatofauti gani na genge la wahuni? Na msimamo wetu bado uko palepale
 
Usisahau hawa
1.walio tekwa au wenye ndugu walio tekwa na kuteswa
2. Ndugu wa walio potea hadi leo hawajulikani walipo
3.walio pigwa risasi pamoja na ndugu zao
4.ndugu wa wale tulio ambiwa ni wakimbizi wa kwenye maroba ufukweni bila uchunguzi
5.walio bambikiwa kesi na kulazimishwa kukiri makosa na kulipa faini ili kesi ziishe
5.walio nyang'anywa pesa zao kwenye account za bank
5.wafanya biashara na matajiri walio kuwa wanalazimishwa kutoa pesa na wakikataa wanatishiwa kupewa kesi za uhujumu hadi wengine kuhama nchi
5. Walio vunjiwa nyumba zao bila fidia
6.walio ibiwa kura zao kwa mtutu wa bunduki
7.watumishi ambao hawajapanda madaraja hadi sasa tangu 2014
8.wakulima wa korosho mtwara wanajua
9.wapemba zanzibar walio pigwa na wengine kuuawa kipindi cha uchaguzi
10.kagera ambao fedha zao za maafa zilibadilishiwa matumizi wakaainshiwa kukejeliwa
11.wanao daiwa na bodi kubadilishiwa % za makato kinyume na sheria
12. Wastaafu ambao wengine wana miaka 5-10 tangu wastaafu na hawajapata pensheni hadi sasa
13.wakenya walio chomewa vifaranga na kutaifishiwa ng'ombe zao
14.wasio pendezwa na lugha za chuki za kutugawa mf. "Msipo niletea fulani sileti maji" utadhan watu wa eneo hilo hawalipi kodi hivyo hawastahili maendeleo

yapo mengi sana sana pamoja na kwamba mazuri yapo pia hasa katika ujenzi wa miundo mbinu yaani hapo nampa 85%
 
Ingependeza zaidi kama Jiwe angeitwa shujaa wa Chato,alipeleka maendeleo na kuwaunganisha watu wa Chato.Huku kwingine alipeleka miundo mbinu kwa ajili ya maslahi yake binafsi!
 
Ingependeza zaidi kama Jiwe angeitwa shujaa wa Chato,alipeleka maendeleo na kuwaunganisha watu wa Chato.Huku kwingine alipeleka miundo mbinu kwa ajili ya maslahi yake binafsi!
Kwani Chato ipo katika ardhi ipi?
 
Rudi hapo # 5 nitajie hao unaowaita wafanyabiashara na matajiri halafu nielezee vyanzo halali vya utajiri wao. Kama haujui endelea kukaa kimya
 
Sasa upinzani unatofauti gani na genge la wahuni? Na msimamo wetu bado uko palepale
Kama unadhani nchi itaendelea kuendeshwa kibabe kama wakati wa Magufuli ni bora uhame mapemaaa! Kifo chake kina kusudi maalum, Mungu si Mpàmbe hadi aone mambo kwa jicho la kishabiki kama wewe.
Tunza maneno haya.
 
Moja ya kigezo cha mashujaa ni kuunganisha jamii na kuheshimu utu. Katika kampeni za uchaguzi Magufuli alikuwa akitamka wazi kuwa hakupeleka na hatapeleka maendeleo kwenye majimbo ya Chadema. Hapo vipi wandugu.
Mshana Jr:Wewe utakua umemuua presida wetu aise btw natamani kuona nyuzi yako related to his death I am sure you have sth to tell.
 
Magufuli R.I.P sio shujaa wa Afrika na hana hata chembe ya kuwa shujaa wa Afrika kwa lipi na kafanyia nini Afrika?
 
Africa inamuomboleza shujaa huyu,vyombo mbali mbali vinataja sifa zake.
Ameonyesha viongozi wa Africa jinsi inavyowezekana kuendelea bila kuitisha msaada.
Rais aliyependa watu Maskini.
Rais alieleta kasi kubwa ya maendeleo.

Inajulikana kila kona ya Africa alikua mchapakazi .
Na tazama news sehemu mbali mbali Africa si wacongo,uganda ,kenya Zambia,
n.k wanaomboleza.
Huyu baba alipendwa acheni joke.
Mlitaka alete Africa nini zaidi ya kuwa mfano bora?
Africa tuna uhuru tayari,na kila nchi ina Rais wake,wetu kupendwa inamaanisha alikuwa mfano bora,kiongozi shupavu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…